Nyafwili
JF-Expert Member
- Nov 27, 2023
- 4,240
- 10,561
Bwana MAPESA amesema biashara yake imeshuka baada ya ndoa.
Bwana MAPESA anamiliki maduka makubwa matatu ya biashara ambapo bidhaa za nyumbani na mahitaji mengine hutolewa, biashara ambayo alikuwa akifanya akiwa mtu mmoja(, bila kuwa na ndoa Kabla).
Biashara Ilikuwa Inaendelea vizuri sana Kwa miaka Kadhaa. Lakini baada ya kufunga ndoa, hakuweza kueleza kilichokuwa kinaendelea, ni ajabu kwamba biashara Yake Ilianza Kuporomoka gafla, kwa sasa kuna duka moja tu lililosalia na bidhaa chache, mmiliki wa duka ameshaanza kumpa taarifa ya kuondoka kwenye hicho chumba alicho panga.
Kuzorota kwa hali, amesema anaota ndoto za kutisha usiku tangu aoe.
Bwana MAPESA anauliza!! Je, hivi vyote ni sawa au bahati mbaya?
Maisha ni zaidi ya vitu vya kimwili, tayari tuna mtoto mmoja wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu.
Nukuu:- Biblia inasema alichounganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe. Yeye ambaye anapata mke, anapata kitu kizuri na kupata fadhili kutoka kwa bwana... Je kwa nini mimi Bwana MAPESA yananikuta haya??
Bwana MAPESA anaendelea Kusema nina mzigo mkubwa sana wa mawazo, na napanga Kujitenganisha na Mke wangu ili nione je, maisha yataludi kama ilivyo kuwa mwanzo kabla sijaoa?
Anaendelea kusema Hatujaangalia au Kuchunguza Kiroho kuhusu Jambo hili,
Lakini bwana MAPESA, bado Anaendelea kujiuliza kuwa mke wake ni mchawi? Au mke wake hana nyota ya biashara?
Bwana MAPESA alisema kama sivyo kwa nini imekua ghafla hivyo?🥴🥴
Mimi kama Nyafwili, Napiga vita Talaka/Upande wa Ndoa, kutokana na dini yangu. ✍️✍️.
Mwana Jf, Unatoa Maoni Gani kuhusu bwana MAPESA na kadhia hii aliyo nayo kwa sasa?