Anataka kuwa mke bora baada ya kunidharau

Anataka kuwa mke bora baada ya kunidharau

Wanawake wengi hawapendi au kujishughulisha na kitu cha kuingiza hela mpaka either aolewe halafu aachike au azalishwe na mwanaume na kumkimbia hapo ndo atakumbuka ma ex wote na anaweza akafanya biashara ila ukimkuta ndo bado ni slay queen wanakuwa na dharau na nyodo pamoja na tamaa yakiwakuta wanashtuka kumekucha walikuwa wanaota.
Akisikia umepata za mboga anarudi
 
Kwa hiyo jumla ni miaka 15? Acheni kuwazeesha watoto wa watu. Subiri haya mnayofanya watafanyiwa watoto wenu wa kike mtaona jinsi roho inauma. Karma
Mkuu, usitishike na miaka 10, unaweza kuta walianzia form 1 demu wake. Sasa chukua 6 years secondary na 4 years university. Hapo kapotezewa muda?
 
S
Tulidumu karibu miaka 10, nia yangu ilikiwa ni kumuoa ila baada ya kukamilisha mipango niliyojiwekea, ilipobaki miezi michache tuoane akanikalisha chini akaniambia kuwa hawezi kuendelea kuwa na mimi.

Ikabidi niheshimu mawazo yake japo roho iliniuma mpaka kufikia hatua nikawa napata maumivu kwenye moyo.

Nakumbuka kuna siku nilikuwa namfuatilia kwenye facebook nikitamani kujua aliyenipiku ananini kunizidi, nikakuta kamposti jamaa fulani mfupi kapiga picha mbele ya rav 4, roho iliniuma sana na ndo ilikuwa mara yangu ya kwanza kukosa usingizi mpaka asubuhi, na kiherehere cha kumfuatia kikaishia palepale.

Baada ya kupita miaka mitano, Mwaka jana siku moja napeleka mzigo wa mteja mara simu ikaita kuchek namba ya airtel, kupokea anasema mimi I, nikamuambia mimi siongeagi na wake za watu akasema hajaolewa.

Akasema amenimiss anatamani kuniona tukapanga tukakutana, nilikuwa na hamu ya kuona maisha anayoishi,
Tukaenda anapoishi ni chumba kimoja kidogo kina kitanda tu na jiko la mkaa, amepauka amekonda. Akawa anampa mtoto kipande cha tikiti maji.

Hana kazi anategemea elfu 50 ya malezi ya mtoto anayopata kila mwezi kutoka kwa baba wa mtoto. Yenyewe aliipata kwa mbinde kupitia ustawi wa jamii.

Akanielezea kuwa yule mwanaume alikuwa ameoa ana watoto wa 3 na amezalisha wanawake kibao.

Akaniomba numpe nafasi awe mke bora mi nikawa namcheki tu alivyopauka.

Hivi kweli nipambanie maisha mpaka hapa nilipo alafu nioe mwanamke mwenye mtoto tena aliyenidhau.

Hakikisheni mkiacha mtu mnaenda kwa aliye bora zaidi. Ni hesabu rahisi tu.
Sasa miaka 10 yote hiyo mlikuwa mnachunguzana nini
 
Kwa hiyo jumla ni miaka 15? Acheni kuwazeesha watoto wa watu. Subiri haya mnayofanya watafanyiwa watoto wenu wa kike mtaona jinsi roho inauma. Karma
Umesoma ukaelewa lakini? Demu mwenyewe ndiye aliemkataa jamaa sasa wewe unamlaumu vp jamaa
 
Biblia yangu inasema usimwache mwanamke mchawi aishi. Braza piga chini asee. Gonga mvinyo furahia maisha. Hicho ni kisasi cha Mungu. Mungu amekupigia maadui zako usiwaonee huruma wewe kandamiza msumari nchi 6 kwenye kidonda.
 
Mwanamke hawezi kukaa na MTU kwa miaka 10 Kama hampendi,Sema alihisi muda unamtupa mkono ndio akaona atafute mtu amuoe apate heshima ya ndoa bahati mbaya akaangua pua..ajali kazini
Kwahiyo mkuu hapo akubali kuwa contingency plan [emoji23][emoji23][emoji23], mnafurahisha kweli. Angekaa chini kipindi kile na kudadavua matendo yake kama anaishi kama mtu mume au kibachelor, sio kujirahisisha halafu useme ninacheleweshwa kuolewa. Wangapi leo hii ndoa zimevunjika wanaishia kupata mtu mwingine na kuanza kuishi kwa sogea tuishi huku wakikataa ndoa. Msimwingize jamaa katika majaribu na machungu tena, tabia haijabadilika kwahuyo mwanamke.
 
Kwa mazingira yoyote yale, Mimi siwezi kurudiana na ex, na kwa sababu hizo hizo huwa simshauri mtu kurudiana na ex wake.

Japo mleta mada ulitaliwa kuelewa mahitaji ya huyo mwanamke kipindi hiko, Miaka kumi unajipanga jamani na mbususu unakula, sio fair kabisa. Mahitaji yako yalikua kujipanga, mahitaji yake yalikua ninini? Hivyo ni salama kusema kuharibikiwa kwake na wewe umechangia.
 
Ndio tumuulize huyu mwenzenu miaka yote hiyo kwa Nini alikuwa hamuoi?na anadai anmpenda?
Ukiingia kwenye maisha kwalengo la kujijenga na mwanamke, ndugu kwakiasi kikubwa asingeweza kufika hapo alipo. Hivyo ukimwona mwanaume anajipanga muda mrefu, either ukubali kumwamini kwakuangalia matendo yake au achana naye. Ndoa sio mapenzi tu, kuna majukumu makubwa sana ambayo jamaa asingeweza kuyatekeleza huyohuyo mwanamke angemdharau.
 
Back
Top Bottom