Anataka tuachane na tayari nimekwishalipa mahari kwao na mipango ya ndoa ipo

afadhalli bomu limekulipukia nje ya nyumba ya ndoa, japo kuna majeraha.
lakini lingelipukia ndani ya nyumba ya ndoa Lazima lingeleta madhara makubwa zaid Mathalani mafarakano , uharibifu, pengine maafaa na mahangaiko kwa wanafamilia

Umeepushwa Jambo apo
 
Acha aende mzee.. muache aende usimlazimishe mshukuru MUNGU ni mapema sana amekupiga hilo tukio.
Itakuchukua muda kidogo kusahau yale mazuri mlipo kuwa pamoja, lakini utamsahau na utajilaumu kwanini ulikuwa unateseka juu yake.
 
Mpe uhuru afanye anachotaka
 
Hapo kwenye paragraph ya mwisho usiseme huyu mpenzi wangu , Sema huyu aliyekua mpenz wangu hatukuwahi kuwa na ugomvi


Pole mkuu
 
Kaka inabid utambue kuna wanawake wanakua na sisi ili kutimiza ndoto zao au kupata support ya kusogeza muda ila punde wanapotimiza ndoto zao hutaka kuondoka maishani mwetu maana hatukua chaguo lao namba 1 au si aina ya mwanaume aliyetamani kuishi naye kwenye ndoa.

Mwache aende, tayari yupo mtu anaempenda zaid kwa sasa.
Ongea na wazazi wake kwa amani ukitaka mali zako na wakiweza kukulipa pokea achana nao, ikishindikana waachie.

Anza maisha mapya na usimpokee hata ndugu zake wakijarb kumrudisha akawasikiliza.
Huyo ashakuonyesha humfai kua mumewe ukiforce utagongewa sana na mwisho atakuja kukuachia watoto.

She better https://jamii.app/JFUserGuide off.
 
Hapo hakwenda kwa bibi yake wala kwa rafikiake. Huyo na mtu wake mwingine kimapenzi. Huyo mtu yupo hapo hapo anapoishi. Na ukizingatia muda mwingi mko mikoa tofauti,basi huyo mtu wake ndio amejenga ukaribu na mazoea kwa kipindi chote ulicho mbali nae.

Hata sasa hajaenda mbali yuko nae karibu hapo hapo. Alienda kwa huyo mtu wake ili wakashauriane aolewe na wewe au yeye huyo atamuoa?. Mpaka sasa kadanganywa tayari kwamba atamuoa,ndio maana kaona avunje uhusiano na wewe kabla ya kufika kwenye ndoa. Ksbb anampenda huyo mtu wake kuliko wewe.

Ushauri kwako. Washirikishe ndugu wa pande zote kwao na kwako waambie hali halisi mchumba wako aliyokuambia. Na uwe imara wewe sana. Waambie ksbb yeye mwenyewe kataka hivyo na iwe hivyo. Muhimu kwako,usimfuatilie tena,achana nae hata usiwe na mawazo nae.

Pia usifanye haraka kuweka mbadala wake. Tulia. Kipindi hili ndio kipindi cha kupiga sana kazi kujiongeza kipato,ksbb hawa wenzetu "ke" maamuzi yao kuna uwezekano huyo kampendea kipato chake kilicho zaidi ya wewe. Soo komaa piga kazi,panga mipango yako vizuri. Hiyo hela uliyoitenga kwa ajili ya purukushani za ndoa nunulia uwanja sehemu nzuri,anzia ujenzi.

Kuwa makini ksbb huyo aliemkimbilia anamtumia tu. Hana nia nae kabisa. Soo akimchakaza na kumtema,huyo binti anaweza kurudi kwako akipiga na magoti. Na hapo ndipo unapoonekanekana udhaifu wa adamu,udhaifu wa Samson. Upumbavu wa sisi wanaume wa sasa. Uwe serious asijaribu hata kukufikia kwa njia yoyote. Hakufai. Majuto yanamsubiri huko mbele.
 
Huu ushenzi umenikuta pia last year,
Tena mimi alikua demu wangu tangu primary 2009 uko tumeish sanaa tumepanga vingi tunakarbia kutimiza ndoto bahat mbaya tu mwenzangu kawah kujipata miez michache kabla yangu kaniomba tuachane. I guess alitaka ale vibunda vyake mwenyewe kama walivyo wabinafsi viumbe hawa.

Alivonyau ananiwish baraka sa mwaka mpya, Tuwaogope sana hawa Viumbe.
 
Amekupunguzia matatizo achana nae
 
Umempenda lakini kakukataa sasa utafanya nini zaidi ya kukubaliana nae? Mpe nafasi labda kaona kuna mtu bora zaidi yako acha aende hata wewe utapata mwingine atakaekuona bora.

Kuna muda kwenye mahusiano mtu anakua haoni thamani yako kabisa unachotakiwa kukifanya ni kuwa mpole tu na kumuacha aende muda utaaamua ipo siku atakumbuka uwepo wako na yeye atapitia maumivu unayopitia sasa maana hakuna mtu bora kuliko mwingine hapa duniani.
 
Hiki suala la kutoa mahari wanaume hardcores wote tulishalikataa wewe ulikua wapi? Dai pesa yako uliyotoa mahari achana na mwanamke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…