Anatropia Lwehikila awashukia wabunge waliodai kunyanyaswa kingono, asema wanajidhalilisha kutojua wapi pa kupeleka malalamiko yao

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Anaandika Anatropia Theonest Lwehikila (Mbunge wa Viti maalumu Segerea).
_________________
Somo la bure kwa wanawake wenzangu hasa wanaokihama CHADEMA. Endeleeni na tuhuma bandia dhidi ya chama kinachojua kilipowatoa. Leo tumependeza, tunanukia, shukrani halisi zimekuwa mateke.

Semeni yote mtakayo lakini aibu zaidi ni kina mama watu wazima (tena wabunge) kusema hadharani mmedhalilishwa kingono. Nafasi ya ubunge iliwapa exposure ya kujua wapi mpeleke malalamiko yenu. Mahakama mnazijua, Ustawi wa jamii mnapajua, hata TWPG viongozi wao mnawajua. Ilikuwaje mkae kimya miaka yote 5? AIBU YENU.!
_
Hata kama ingekuwa kweli, mnasifa gani za kuendelea kuwa viongozi kama hamuwezi kujisaidia. Mtawezaje kusaidia mabinti na wanawake wengine wanaonyanyasika wapate msaada kama ninyi wenyewe mmeshindwa kupata msaada? Mmechekesha kweli.

Nawasihi acheni kujidhalilisha na kuwadhalilisha wanawake wenzenu. Acheni shutuma za kitoto. Hao wanaowaandikia hizo 'statement' wanawapotosha sana.

Jamii inategemea kuwaona mmestaarabika baada ya kumaliza Ubunge wenu wa Viti Maalumu mkijiandaa kwenda kugombea majimboni. Sasa kama mnadai mmedhalilishwa kingono na mkakaa kimya kwa miaka mitano, mtawezaje kuwasemea wananchi kero zao? Mmeshapoteza point.

Endeleeni kusema uongo iko siku mtahitajika kupeleka ushahidi mahakamani. Badilikeni nawaonya.!
 
Wale akina mama wamejitoa ufahamu.
Walikuwa wapi siku zote kutoa tahadhari juu ya kunyanyaswa kingono? , ina maana walikubali kunyanyaswa kingono ili waendelee na vyeo?

Au ina maana hata huko wanapokwenda wakinyanyaswa tena kingono watavumilia ili mradi kulinda vyeo?

Na je akitokea mtu akataka awanyanyase kingono watakubali ili mradi wapate cheo watakubali ILA tu watamsema baada ya muda wa hicho cheo kuisha?

Kwa kweli wamezitia aibu familia zao, masikini wanawake wale walioshikwa akili na CCM


=====
Wabunge wakiolalamikia kuwa na unyanyasaji wa kingono ni Suzana Maselle (Mwanza) na Joyce Sokombi (Mara) ambao wametangaza kuondoka CHADEMA mara baada ya kumaliza kipindi chao cha Ubunge, Juni mwaka huu

Wamesema hayo Mei 22, walipokuwa wanaongea na waandishi, na kusema sababu nyingi za kuondoka kwao ikiwemo unyanyasaji wa kingono ambao hutokea kwa kuwa uongozi kwa asilimia kubwa unashikiliwa na wanaume.
 
Hata confidence hawakuwa nayo wakati wakiongea, walikuwa wanaongea huku wakitetemeka kudhihirisha walichokuwa wakiongea ulikuwa uongo mtupu.

Halafu kusema wamedhalilishwa kingono, naona wamejidhalilisha wenyewe, nani huyo wakutamani watu wazima wa umri ule?

Ni vyema wanaokimbia CDM wakatunga uongo utakaotunza heshima zao, sio kutunga uongo utakaowavua nguo wenyewe mbele ya jamii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zamani kidogo nilikuwa nilikuwa nilifikiri ni mtu ukishakuwa mbunge automatically utakuwa na akili.

Unakubali katumika kirahisi hadi unatia kinyaa
Wewe ni sawa na mie, na sio wabunge tu bali hata viongozi wote kwa ujumla (mawaziri, ma rc, dc nk)

Kwa sasa nimegundua kumbe kuna watanzania wengi sana wapo smart kuwa viongozi kuliko hao waliopewa dhamana.

Demokrasia inachelewesha maendeleo barani Afrika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo naye naona mkuyati wa DJ umemkolea, maana Mbowe ni kama mfalme Mswati... Mara anende na Joyce Dubai, mara awaferengue hapa hapa bongo. Hao wanaoona kuwa DJ yupo sahihi kuwatafuna bora wake kimya, wenzao wamechoka kudhalilishwa!
 
Hizi kauli zao zinawatokea puani baadae. Chadema mna matatizo makubwa ya ndani mnapaswa kujirudi. Mnaenda kuifanya NCCR chama kikuu cha upinzani kirahisi sana kwa ubishi wa kipumbavu.

Andaeni taasisi huru itakayo kusanya maoni ya wabunge, madiwani na viongozi waandamizi na baadae kutoa mapendekezo wazi na yafanyiwe kazi. Hata ukiwa nje utaona kuna wachache wamegeuka ndio wenye chama na wengine hawapewi kipaumbele.

Baada ya uchaguzi mkuu wapenda mageuzi na wanaharakati watasonga mbele na NCCR na kuwasahau. Acheni kujipa moyo na comments za kwenye social media ambazo haziwezi kuwapa hata udiwani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…