Anatropia Lwehikila awashukia wabunge waliodai kunyanyaswa kingono, asema wanajidhalilisha kutojua wapi pa kupeleka malalamiko yao

Anatropia Lwehikila awashukia wabunge waliodai kunyanyaswa kingono, asema wanajidhalilisha kutojua wapi pa kupeleka malalamiko yao

Watu wazima !!! ingekuwa WAMEBAKWA ! hilo ni suala lingine lkn mtu mzima kama ni kweli kumbuka UMETONGOZWA , ukakubali maisha yakaendelea.

Watu wamekutana shuleni, vyuoni, makazini na hata Bungeni, wakatongozana , wakakubaliana maisha yakaendelea!.

Kuja hadharani na kusema , maisha yaliendelea kule japo mimi sikupenda hali ile baada ya miaka 5 kupita huo siyo UUNGWANA nyamazeni .

Ni kujidhalilisha na kudhalilisha utu wa MWANAMKE , kuonesha mwanamke ni chombo tu hata awe MBUNGE hawezi kujisimamia pale anapoona POSHO.
 
Acha kuwabeza wenzako. Njaa ni hatari na inaua kuliko corona isipodhibitiwa. Suala la rushwa ya ngono (sextortion) ni la kimataifa fanya utafiti utajua sababu zake au wasiliana na watakupa uelewa. Bado CUF tunatafakari mchezo uliochezwa Ukawa Segerea
 
Awanyanyase nani sasa? Wenyewe sura nzito vizee waende zao bwana.Watu wazima ovyoo
 
Anatropia ni kimada wa John Mrema ambaye yuko makao makuu CHADEMA. Na yeye ni mnufaika wa ubunge wa 'VITU MAALUM' wa CHADEMA. Alilamikiwa sana mwanzoni alipopitishwa lakini nani angesikiliza na kumwondoa kiburudisho cha Mrema.

Achunge kauli, hakuna ambaye angeamini kwamba Sussane Masele ambaye ni mke wa Tumaini Makene angeweza kusepa na kuiponda CHADEMA.
 
Walidhalalishwajwe kingono na wenyewe wana Mabwana zao?.
 
Hata confidence hawakuwa nayo wakati wakiongea, walikuwa wanaongea huku wakitetemeka kudhihirisha walichokuwa wakiongea ulikuwa uongo mtupu.

Halafu kusema wamedhalilishwa kingono, naona wamejidhalilisha wenyewe, nani huyo wakutamani watu wazima wa umri ule?

Ni vyema wanaokimbia CDM wakatunga uongo utakaotunza heshima zao, sio kutunga uongo utakaowavua nguo wenyewe mbele ya jamii.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wameolewa wale Mkuu, na Wana Watoto.
 
Mishankupe yenyewe sasa inayosema imenyanyaswa kingono..hadi unacheka..

Ni Sawa na bar maid aseme kashikwa mkono na mteja..
 
Mbunge mzima unatumikishwa kwa kipindi cha miaka mitano, upo kimya mtu ambaye jamii tunaelewa unauelewa mbona wa Mambo ya kisiasa, kiuchumi na kisheria, mtu ambaye unahusika na kutunga Sheria za nchi, dah hii ni aibu na kujidhalilisha kiwango kikubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi kauli zao zinawatokea puani baadae. Chadema mna matatizo makubwa ya ndani mnapaswa kujirudi. Mnaenda kuifanya NCCR chama kikuu cha upinzani kirahisi sana kwa ubishi wa kipumbavu.

Andaeni taasisi huru itakayo kusanya maoni ya wabunge, madiwani na viongozi waandamizi na baadae kutoa mapendekezo wazi na yafanyiwe kazi. Hata ukiwa nje utaona kuna wachache wamegeuka ndio wenye chama na wengine hawapewi kipaumbele.

Baada ya uchaguzi mkuu wapenda mageuzi na wanaharakati watasonga mbele na NCCR na kuwasahau. Acheni kujipa moyo na comments za kwenye social media ambazo haziwezi kuwapa hata udiwani.

Sent using Jamii Forums mobile app
NCCR ipi hiyo unayoiongelea?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo hili limeota mizizi Chadema hata Lissu aliripoti twitter badala ya kuripoti polisi!
 
Wale akina mama wamejitoa ufahamu.
Walikuwa wapi siku zote kutoa tahadhari juu ya kunyanyaswa kingono? , ina maana walikubali kunyanyaswa kingono ili waendelee na vyeo?

Au ina maana hata huko wanapokwenda wakinyanyaswa tena kingono watavumilia ili mradi kulinda vyeo?

Na je akitokea mtu akataka awanyanyase kingono watakubali ili mradi wapate cheo watakubali ILA tu watamsema baada ya muda wa hicho cheo kuisha?

Kwa kweli wamezitia aibu familia zao, masikini wanawake wale walioshikwa akili na CCM


=====
Wabunge wakiolalamikia kuwa na unyanyasaji wa kingono ni Suzana Maselle (Mwanza) na Joyce Sokombi (Mara) ambao wametangaza kuondoka CHADEMA mara baada ya kumaliza kipindi chao cha Ubunge, Juni mwaka huu

Wamesema hayo Mei 22, walipokuwa wanaongea na waandishi, na kusema sababu nyingi za kuondoka kwao ikiwemo unyanyasaji wa kingono ambao hutokea kwa kuwa uongozi kwa asilimia kubwa unashikiliwa na wanaume.
Mdee sio mtu mzuri kabisa!
 
Anaandika Anatropia Theonest Lwehikila (Mbunge wa Viti maalumu Segerea).
_________________
Somo la bure kwa wanawake wenzangu hasa wanaokihama CHADEMA. Endeleeni na tuhuma bandia dhidi ya chama kinachojua kilipowatoa. Leo tumependeza, tunanukia, shukrani halisi zimekuwa mateke.

Semeni yote mtakayo lakini aibu zaidi ni kina mama watu wazima (tena wabunge) kusema hadharani mmedhalilishwa kingono. Nafasi ya ubunge iliwapa exposure ya kujua wapi mpeleke malalamiko yenu. Mahakama mnazijua, Ustawi wa jamii mnapajua, hata TWPG viongozi wao mnawajua. Ilikuwaje mkae kimya miaka yote 5? AIBU YENU.!
_
Hata kama ingekuwa kweli, mnasifa gani za kuendelea kuwa viongozi kama hamuwezi kujisaidia. Mtawezaje kusaidia mabinti na wanawake wengine wanaonyanyasika wapate msaada kama ninyi wenyewe mmeshindwa kupata msaada? Mmechekesha kweli.

Nawasihi acheni kujidhalilisha na kuwadhalilisha wanawake wenzenu. Acheni shutuma za kitoto. Hao wanaowaandikia hizo 'statement' wanawapotosha sana.

Jamii inategemea kuwaona mmestaarabika baada ya kumaliza Ubunge wenu wa Viti Maalumu mkijiandaa kwenda kugombea majimboni. Sasa kama mnadai mmedhalilishwa kingono na mkakaa kimya kwa miaka mitano, mtawezaje kuwasemea wananchi kero zao? Mmeshapoteza point.

Endeleeni kusema uongo iko siku mtahitajika kupeleka ushahidi mahakamani. Badilikeni nawaonya.!
Kwa hiyo hawa wanawake tayari weshaliwa kinguvu na wakatoa ushirikiano katika tendo hilo?
Wamepoteza sifa za kuolewa kama bado na kama wapo kwenye ndoa ni aibu ya familia na ukoo walio olewa.
Kwa jamii sisi tushawaelewa kwamba ni watu wasioweza kutetea haki zao wenyewe hivyo za wengine ndio kabisaaa kuingia choo cha jinsia tofauti.
Niwaaase kaeni mle hizo za kununuliwa na ni maandalizi yenu ya kupotea karika siasa za nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unawasahihisha au unawasemea tena ujinga acheni waondoke tu hata nikibaki mie nitakuepo. Bungeni nating
Aache kukurupuka. Anafanya makusudi kupotosha akijua nyumbu huwa hawatafakari. Wao ni kuzungusha mikono na kuunga mikono.

Hawakusema wamedhalilishwa. Bali walichosema ni kuwa "taratibu za upatikanaji viti maalumu chadema zinatoa mwanya wa udhalilishaji kingono"

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zamani kidogo nilikuwa nilifikiri ni mtu ukishakuwa mbunge automatically utakuwa na akili.

Unakubali katumika kirahisi hadi unatia kinyaa
Siku hizi jamii imechagua upumbavu kuwa style ya maisha.
Wapumbavu ndiyo wanachaguliwa na kushabikiwa kisiasa , kijamii, kitamaduni na hata kidini.
Mijadala hapa JF inajadiliwa kipumbavu zaidi kuliko hoja zenye mashiko ya kiakili nzuri, busara na hekima.
 
Back
Top Bottom