Anayedaiwa kulala na kula Serena kisha kutokomea aachiliwa huru

Anayedaiwa kulala na kula Serena kisha kutokomea aachiliwa huru

Unaweza kuta tangu waanze biashara hapa Tz hajawahi kutokea mteja kama huyu. Nafikiri kuanzia sasa wataanza kuangalia watu usoni
Kwa serena hii sio kesi ya kwanza, wapo wanasiasa washadaiwa mihela kibao, viongozi washawapangishia vimada wakagoma kulipa, hii ndio picha halisi ya uwekezaji tz unapigwa mchana kweupe na hamna msaada, ingekuwa dubai washakata kichwa siku nyingi
 
Tangu awali wangefungua kesi ya madai, hawa mameneja tunawatoaga wapi? Itabidi nikaombe kazi ya kufua mashuka hapo kuna hela za bure
Swali la kujiuliza hivi hotel kubwa kama Serena haina mwanasheria? Na kama yupo hakujua tangia mwanzo kama hili shauri ni la madai mpaka wakampeleka Polisi kijinai?
Hakika tuna watu wanaojiita wasomi maofisini lakini vichwani ni bure kabisa
 
😁 Baba wa mtu fulani na ni mume wa mtu fulani huyo..
sasa mpaka anakula hawakujua kuwa anakula nakulala na utaratibu si mtu huwa analipa kwanza ndo anatumia au vipi...?
Kenzy eh acha kuniaibisha mkuu. Hotel kubwa zote huduma hutolewa kwanza then malipo baadae(check out). Pia unatakiwa ufahamu kuna watu au taasisi wanapata huduma on credits then wanalipa baadae, mbona hili ni swala dogo ambalo kila mtanzania anapaswa kulifahamu bwana Kenzy?🤔🙄
 
Kenzy eh acha kuniaibisha mkuu. Hotel kubwa zote huduma hutokewa kwanza then malipo baadae(check out). Pia unatakiwa ufahamu kuna watu au taasisi wanapata huduma on credits then wanalipa baadae, mbona hili ni swala dogo ambalo kila mtanzania anapaswa kulifahamu bwana Kenzy?🤔🙄
mh! mambo yameshabadirika watu hulipia kulala kwanza nakula,na pia kama kama atafanya extra services hizo ndio hulipia wakati anatoka wewe ndio unaniaibisha!,by the way kila hotel na utaratibu wake lkn kwa utaratibu wa kutumia kwanza halafu alipe baadae ni utaratibu wa hovyo sana!
 
Bwana Kenzy umeshawahi kulala hotel gani kubwa nchini? Tuanzie hapo kwanza alafu twende with facts on service provision.
 
Bwana Kenzy umeshawahi kulala hotel gani kubwa nchini? Tuanzie hapo kwanza alafu twende with facts on service provision.
sijawahi ila navyofahamu ktk vyanzo vyangu vya hakika wanalipa kwanza zile night atakazolala na kama kuna gharama za chakula hulipia moja kwa moja.. so kuna inclusive services na extra hizi extra ndio hulipia baadae!.
utaratibu hutofautiana baina ya hotel na hotel hicho ndio nachofahamu.
 
mh! mambo yameshabadirika watu hulipia kulala kwanza nakula,na pia kama kama atafanya extra services hizo ndio hulipia wakati anatoka wewe ndio unaniaibisha!,by the way kila hotel na utaratibu wake lkn kwa utaratibu wa kutumia kwanza halafu alipe baadae ni utaratibu wa hovyo sana!
Wewe labda unaongelea lodge za mtaani ila kwenye hotels kubwa huwa wanahesabu bili hadi siku ya mwisho unayoondoka ndio unalipa.
 
Wewe labda unaongelea lodge za mtaani ila hotels kubwa huwa wanahesabu bili hadi siku ya mwisho unayoondoka ndio unalipa.
haha! ngoja nikuache kama ulivyo ila nikuambie ukweli waulize wenye hotel ndio huwa wanajua vichwa vya wageni wao walivyowasumbufu!.. ndio maana wakaweka utaratibu wakulipia kwanza ukiona kaenda kulipia wakati anatoka huwa ni extra charge labda alitumia vitu vyengine vya ziada!.. ndio maana nikaandika kama hao Serena wanamlipisha mteja bills zote siku anatoka basi ni utaratibu wa hovyo sana!.
 
Wewe labda unaongelea lodge za mtaani ila kwenye hotels kubwa huwa wanahesabu bili hadi siku ya mwisho unayoondoka ndio unalipa.
Siyo kweli...
Kwa mtu binafsi hupaswa kulipia malazi kabla ya kuingia. Gharama unazoweza kulipia mwishoni ni kama laundry, chakula na vinywaji.

Wanaoruhusiwa kupata huduma ya malazi na kulipia baadae ni taasisi za serikali, mashirika na makampuni kwa mikataba maalum.

Kwa case ya huyu mwamba wa serena kuna taarifa hatujaelezwa na lazima alifanya udanganyifu kupitia mkataba fulani wa malazi.
 
Mtanzania, Denis Mfumbulwa (44) anayedaiwa kujipatia huduma ya kula katika Hoteli ya Serena bila kulipa, ameachiwa huru katika Mahakama ya Mwanzo Kariakoo jijini Dar es salaam kwa sababu hakuna ushahidi wa kuthibitisha kama kesi hiyo dhidi yake ni ya jinai.

Mfumbulwa ambaye ni Mkazi wa Goba ameachiwa leo na Hakimu Gladness Njau wakati kesi hiyo ilipoitwa mahakamani hapo kwa ajili ya kusikilizwa.

Mapema Meneja wa Hoteli hiyo, Desdery Doto alifika Mahakamani hapo kutoa ushahidi ambapo alipoulizwa alidai Mshtakiwa alifika hotelini hapo na kupata huduma ya chakula na malazi bila kulipa na kisha akatoweka.

Kufuatia maelezo hayo, Hakimu Gladness Njau alimuachia huru Mshtakiwa huyo akisema “inaonekana asili ya shauri hili ni la madai na siyo jinai hivyo kama Mlalamikaji ataona inafaa afungue kesi ya madai”

Katika kesi hiyo Mshtakiwa Mfulumbwa anayeishi Goba Kulangwa anadaiwa kuwa Machi 6,2022 hadi Machi 28,2024 kwa nyakati tofauti katika Hoteli ya Serena Wilaya ya Ilala, Dar es salaam alijipatia huduma ya malazi na chakula yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 21 bila kulipa ambapo baada ya kupatiwa huduma hiyo alitoweka huku akijua kuwa kitendo hicho ni kinyume na sheria.

Akizungumza nje ya Mahakama Meneja Doto amesema yuko tayari kuendelea na kesi ya madai hivyo anasubiri nakala ya hukumu.

Pia, soma=> Alala na kula Serena kisha kutokomea bila kulipa deni la milioni 21, adakwa na kufikishwa mahakamani

Hawa machalii wa Moshi mbwembwe nyingi sana kumbe sanaa tupu..fuatilieni vizuri...lazima ni kule kule connection. Kama yule mzee asiyechana nywele 😂 😂 😂 😂
 
Back
Top Bottom