Anayedaiwa kulala na kula Serena kisha kutokomea aachiliwa huru

Kuna maelezo yanakosekana hapa. Sidhani kama ni mtu hohehahe amejitokea tu nyumbani na kwenda kufanya haya. Ni hoteli gani wataruhusu mtu kukaa siku zote hizo bila kulipa huku anakula na kulala?
Wateja wengine huwa wanatumia credit cards ambazo baada ya muda malipo yana bounce kutokana na insufficient funds!!
 
Polisi aliyeandaa kesi hiyo Dpp atafutwe alishindwaje kutambua hiyo ni madai
Naona walikua wana force iwe jinai ili mteja aogope,na kosa najua waliweka la kujipatia chakula na malazi kwa njia ya udanganyifu, sema hakimu kasanuka na kuitupa kesi kwenye madai!!
 
Hapo umeshahukumu bila kusikiliza pande zote mbili?
 
Hotel kubwa hivi hotel ya hadhi haina mwanasheria mbobezi kweli katika maswala ya sheria, mimi sijasomea sheria lakini its very obvious hiyo kesi ni kesi ya madai inakuaje kesi ya jinai. Manager wa hotel nae chenga
 
Yani mteja akae tangu 2022 mpaka 2024 bure na wanasubiri kumdai huu utaratibu wa wapi, huyo manager wa hotel hafit hiyo position anatakiwa jiuzulu
 
Wewe labda unaongelea lodge za mtaani ila kwenye hotels kubwa huwa wanahesabu bili hadi siku ya mwisho unayoondoka ndio unalipa.
Ni prepaid bro, aidha kabla hauja check in ama wakati una check in pale reception... Ni wageni wachache sana wanapata access ya kuingia bila kufanya malipo ya kabla (kutokana na sababu zao) kama mtandao kusumbua wakati wa malipo

Unajua kuwa hotel zina sera ya kumtaka mteja aache details za Kadi iliyo na kiasi cha pesa... ili ukisumbua watu wanavuta pesa kutoka kwenye kadi..??

Unajua kama kuna hotel zina sera ya malipo ya kabla angalau 25% ili kulinda malazi yako uliyo reserve kabla ya kufika (arrival/check in) ili ikitokea kama unafanya last minute cancelation basi pesa inafidiwa kama hasara..???

So kuhitimisha hotel zina sera za malipo ya kabla, lipa ndio uingie chumbani
 
Uko sahihi kuna kitu nilichanganya,kuna kipindi nilikuwa naishi kwenye mahotel then ikawa siku ya kucheck out tunahesabu bills zote kisha wanalipwa lakini nimekumbuka kumbe ilikuwa ni kwa sababu ya udhamini wa kampuni niliyokuwa nafanyia kazi.
Ila kwa mtu binafsi ni kweli hawawezi kukubali maana akitoroka hawana pa kumpata.
 
Hakuna kesi hapo.
 
sasa mbona ulikuwa unanishupalia mmbichwa...??๐Ÿ˜‚
 
Bila shaka hakimu ameamua hivyo ili kuwezesha hotel kuweza kupata malipo yake. Maana kama angeendelea na jinai kisha mhusika akafungwa mdai hawezi kuja tena kufungua kesi ya madai maana atazuiliwa kuwa kipengele kuwa kesi ilishaamuliwa tayari.
We huelewi nini? Nature ya kesi sio ya jinai bali ni ya madai .hakimu hajaamua kumuachia huru kwa kutaka au kupenda kwake au kwa kutoka kumsaidia mtu fulani bali ni kwa matakwa ya sheria. Ata angeamua kuendesha kesi kama ya jinai akamfunga jamaa ,uko mbele jamaa angekata rufaa na kutoka .jifunze kuelewa kilichoandikwa.
 
Ngoja niingie mitandaoni na mimi nichague moja kali kuizidi Serena ili nile bata kiaina... ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ