Anayedaiwa kutengeneza radi auawa na wananchi

Anayedaiwa kutengeneza radi auawa na wananchi

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2009
Posts
16,908
Reaction score
19,123
Katavi. Baraka Said (30) mkazi wa kijiji cha Mtisi halmashauri ya Nsimbo ameuawa na wananchi baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali kwenye paji la uso na kupigwa na kitu kizito kisogoni akituhumiwa kujihusisha na ushirikina wa kutengeneza radi.

Akizungumza na wanahabari leo Januari 29, 2022 kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi, Sylvester Ibrahimu amesema tukio hilo limetokea Januari 24, 2022 saa 12 jioni kijijini hapo.

Amesema wananchi hao walimtuhumu marehemu kutengeneza radi iliyompiga Anjelina Revocatus (16) mkazi wa kijiji hicho na kusababisha kifo chake wakati anatibiwa hospitali ya rufaa Mkoa wa Katavi.

"Watuhumiwa nane wamekamatwa,John Mayonjuwa, Mashaka Mathias, Sele Richard, Revocatus Reymond, Julias Dalali, Hawa Rashid, Agnes Rashid na Tausi Abdu. Upelekezi ukikamilika watafikishwa mahakamani," amesema Ibrahimu.

Katika tukio jingine Ibrahimu amesema nyumba 10 zilizojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi kijiji cha Igongwe zimechomwa moto na kuteketeza mali zote zilizokuwa ndani.

Amesema tukio hilo limefanywa na baadhi ya wananchi wa Stalike waliojichukulia sheria mkononi wakigombania mashamba kati yao na kijiji cha Igongwe lililopelekea kifo cha Klisent Mwananjela (40) mkazi wa kijiji cha Stalike.


 
Ndani ya nini? Unapapenda sana ndani eeeenh? Akitoka mtunuku na ndani kwako basi.

Yaani we jamaa usipochafuaga hali ya hewa kwenye uzi za watu hujisikii kabisa aisee. Shida yako nini haswa mangi?
Kuna sehemu ya nyuma itakuwa inamtekenya.
 
What a shame!Hili ndiyo Taifa ambalo limejengwa kwa miaka 60 ya uhuru ambapo watu wake bado wanaamini kuwa radi hutengenezwa na binadamu🚶🚶🚶
 
Itakuwa Anjelina Revocatus alimnyima mshikaji mzigo sasa masela wakamzomea jamaa.... KUMBUKA JAMAA ALIPENDA SANA SIFA ZA KIJINGA NA KUTISHIA WATU NA RADI.... alivyo mjinga akajisifia mbele ya wakulungwa kwamba eti yeye ndiye alituma radi kwa binti mzuri Anjelina.....
 
Napata wapi technology ya kutengeneza radi mtu aniuzie
 
Kiwango duni sana cha elimu kinawafanya waamini radi inatengenezwa na mtu. Imani za kishirikina
Ndiyo ni imani za kishirikina, lakini sumbawanga unapajua ? Kaulize radi huko, ndiyo utajua kama ni elimu ndogo au la, ila kibaya zaidi kama itakuwa imekupitia wewe mwenyewe hautajifunza kitu
 
Ndani ya nini? Unapapenda sana ndani eeeenh? Akitoka mtunuku na ndani kwako basi.

Yaani we jamaa usipochafuaga hali ya hewa kwenye uzi za watu hujisikii kabisa aisee. Shida yako nini haswa mangi?
Acha aongee. Nchi imefunguliwa
 
Halafu humu JF watu wanauliza eti kwanini watu wa Kanda hio hua hawarudi makwao mwisho wa mwaka Kama wachaga.

Nadhani jibu mmelipata,urudi kwenu ukapigwe na radi ya kutengenezwa na engineer Baraka Saidi Hiiiiiiiiiiiiiiiii nahene loloooo 😄😄😄
 
Halafu humu JF watu wanauliza eti kwanini watu wa Kanda hio hua hawarudi makwao mwisho wa mwaka Kama wachaga.

Nadhani jibu mmelipata,urudi kwenu ukapigwe na radi ya kutengenezwa na engineer Baraka Saidi Hiiiiiiiiiiiiiiiii nahene loloooo [emoji1][emoji1][emoji1]
Huwa wanarudi japo si kwa muda maalumu kama wachaga wao ni muda wowote!
 
Yaani radio ya inatengenezwa na mtu?
Huu ujinga wa Watanganyika upo Kwa kiwango Cha Juu mno!
 
Huwa wanarudi japo si kwa muda maalumu kama wachaga wao ni muda wowote!
😄😄 sehemu ambayo mtu akijenga kwao nyumba ya bati tu kifuatacho Ni kulogwa?

Engineer Baraka piga radi huyo.
 
Back
Top Bottom