Kusali ni muhimu, lakini baadhi ya tabia na sheria za baadhi ya makanisa yanachangia sana kuvunja moyo watu kuabudu.
Naomba mwenye kujua kanisa lolote lenye sifa zifuatazo ili nijiunge;
- Liwe ni kanisa la kikristu
- Liwe na mfumo wa kitaasisi (yaani management iwe kimfumo wa kitaasisi)
- Liwe linapatikana angalau kila wilaya/mkoa
- Misingi ya waumini wake iwe ni ile ya teamwork (umoja bila kubagua masikini au tajiri hususani wakati wa matatizo ya mmoja mmoja)
- Liwe ni kanisa lisilotegemea uwepo wa mchungaji/kiongozi mmoja
- Liwe ni kanisa lenye ratiba maalum ya kuzingatiwa (standards)
- Liwe ni kanisa linalojali malezi ya watoto kiroho
- Liwe ni kanisa la watu wenye akili timamu.
- Liwe ni kanisa lenye kupenda haki, usawa na uwazi
- Liwe ni kanisa linaloponya, kukuza na kujenga imani kwa waumini wachanga n.k
Yoyote anayefahamu kanisa lenye hizo sifa anifahamishe!! Natafuta kanisa la kujiunga!
1. liwe kanisa la kikristu (hapo unaonekana mkatoliki, kanisa lililokufa limebaki mifupa tu,okokeni mmwone Mungu maishani mwenu).
2. Mfumo wa kitaasisi (hiyo sio garantii kwamba ni kanisa sahihi).
3. kila mkoa/wilaya (hiyo sio garantii kwamba ni kanisa sahihi).
4. teamwork na kusaidiana/kubaguana etc (hakuna kanisa kama hilo siku hizi, popote utakapoenda treatment ya watu inatofautiana na kipato chako, elimu, michango kwa church, wadhifa n.k. hii ni kwasababu, kikawaida mtu anayestahili heshima, mpe heshima yake hata atakapokuja church. hatutegemei Mkuu wa Jeshi Mabeyo aje church halafu tumkalishe au tumchukulie kikawaida kama tunavyokuchukulia wewe, ana hadhi yake hata kama pale church sote tupo sawa. usipompa heshima yake nalo ni kosa. sisemi kuwa ni kosa na sisemi uwa ni sahihi.
5. kutegemea uwepo wa mchungaji (najua hapa unamsema kakobe, au wengine. kila kanisa linategemeana na nani amelianzisha na aliyeanzisha ametoka vipi na Mungu, sio kila jumuiya ya kikanisa itakusaidia umwone Mungu, wengine hata kama unawaona wakuda na hauwaelewi Mungu anawatumia na wangeweza kukusaidia).
6. kanisa lenye ratiba maalumu (hapo utayapata makanisa ya shetani au ya mafarisayo tu ambayo yanampangia Mungu ratiba. kanisa halisi ni Mali ya Roho Mtakatifu ndio analiongoza, kama Roho Mtakatifu atataka muendelee na ibada masaa sita au kumi, mtaendelea, kama atataka muendelee lisaa limoja mtamsikiliza. huwezi kumpangia Mungu masaa. ni sawa na mtu aliyeenda kuchimba dhahabu akakuta dhahabu inatema mno, lakini akajiwekea masharti kuwa hata kama dhahabu inapatikana ikifika saa fulani naondoka. unajuaje muda ule unapoondoka ndio kisima cha baraka/mafuta ya Mungu kitatibuka? naongea na watu wanaomjua Mungu tu hapa, wengine hamtanielewa. makanisa yote yenye ratiba za kumpangia Mungu, ni ya kifarisayo na kidini, na hayamsaidii muumini kumjua au kumwona Mungu katika maisha yake.
7.
kanisa linalojali malezi ya watoto (hapo nakubaliana na wewe, ndio kazi mojawapo ya kanisa hiyo).
8. kanisa la watu wenye akili timamu (hapo hujui unaongea nini, hao unaowadharau na kuwaona hawana akili timamu yawezekana ndio waliokuzidi hata wewe akili. siku ya pentecost watu wengi walishangaa mitume wanaponena kwa lugha, wengine wakasema wamechanganyikiwa, wengine wakasema wamelewa, hadi Petro aliposimama na kuwaelewesha. ndivyo mlivyo mafarisayo wa siku hizi, watu wanapobubujika na kukutana na Mungu, mnasema hawana akili timamu, kumbe hamjijui kuwa ninyi ndio msio na akili. Y
esu aliwaita watu kama ninyi kuwa ni makaburi yaliyopakwa rangi kwa nje ila ndani yamejaa mifupa mitupu tena inayonuka (emphasis added).
9. kanisa linalopenda haki na usawa. sijui una maanisha nini kwa kusema hivyo. kanisani tunaenda kumwabudu Mungu, ni haki gani unaenda kutafuta kanisani? au katiba mpya?
10. namba kumi nakubaliana na wewe.