Anayefahamu kanisa zuri lenye sifa zifuatazo, anijulishe nijiunge tafadhali

Anayefahamu kanisa zuri lenye sifa zifuatazo, anijulishe nijiunge tafadhali

Based on those criteria Tanzania Assemblies of God might be a good fit. Nasema hivyo nikiwa muumini wa RC
 
5,6 na 9. ni kizuizi kwa kanisa langu, yaangu hivyo vipengele vitatu tu ni balaa....ukija kusali siku ya kwanza usigundua hayo matatizo basi ukirudi mara ya pili lazima utagundua huo udhaifu na utakimbia utatangaza kuwa walokole wezi. Basi nakushauri nenda kwengineko sio huku ninakosali mimi maana nitapata aibu uniseme vibaya😛😛
 
Utaitambuaje dini ya kweli?
1. Hakikisha inatumia biblia kama chanzo cha mafundisho yake.. Sio falsafa za binadamu.
2. Waumini hawaungi mkono upande wowote wa siasa
3. Hawajiungi kupigana.(jeshi). Wala kuombea majesh yao yakashnde vita fulan..kumbuka nchi mbili znadin hiyohyo na wote mnaombea nch yenu ishinde. Mungu mmoja aamueje vita hyo?
4. Waumini wapendane kikweli. Bila unafiki.. Anza kuchunguza UPENDO Baina ya viongoz..
5.Usiamini miujiza yao.. Muujiza hata kwa nguvu tofauti utafanya... Mbona wanaoponya walemav hawafufui wafu? Mbona covid imewashinda? Mtaan walemav kibao pembezoni mwa lami, kwanini wasishuke kwenye v8 zao wawaponye..?
TAFADHALI. ANZIA HAPA
www.jw.org/sw
 
Hapo kwenye namba moja umesema waziwazi kwamba liwe ni Kanisa la Kikristu . Sina nyongeza zaidi ya ulivyosema.
 
Kusali ni muhimu, lakini baadhi ya tabia na sheria za baadhi ya makanisa yanachangia sana kuvunja moyo watu kuabudu.

Naomba mwenye kujua kanisa lolote lenye sifa zifuatazo ili nijiunge;
  1. Liwe ni kanisa la kikristu
  2. Liwe na mfumo wa kitaasisi (yaani management iwe kimfumo wa kitaasisi)
  3. Liwe linapatikana angalau kila wilaya/mkoa
  4. Misingi ya waumini wake iwe ni ile ya teamwork (umoja bila kubagua masikini au tajiri hususani wakati wa matatizo ya mmoja mmoja)
  5. Liwe ni kanisa lisilotegemea uwepo wa mchungaji/kiongozi mmoja
  6. Liwe ni kanisa lenye ratiba maalum ya kuzingatiwa (standards)
  7. Liwe ni kanisa linalojali malezi ya watoto kiroho
  8. Liwe ni kanisa la watu wenye akili timamu.
  9. Liwe ni kanisa lenye kupenda haki, usawa na uwazi
  10. Liwe ni kanisa linaloponya, kukuza na kujenga imani kwa waumini wachanga n.k
Yoyote anayefahamu kanisa lenye hizo sifa anifahamishe!! Natafuta kanisa la kujiunga!
1. liwe kanisa la kikristu (hapo unaonekana mkatoliki, kanisa lililokufa limebaki mifupa tu,okokeni mmwone Mungu maishani mwenu).

2. Mfumo wa kitaasisi (hiyo sio garantii kwamba ni kanisa sahihi).

3. kila mkoa/wilaya (hiyo sio garantii kwamba ni kanisa sahihi).

4. teamwork na kusaidiana/kubaguana etc (hakuna kanisa kama hilo siku hizi, popote utakapoenda treatment ya watu inatofautiana na kipato chako, elimu, michango kwa church, wadhifa n.k. hii ni kwasababu, kikawaida mtu anayestahili heshima, mpe heshima yake hata atakapokuja church. hatutegemei Mkuu wa Jeshi Mabeyo aje church halafu tumkalishe au tumchukulie kikawaida kama tunavyokuchukulia wewe, ana hadhi yake hata kama pale church sote tupo sawa. usipompa heshima yake nalo ni kosa. sisemi kuwa ni kosa na sisemi uwa ni sahihi.

5. kutegemea uwepo wa mchungaji (najua hapa unamsema kakobe, au wengine. kila kanisa linategemeana na nani amelianzisha na aliyeanzisha ametoka vipi na Mungu, sio kila jumuiya ya kikanisa itakusaidia umwone Mungu, wengine hata kama unawaona wakuda na hauwaelewi Mungu anawatumia na wangeweza kukusaidia).

6. kanisa lenye ratiba maalumu (hapo utayapata makanisa ya shetani au ya mafarisayo tu ambayo yanampangia Mungu ratiba. kanisa halisi ni Mali ya Roho Mtakatifu ndio analiongoza, kama Roho Mtakatifu atataka muendelee na ibada masaa sita au kumi, mtaendelea, kama atataka muendelee lisaa limoja mtamsikiliza. huwezi kumpangia Mungu masaa. ni sawa na mtu aliyeenda kuchimba dhahabu akakuta dhahabu inatema mno, lakini akajiwekea masharti kuwa hata kama dhahabu inapatikana ikifika saa fulani naondoka. unajuaje muda ule unapoondoka ndio kisima cha baraka/mafuta ya Mungu kitatibuka? naongea na watu wanaomjua Mungu tu hapa, wengine hamtanielewa. makanisa yote yenye ratiba za kumpangia Mungu, ni ya kifarisayo na kidini, na hayamsaidii muumini kumjua au kumwona Mungu katika maisha yake.

7. kanisa linalojali malezi ya watoto (hapo nakubaliana na wewe, ndio kazi mojawapo ya kanisa hiyo).

8. kanisa la watu wenye akili timamu (hapo hujui unaongea nini, hao unaowadharau na kuwaona hawana akili timamu yawezekana ndio waliokuzidi hata wewe akili. siku ya pentecost watu wengi walishangaa mitume wanaponena kwa lugha, wengine wakasema wamechanganyikiwa, wengine wakasema wamelewa, hadi Petro aliposimama na kuwaelewesha. ndivyo mlivyo mafarisayo wa siku hizi, watu wanapobubujika na kukutana na Mungu, mnasema hawana akili timamu, kumbe hamjijui kuwa ninyi ndio msio na akili. Yesu aliwaita watu kama ninyi kuwa ni makaburi yaliyopakwa rangi kwa nje ila ndani yamejaa mifupa mitupu tena inayonuka (emphasis added).

9. kanisa linalopenda haki na usawa. sijui una maanisha nini kwa kusema hivyo. kanisani tunaenda kumwabudu Mungu, ni haki gani unaenda kutafuta kanisani? au katiba mpya?

10. namba kumi nakubaliana na wewe.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]View attachment 1791855
but they know deep in their hearts that their denomination (catholic) does not help them spiritually to know God. they are drunkards just like any other, priests and nuns know what they always do in the missions, they visit witch doctors just like any other and they teach no truth of the Bible but truth of their religion.
 
Fafanua kidogo mkuu
Kwa kusaidia tu japo sio kwa umuhimu kuna makanisa mengi tu yanaongozwa na vichaa kuna moja wapo linatoa hadi dressing codes mara unasikia jpili ijayo ni old school sunday[emoji23][emoji23]
 
Kwa kusaidia tu japo sio kwa umuhimu kuna makanisa mengi tu yanaongozwa na vichaa kuna moja wapo linatoa hadi dressing codes mara unasikia jpili ijayo ni old school sunday[emoji23][emoji23]
kanisa pekee ninalojua kuwa ni la vichaa na machizi, ni kanisa la pool of siloam, wale wanaoamini kuwa Munuo aliyeanzisha kanisa ni mungu, wanaamin Damu ya Yesu na Jina la Yesu vimepungua nguvu hivyo hawaombi kwa Jina la Yesu wala Damu ya Yesu. pia, Munuo aliwafundisha kuwa yeye kwa maombi yake alishamuua shetani, ajabu yake hadi leo shetani bado mzima na anaendelea kudanganya walimwengu. kuna watu wanamwamini huyu mchaga huwaambii kitu. alikufa kwa tetenasi wakaweka mochwari siku tatu wakiamini atafufuka walipoona ananuka wakaenda kuzika kule njia ya bagamoyo, wanapozika wakatangaza kuwa wamemwona anapaa. wanavaa manguo meupe utafikiri misukure. hawa peke yao ndio machizi na nikiwaangalia uwa nawaonea hurma sana. mpo wazee wa mbezi makonde?
 
1. liwe kanisa la kikristu (hapo unaonekana mkatoliki, kanisa lililokufa limebaki mifupa tu,okokeni mmwone Mungu maishani mwenu).

2. Mfumo wa kitaasisi (hiyo sio garantii kwamba ni kanisa sahihi).

3. kila mkoa/wilaya (hiyo sio garantii kwamba ni kanisa sahihi).

4. teamwork na kusaidiana/kubaguana etc (hakuna kanisa kama hilo siku hizi, popote utakapoenda treatment ya watu inatofautiana na kipato chako, elimu, michango kwa church, wadhifa n.k. hii ni kwasababu, kikawaida mtu anayestahili heshima, mpe heshima yake hata atakapokuja church. hatutegemei Mkuu wa Jeshi Mabeyo aje church halafu tumkalishe au tumchukulie kikawaida kama tunavyokuchukulia wewe, ana hadhi yake hata kama pale church sote tupo sawa. usipompa heshima yake nalo ni kosa. sisemi kuwa ni kosa na sisemi uwa ni sahihi.

5. kutegemea uwepo wa mchungaji (najua hapa unamsema kakobe, au wengine. kila kanisa linategemeana na nani amelianzisha na aliyeanzisha ametoka vipi na Mungu, sio kila jumuiya ya kikanisa itakusaidia umwone Mungu, wengine hata kama unawaona wakuda na hauwaelewi Mungu anawatumia na wangeweza kukusaidia).

6. kanisa lenye ratiba maalumu (hapo utayapata makanisa ya shetani au ya mafarisayo tu ambayo yanampangia Mungu ratiba. kanisa halisi ni Mali ya Roho Mtakatifu ndio analiongoza, kama Roho Mtakatifu atataka muendelee na ibada masaa sita au kumi, mtaendelea, kama atataka muendelee lisaa limoja mtamsikiliza. huwezi kumpangia Mungu masaa. ni sawa na mtu aliyeenda kuchimba dhahabu akakuta dhahabu inatema mno, lakini akajiwekea masharti kuwa hata kama dhahabu inapatikana ikifika saa fulani naondoka. unajuaje muda ule unapoondoka ndio kisima cha baraka/mafuta ya Mungu kitatibuka? naongea na watu wanaomjua Mungu tu hapa, wengine hamtanielewa. makanisa yote yenye ratiba za kumpangia Mungu, ni ya kifarisayo na kidini, na hayamsaidii muumini kumjua au kumwona Mungu katika maisha yake.

7. kanisa linalojali malezi ya watoto (hapo nakubaliana na wewe, ndio kazi mojawapo ya kanisa hiyo).

8. kanisa la watu wenye akili timamu (hapo hujui unaongea nini, hao unaowadharau na kuwaona hawana akili timamu yawezekana ndio waliokuzidi hata wewe akili. siku ya pentecost watu wengi walishangaa mitume wanaponena kwa lugha, wengine wakasema wamechanganyikiwa, wengine wakasema wamelewa, hadi Petro aliposimama na kuwaelewesha. ndivyo mlivyo mafarisayo wa siku hizi, watu wanapobubujika na kukutana na Mungu, mnasema hawana akili timamu, kumbe hamjijui kuwa ninyi ndio msio na akili. Yesu aliwaita watu kama ninyi kuwa ni makaburi yaliyopakwa rangi kwa nje ila ndani yamejaa mifupa mitupu tena inayonuka (emphasis added).

9. kanisa linalopenda haki na usawa. sijui una maanisha nini kwa kusema hivyo. kanisani tunaenda kumwabudu Mungu, ni haki gani unaenda kutafuta kanisani? au katiba mpya?

10. namba kumi nakubaliana na wewe.
UNAKUBALI NA KUKATAA!
Sijui hata unapinga nini!

Hujui kuwa kuna makanisa husali uchi?
Kama hakuna vichaa nabii Tito alipelekwa mirembe kufanya nini?

Kiufupi nilichoandika ni fleva za nahitaji yangu!

Ni sawa na kuandaa chakula mwingine anachemsha mwingine kukaanga
 
Sidhani kama kuna kanisa la aina hii duniani hapa, makanisa mengi suala la haki sijui kuangalia haki za binadamu hakuna. Ndio maana wametulia kuhusu mgogoro kati ya Israel na Parestina
Wanaunga mkono Israel
 
Linabagua Na kutenga waumini kwa migongo ya sacrament, Halitoi huduma kwa baadhi ya watu pasipo kuwasaidia watoke waliko, halibatizi watoto hadi maoni ya jumuiya, Halina umoja wakati wa matatizo
Naimba nikupinge kwa facts...sakrament ina vigezo vyake, kwa mfano huwezi kukomunika km hujapata sakrament ya ekaristi.huo misaada wa kijamii utasaidiwa kwa kuanzia ngazi ya jumuiya ndogondogo.hiyo ndio maana ya taasisi
 
Makanisa mazuri ni haya makubwa kwa maana sio mali binafsi.Kama haya ya watu binafsi sali Yale mchungaji wake alikuwa sauli zamani hawa wanamjua shetani ndani nje na huwa wameapa kupambana na shetani sababu ya walipokuwa sauli shetani aliwatesa Sana aliwadanganya wakatoa kafara ndugu,mke, watoto na awakupata faida baada ya kuujua uongo wa shetani wakatangaza vita na shetani ikiwemo kutoa Siri zote za shetani wakapambana na shetani kiroho wakamshinda shetani hawa ndio watumishi wa kweli.Unakuta kabla alikuwa ni freemason,mchawi,mganga, jambazi,kahaba mkubwa akatoka huko baada ya kuijua kweli, mtumishi huyu huwa ni kweli anamtumikia Mungu,ila ukiingia kwenye makanisa ya kishirikina Yale madhabauni wamezika sanda ya maiti ukiingia kanisa hilo huwezi toka bila neema ya Mungu.Wapo wengine ujiita mungu na wafuasi wao wanawaabudu kabisa na uwaambii kitu mfano kanisa la baba godi, mfalme zumaridi mwanza hawa ni washirikina kabisa na ujiita wao mungu, kanisa la baba godi awatumii biblia wanadai walishavuka level ya kutumia biblia,pili biblia imekosewa,tatu baba godi ndie mungu wanafata maagizo yake.
So sio KILA kanisa lenye msalaba ni la kuingia mengi ni mahekalu ya shetani.
Yapo mafundisho ya kulijua kanisa la kweli.Washirikina ulitaja jina la Yesu na halina shida kwao so usidanganywe na mshirikina madhabauni akitumia jina la Yesu kutenda miujiza.
Mwisho ukishika dini kamata kwa akili mbili,sio KILA uambiwacho na mchungaji wako unakiingiza akilini bila kukichuja kupitia maandiko.
 
Bwana Lee Yuan Kew moja ya binadamu aliyefanya makubwa na ya kuigwa Katika taifa la Singapore;Kuitoa Nchi katika dimbwi la umaskini mpaka taifa zuri kiuchumi( From third world to First World);

Bwana Lee kuan yew Mwaka 5/05/2001 alifanya interview's..PBS:Commanding Heights.

Aliulizwa swali kuhusu Julius Nyerere na Falsafa zake: na njisi alivyomtambua akajibu kama ifuatavyo:

"Oh yes Julius Nyerere is a good Christian;
He wanted to do good to his people;
He great Christian;
He quote you chunk of the bible;
He was a preacher Also,

He was devout catholic"

Mwalimu alikuwa Mkatoliki nje ndani.

Mosi; Mimi nimeachana na dini/imani za kigeni Miaka 7saba sasa imepita:

Baada ya miaka kadhaa project Kubwa ya weza kutokea:

Project: "Alisina utachomwa Moto nakuapia"

Publisher: Black Conscious movement (BcM)

Editor/:Bart D Ehrman.

Sasa kuhusu kanisa ulitakalo:

Kuna kanisa/ huduma,wao hujuita Spirit word ministries..neema juu ya neema.

Inaongozwa na mzee wa neema size masizi ana channel Yake inaitwa Top plus.

Mafundisho na mafunzo yao ni Tofauti Sana na makanisa yote ya Tanzania...mfano unaambiwa hakuna dhambi, hakuna siku ya mwisho.

Mwanzo itakuwa ngumu maanake wanageuza meza mafundisho uliyokuwa umeyashikilia ambayo ndio yamejaa makanisa yote tanzania.

Huwa kunawatoa ushuhuda wa njjsi maneno au mafundisho ya mzee wa neema yalivyo wabadilisha na huwa na waeelewa njinsi wanavyojisikia,hiyo huwa imesababishwa na Athari za dini/kanisa/imani mojawapo ikiwa na kukushindilia hisia za kuhukumika:

Kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.

Spirit word ministries huwa wanatambaa na kuidadavua Warumi 3:19-28 waraka was mtume Paulo.

Kama hakuna sheria hakuna dhambi.

Huwa nikiwatazama Top plus huwa namkumbuka bwana James Ku gel myahudi How to read the Bible,Sabab u huwa nawaona wanasoma vitabu mbalimbali vya dini mfano injili ya Nicodemus.

Shukrani Mkuu:

"If God listened to the prayer's of men,All men would quickly have perished for they are forever praying for evil against one another"- Epicurus
 
Back
Top Bottom