naomba kujua mchanganuo wa kiwango cha mshahara na asilimia yake ktk kodi ya "pay as you earn" (PAYE)
Soma jedwali hili.
[TABLE="align: left"]
[TR]
[TD]MSHAHARA KWA MWEZI[/TD]
[TD]KIWANGO CHA KODI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Shilingi 0 –Mpaka shilingi 170,000[/TD]
[TD]HAKUNA yaani mshahara huo umesamehewa kodi[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Shilingi 170,000 –Mpaka shilingi 360,000[/TD]
[TD]Kodi ni 12% ya ziada ya shs 170,0000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Shilingi 360,000 –Mpaka shilingi 540,000[/TD]
[TD]Kodi ni sh 22,800 kujumlisha 20% ya ziada ya 360,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Shilingi 540,000 –Mpaka shilingi 720,000[/TD]
[TD]Kodi ni sh 58,800 kujumlisha25% ya ziada ya 540,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Shilingi 720,000 –Na zaidi[/TD]
[TD]Kodi ni sh 103,800 kujumlisha 30% ya ziada ya 720,000[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Mfano:
Mshahara ni shilingi 509,888.89 KODI ITAKUWA KIASI GANI?
JIBU
Mshahara wa shilingi 509,888.89 utasamehewa 10% ya NSSF ikiwa mwajiriwa ni mwanachama wa NSSF na mshahara wake unakatwa hiyo NSSF ambayo ni 10%. Hivyo hivyo kwa wanachama wote wa mifuko ya hifadhi ya jamii inayotambulika na srikali.
Kwa hiyo shilingi 509,888.89 ukitoa 10% yake unapata NSSF ni shs 50,988.89.
Unachukua shs 509,888.89 tos shilling 50,988.89 unapata sh 458,900. Hizi shilingi 458,900 ndo zitatozwa kodi ya PAYE. Kutokana na jedwali hapo juu kodi yake itaangukia kwenye band three hapo juu.
Shilingi 458,900 ipo kati ya shilingi 360,000 mpaka 540,000
Yaani shs 458,900 ni ziada ya 360,000
Unachukua shs 458,900 unatoa na shs 360,000 unapata shs 98,900 ndio hiyo ziada ya 360,000!!!
Kwa hiyo shs 98,900 unaitoza asilimia 20 itakuwa (20%xshs 98,900)= sh19,780
Kwa hiyo jumla ya kodi ni ile kodi fixed iliyopo kwenye jedwali shs 22,800+shs19,780 ambayo jumla ya kodi ya mshahara wa Shs 509,888.89 ni SHS
42,580