Kuna kipindi huwa mnapandisha nyuzi ambazo watu huwa tunabaki tunawashangaa sana, mwenyekiti wako sio ndio alimnadi Lowasa Tz nzima???Huyu Mzee baada ya ccm kumkata kwenye kura za maoni , akaomba kujiunga na Chadema , Chadema ikamsaidia kupata Ubunge na ikampandisha hadi kuwa Katibu Mkuu wa Chama , baadaye mwaka 2015 akashirikiana na Askofu Gwajima kumshawishi Lowassa ajiunge na Chadema , Kamati kuu ikapewa Taarifa na Bwana Lowassa akaingia Chadema na kupitishwa kugombea Urais .
Baada ya Lowassa aliyeletwa na Dr Slaa kupitishwa kugombea Urais , Dr Slaa akajiondoa Chadema kwa Ushawishi wa Mchumba wake na kwa ushawishi pia wa Dr Mwakyembe , akaingia ccm na kuwa mpiga debe wao , akalipwa Ubalozi kwa kazi hiyo ya kupiga debe na kutukana Lowassa na Sumaye , ambao kwa sasa wako wote chama kimoja .
Kwa kufupisha tu nina swali dogo kuhusu huyu Mzee , Juzi alimsifia Dr Magufuli kwa kuwa Mwanademokrasia na kuilaumu serikali kwa kumnyima fursa ya kumuombea alipokuwa Mgonjwa , na kwamba hadi leo moyo wake uko ndani ya magufuli au sijui magufuli ndio yuko kwenye moyo wake .
Sasa hebu msomeni hapa halafu mtueleze kile anachokisimamia .
View attachment 2164960
Kiufupi, hata chembe chadema hamumuwezi Dr.
Kikundi chenu angalau Mnyika na Heche tu