Inawezekana kuna jambo unajaribu kulielezea, lakini hujapata njia nzuri ya kulieleza likaeleweka kirahisi.
Ngoja mimi nijaribu kwa kifupi, kama hivi ndivyo unavyowaza juu ya CHADEMA.
Mbowe, ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA, na ambaye bila shaka anapozungumza anawakilisha mawazo ya chama hicho, kisha eleza yaliyozungumzwa kati yake na Samia walipokutana baada ya kutoka jela. Hili linaeleweka, na sina sababu ya kuyarudia hapa waliyoazimia kuyafanya.
Sasa niambie, katika muda huu mfupi, na ukizingatia hayo waliyokubaliana, utategemea vipi CHADEMA waonyeshe yale yale waliyokuwa wanaonyesha wakati wa Magufuli, wakati ambapo walikuwa wakiwindwa kupigwa virungu, kuwekwa mahabusu, na hata kutishiwa kuuwawa?
Hilio moja.
La pili, hata kama halina uzito mkubwa kwa sasa; anayoyasimamia Samia ndani ya chama chake, na matamanio ya mafanikio anayotarajia kwenye utawala wake, hayana tofauti kubwa sana na yale yanayotamaniwa na CHADEMA, kisera. Tofauti pekee iliyopo kwa sasa kati ya CCM ya Samia na CHADEMA ya Mbowe, ni kushikilia, au kutafuta madaraka ya kuongoza nchi. Samia hataki katiba mpya, siyo kwamba haoni ubovu wake, ila katiba hiyo inampa wigo zaidi wa kumbakisha madarakani.
CHADEMA wao wanaona Katiba hii ni kizingiti kikuu kinachowanyima fursa ya kushika madaraka, kwa hiyo watafanya kila juhudi, ipatikane Katiba Mpya.
Sasa basi, kama bado unaona CHADEMA wamenyang'anywa agenda ya mambo ya kusimamia, ikiwa ni pamoja na hili la Katiba Mpya, hapo nadhani labda una maana nyingine ambayo bado hujaielezea hapa ili tukuelewe vizuri.
Uwanja ni wako.