Anayejua kuhusu hili la RITA anisaidie tafadhali

Anayejua kuhusu hili la RITA anisaidie tafadhali

Wakati wa kujaza form online nimekosa kipengele cha kuchagua inchi, only Tanzania iko pale, so huna option nyingine,

Sasa ndio nikauliza anaejua je tunafanyeje?
 
Mie baba ni mtanzania, mama ni mkenya
Mpaka sasa ana uraia wa inchi mbili mpaka atakapofika 18
Ila wakuu nimeomba kwa anaejua tafadhali anielekeze naona uvivu kurudi tena rita
Yeye ni mkenya, inamaanisha kazaliwa Kenya ,Kuzaliwa Kenya tayar yeye ni mkenya hata kama wazazi wote wangekua watanzania .
Taifa lake ni mahali au eneo alipozaliwa.

Asili yake mtanzania, inamaanisha baba yake ni mtanzania yaan asili ya alikozaliwa babayake .
Asili ni vinasaba vyake aka DNA ni vyawapi au vilipotokea .

Mfano bongo kuna waarabu wamezaliwa huku ,hao ni watanzania wenye asili ya kiarabu.

Haraka sana fanya namna utaifa wake uwe Tanzania maana mpk sasahivi anahesabika ni mkenya sababu kazaliwa kwenye hospitali iliyopo kwenye ardhi ya Kenya.
Kumbuka nchi yetu haina na hairuhusu uraia pacha kwahiyo mfanyie dogo mafekechee mapema au muache akikua achague mwenyew achukue utaifa wa Tanzania au abaki na utaifa wa Kenya.

NB:Zingatia neno ASILI pia tofautisha neno hilo na UTAIFA.
Mie baba ni mtanzania, mama ni mkenya
Mpaka sasa ana uraia wa inchi mbili mpaka atakapofika 18
Ila wakuu nimeomba kwa anaejua tafadhali anielekeze naona uvivu kurudi tena rita
 
Hapa sasa umenisaidia kidogo, ingawa bado hujaniongoza kipi cha kufanya baada ya kushindwa kuipata kenya kwenye form ya maelezo ya mtoto online ya rita website
Nenda sehemu aliozaliwa bro vp Kwan ???!!
Ww Rita washakwambia ni Tanzania tu wewe unalazimisha usaidiwe ibadilike iwe Kenya aisee sisi wabongo bhana n washamba kweli tunahitaji elimu Sana ili tuondoe ujinga vichwan mwetu
Chakukusaidia nenda kwny mamlaka ya Kenya inayohusiana na vyeti vya kuzaliwa umpatie mtoto cheti au pita njia za panya ufoji cheti cha kuzaliwa bongo aishi nacho haijalishi mbeleni itakuwaje.
 
Nimejaza form, ila nimeshinde
Yes ni dhambi kuongopa, ningeweza kutengeneza tangazo hospitali yeyote ile then nikatoa chetu kirahisi, ila kiukweli ningekuwa nimemdhulumu sana mtoto, baadae akikua atakuwa anasema uongo maisha yake yote, kwani akiulizwa atasema nimezaliwa tz wakati ukweli ni amezaliwa kenya
Kama ni hivo basi kubali tu aendelee kuwa mkenya na chakumsaidia mtoto nenda kachukue cheti chake Cha kuzaliwa Kenya alaf akikua atajua yeye achague wapi
 
Kiufupi lazima ujue maana ya cheti cha kuzaliwa. Pia mahusiano ya cheti cha kuzaliwa na uraia. Huwezi kuzaliwa ardhi ya Kenya ukaomba cheti cha kuzaliwa Tanzania. Na huwezi kuzaliwa ardhi ya Tanzania ukaomba cheti cha kuzaliwa Kenya. Hizi ni nchi mbili tofauti zenye sheria zake tofauti. Mtu anapewa cheti cha kuzaliwa na mamlaka ya nchi au ardhi ya nchi aliyozaliwa. Cheti cha kuzaliwa lazima kionyeshe mahali alipozaliwa mtoto. Hivyo Tanzania haina mamlaka ya kutoa cheti cha kuzaliwa kwa mtu aliyezaliwa Kenya na hata ingekitoa kisingetambuliwa na Kenya wala kumsaidia mtoto huyo .

Pia kuwa na cheti cha kuzaliwa Tanzania siyo proof ya kuwa wewe ni raia wa Tanzania. Kasome kwenye vyeti vya kuzaliwa vinavyotolewa siku hizi na RITA kule chini kuna NB na maandishi ya kukolezwa kuwa kuwa na cheti hicho siyo proof ya Utanzania.
 
Wakati wa kujaza form online nimekosa kipengele cha kuchagua inchi, only tanzania iko pale, so huna option nyingine,
Sasa ndio nikauliza anaejua je tunafanyeje?
Sasa kama amezaliwa Kenya unatakaje apatiwe cheti cha kuzaliwa cha Tanzania na umesema kabisa hutaki kupindisha? Nenda kamsajili Kenya awe na cheti cha Kenya; baadae huku umtaftie passport. Hatuna uraia pacha. Kalale
 
Hiyo online application mbona kwangu haifanyi kazi au ndio mambo ya tovuti za serikali
 
Nimejaza form, ila nimeshinde
Yes ni dhambi kuongopa, ningeweza kutengeneza tangazo hospitali yeyote ile then nikatoa chetu kirahisi, ila kiukweli ningekuwa nimemdhulumu sana mtoto, baadae akikua atakuwa anasema uongo maisha yake yote, kwani akiulizwa atasema nimezaliwa tz wakati ukweli ni amezaliwa kenya
Mkuu kama hutaki taabu ,
 
Sasa kama amezaliwa Kenya unatakaje apatiwe cheti cha kuzaliwa cha Tanzania na umesema kabisa hutaki kupindisha? Nenda kamsajili Kenya awe na cheti cha Kenya; baadae huku umtaftie passport. Hatuna uraia pacha. Kalale
Si anafata uraia wa baba? Baba si ni mtanzania?
 
Back
Top Bottom