Anayejua kuhusu hili la RITA anisaidie tafadhali

We chawa kumbe ulikua Kenya ndo maana tulipumzika humu
 
Asante ila bado hujanisaidia, naona kama umenisimanga tu
Omba cheti cha kuzaliwa huko Kenya.
Hapa bongo atakuwa anakitumia sehemu zote zinazohitajika hadi atakapofuka 18.
Mimi binafsi sijawahi experience husumbufu huko mashuleni. Nina mtoto anatumia cheti cha nje. Relax kachukue cheti chake Kenya
 
Omba cheti cha kuzaliwa huko Kenya.
Hapa bongo atakuwa anakitumia sehemu zote zinazohitajika hadi atakapofuka 18.
Mimi binafsi sijawahi experience husumbufu huko mashuleni. Nina mtoto anatumia cheti cha nje. Relax kachukue cheti chake Kenya
Asante sana
 
Mjazie mkoa wa Tanzania ili atakapotaka kuja kuwa kiongozi mkubwa kwa maana ya Rais wa nchi asijekuletewa zengwe na kuondoshwa.
 
RITA ni mamlaka inayojishughulisha na usajili wa vizazi na vifo, vinavyotokea ndani ya mipaka ya Tanzania.
Mtoto wako aliyezaliwa Kenya anapaswa kuwa na cheti cha kuzaliwa cha Kenya.

RITA hawana mamlaka ya kutoa cheti cha kuzaliwa cha Tanzania wakati mtoto amezaliwa Kenya.
Kwa kuwa wewe ni mtanzania wakati mama yake ni mkenya, mwanao ana hadhi ya kuwa na uraia wa nchi mbili hadi pale atakapofikisha miaka 18, atapowajibika kuukana uraia wa nchi mojawapo kati ya hizo mbili.

Kwa sasa mtoto wako kama yupo hapa Tanzania atapata huduma zote za kijamii kama mtu mwenyewe uraia pacha mwenye cheti cha kuzaliwa cha Kenya kama nyaraka muhimu itakayotumika kuamua uraia wake siku zijazo.
 
Kwa hoja yako hiyo basi
Mtoto ni mkenya kwahiyo cheti cha kuzaliwa kaombe Kenya na pia huku Tanzania fanya process za Idara ya Uhamiaji halafu ndo uje uende Rita huo ndo ukweli.!
Kwa Tanzania kwa mtu ambaye siye raia ananzia Uhamiaji kwanza halafu Taasisi nyingine ndo zinaendelea.!
Wadau walikuwa wanakurahishia tu Maana Mtoto ni mdogo hajui chochote na huko Kenya kaenda kuzaliwa tu na hapajui na wewe unataka ulingishie/Utambe(Sifa) Uonyeshe mtoto kazaliwa nje ya Nchi kwenye cheti na Document nyingine.!
 
Okey,

lakini kwanini asipewe hapa cheti na kiandikwe kuwa amezaliwa kenya na mama mkenya ila baba ni mtanzania?
Na je, nikitaka kumuombea passport book sasa hivi atweza kupewa?
 
Hahaaaa....jamaa anatafuta sifa ambazo hata hazina msaada kwa mtoto na yeye mwenyewe
 
Hapana hayo ya kulingisha na kujidai mie sina, muhimu mwanagu apate vheti cha kumtambulisha kama mtanzania kwa kuwa mie baba yake ni mtanzania
 
Mwamba tulia Mtoto tu Alipozaliwa ndiyo kwenu. Huyo Mkenya Mwamba.
Ila kama hupendi nenda Ubalozi wa Kenya pale Harambe plaza Oysterbay Kenyata Drive na nyaraka zako Alipozaliwa Mtoto wako utakana uraia wa kenya wa mwanao kisha utapewa nyaraka ambazo zitakuwezesha kwenda Rita ili ufanikiwe.
Futilia taarifa za Prof Kabundi juu ya Mambo ya uraia kupitia Youtube.
 
Hivi kuzaliwa kenya ni sifa? Mbona kenya ni wachivu kuliko hapa? Ni kwamba mama yake ni mkenya ndio akaenda kuzalia kwao
Wewe acha kukaza jugula. Sajili mtoto kama mtanzania vinginevyo kama unasimamia ukweli kwanini usiende kumchukulia cheti Cha kuzaliwa Kenya. Utaingia gharama kwa kukaza fuvu, nenda uhamiaji wakupe taratibu maana naona huelewi.
 
Okey,

lakini kwanini asipewe hapa cheti na kiandikwe kuwa amezaliwa kenya na mama mkenya ila baba ni mtanzania?
Na je, nikitaka kumuombea passport book sasa hivi atweza kupewa?
Documents zitakazofuatia ndizo zitakazoandikwa kuonyesha kuwa kazaliwa Kenya,.... kitambulisho cha taifa na pasi ya kusafiria ndio vitakavyoonyesha. Cheti cha kuzaliwa ni uthibitisho wa mahali ulipozaliwa na husajiliwa alipozaliwa, hakitolewi zaidi ya mara moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…