Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Habari wanabodi,
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Binafsi namuona kama bado anatumikia cheo chake cha zamani kuliko hiki alichonacho sasa. Inawezekana hii inasababishwa na mazoea ya anafasi aliyotoka kiasi kwamba anaegemea kwenye mambo ya ujenzi tu huku sekta nyingine kama afya, elimu na uchumi zikidorora.

Wenzangu mnamuonaje??.
 
Nadhani bado hatujamuombea vizuri...

Kwamaana ametuahidi tukimuombea hatatuangusha...

Yeye mwenyewe alishaonesha mfano kwa ziara za kustukiza makanisani... anamstukiza mpaka Mungu huyu binadamu.
 
Mifugo,uvuvi na ujenzi ndicho anachokijua kwa ufasaha mengine atajifunza taratibu kila uchao.
 
Mkuu hii ndoto yako inatisha sana japo ina ukweli mtupu. wasiwasi wangu wasije kuangaika na ndoto yako maanake watawala wanogopa ndoto kuliko majambazi.
 
Kuna watu wana nyota zao bana wengine wana nyota za Chips mayai
Wenzetu na sisi tuna nyota za punda yaani ni mpaka ubebeshwe mzigo ndio ule

Ndio dunia hii
 
Ikulu bwana ukienda na misimamo yako ya kina alinacha lazima ukalie kuti kavu.. Ukileta ubaboe wako utapotea kabisa..sasa hivi inabidi magu ajikite kwenye kuiba kura 2020 la sivyo hatoboi.. Kama Tu JK alisababisha ccm ikahindwa 2020 hadi kuoba kura sembuse magu ambaye ana chuki na visasi..
Hajali vijana wasio na ajira yeye kwa vile anakula mara tatu kwa siku basi.. Hajui mwenye njaa afe tu huko.
 
Huwa kuna muda naona kweli huyu Mkulu ni zaidi ya mtemi yaani. Huwa anaamini Uelewa wake upo Juu saana kuliko mtu yoyote hapa Nchini.

Yaani Waandishi wa Habari wanaomba mswada wa sheria ya Habari 2016 Washirikishwe yeye kawaona wajinga!!. Siyo hilo tu ni mengi tu anatupuuza saana huyu Mkulu.


Basi tu ila yana mwisho wake, hakuna lidumlo milele.
 
Yaani kausaini ule mswada haraka sana utafikiri anasaini mikopo ya wanachuo ili wapewe wanafunzi wote bila ubaguzi
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…