Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Wakinamama wajasiriamali wa nyamagana mwanza wamenisikitisha sana leo kwenye taarifa ya Habari wanaiomba serikali iwaangalie kwa jicho la huruma, wote walikua wanajielezea huku wakitoka machozi, aibu kubwa hii kwa serikali ya mamantilie na mabodaboda ni kweli dereva umetusahau ivi..
 
hahaha ivi kaenda veta kweli?
 
Kwa jinsi mnavyoonesha kumchukia kwa kuwasababishia maisha Magumu na kuvuruga siasa za nchi yetu, kama kweli watu wa Tanga, Pemba, Sumbawanga na kwingineko wangekuwa na uchawi basi bila shaka wangeshamloga. Kumbe hakuna uchawi duniani.

Hakuna mwenye uwezo wa kumloga?
 
Mnavyo.... wewe unajitoa?
 
Huyo halogeki maana alishajipanga anawaganga wake toka kibondo
 
Mshana jr hebu njoo baba unahitajika hapa tusaidiane.
 
Kama kuna kitu kimemponza mtawala wa sasa, rais Magufuli ni papara.
Ngumu hata kujua dira/muelekeo katika mipango yake kwa kuwa hawezi kujizuia hata dk akiwa na jambo. Hii imepelekea wananchi kutomuelewa pamoja na mwanzoni walikuwa na imani naye sana. Hii ni tabia itakayom-cost dearly katika uchaguzi ujao wa 2020.

Jikumbushe matukio haya machache uelewe ninachozungumza:
  1. Hakuna haja ya sherehe za uhuru - nchi chafu na tutatumia siku hii kwa ajili ya usafi, mwaka mmoja baadae: sherehe ipo na jiji chafu!
  2. Nimeambiwa kuna watu wameficha sukari, nitawakamata, na kunyang'anya sukari na wao watakwenda ndani. mwaka sasa, hakuna sukari iliyokamatwa na kupewa wananchi, hakuna aliyefungwa na bado sukari ipo juu.
  3. Serikali inahamia Dodoma mara moja, safari itaanza kabla ya bajeti ijayo, miezi karibu 6 sasa hakuna hata karani aliyefika Dodoma ukiachilia mbali Waziri Mkuu ambaye maandalizi yalianza na Lowassa.
  4. Pesa zimefichwa majumbani, nitabadilisha pesa zote. Hadi sasa hakuna aliyekamatwa na hizo pesa zilizofichwa.
Haya ni mambo ambayo kwa kifupi naona yanam-cost sana mkuu na kama hatofanyia kazi, atali-cost taifa lake na chama chake. Yote anayoyasema mkuu inawezekana yalikuwa sawa, ya msingi na labda alipata fununu za kutosha. Shida yake ni papara, kuna saa amefanya mambo kama Katibu mwenezi wa chama cha siasa, anazungumzia kila jambo matokeo yake anatoa pre-mature conclusions, anatoa misimamo ambayo haitekelezi na inabaki kama deni ktk utendaji wake!

Ikifika 2020 watu wakarejea ahadi, kauli, mipango na utendaji lakini pia, leo hii ni muelekeo gani tunaenda hatujui! Huwa mkuu anakuja na matamko au mipango out of blue, watu wake ndio usiseme, wanaibuka na maagizo mengine hayakufuata sharia/taratibu, au mengine hayatekelezeki!

All in all kama kuna sehemu mkuu anahitaji mtu wa kumshauri ni hapa katika kitengo cha habari/usemaji ambao ni mwiba mgumu kwake kuliko eneo jingine lolote!
 
Chaguo la mungu halifanyi makosa, hayo ni maono aliyopewa na mungu. Utimilifu wa maono hayo ndio hakuambiwa kwahiyo inawezakana katabiri yatayojiri miaka 50 ijayo. Vumilieni tu. Nabii wake kasema mengi pia ikiwemo asimamapo basi mungu kasimama. Kwa kifupi tupo katika zama za wateule na wawakilishi wao. Hakuna makosa, kuna mipango mingi tu itakayotekelezeka ki mungu mungu.
Kwa sasa wanaadhibiwa wale watabiri waongo wanaodai mteule wa mungu atakufa maana analeta madhara makubwa sana kwa maendeleo ya nchi kwa kutamka maneno kama hayo. Wakiisha manabii wa uongo ndio mipango itatekelezwa kama vile kuwajibisha watu wenye makosa madogo madogo mfano wa kina Lugumi n.k. Tumuombee mkuu kwa dhati tu ili afanikiwe kuangamiza watabiri waongo maana hicho ndicho kipaumbele cha sasa. Ameen
 
Mkuu ni kama mchezaji aliyeko bench anaona nafasi kibao za kufunga. Akiingia uwanjani anakosa hata bao la wazi. Sasa hiv inatumika nguvu kubwa kuuaminisha umma kwamba kuna upambanaji wa ufisadi na mahakama ipo lakini kigugumizi cha kuanza kazi tayari na kimepewa jina ni makaburi!! Njia pekee ya kudhibiti ukweli ni kuminya demokrasia. Viwanda vinavyohubiriwa saa hii waziri wa viwanda kila siku anatoka na single mpya, mara napiga sound tu, Dangote anataka vya kunyonga nk.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…