Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Mtu ambaye hakujiandaa kuwa raisi kufanya mambo kama yale siyo kosa lake .
Ulishaona wapi raisi wa nchi gani ?anateua watu wasiokuwa na taaluma kwenda kuwaongoza wananchi .
Magufuli kasema mubashara kabisa kua alikua anabip tu URAIS mara kashangaa kapiga,kama alibip 2020 akigombea tena atasemaje?
 
I am just thinking what if tatizo halipo kwenye gari, yani abilia tumeona namna matairi yanavyo badilishwa kila siku, mara cabreta, juzi tulimwaga oil, lakini wapi gari bado halisongi.

Kondakta na mpiga debe hawana tatizo kwakua wanafata maagizo ya dereva, tumesha badili kila kifaa tulichodhani kibovu kwenye gari lakini hatuoni mabadiliko wara hali ya gari kusonga mbele na safari.

Dereva huyu tumemuajiri mpya baada ya kudhani yule aliyepita hawezi kuliendesha gari letu, dereva wetu alikuja kwa mbwembwe sana kama kuvuta mafuta kwa kasi kama gari linataka kuondoka alipiga honi kwanguvu mpaka abiria wa mabasi mengine wakatamani kama wangejaliwa kumpata huyu dereva wetu mpya.

Lakini baada ya muda kupita tumekaa kwenye basi masaa kadhaa hatuoni dalili ya safari kuanza na wale wauza bidhaa kama pipi na maji abiria wameanza kushuka mmoja mmoja kutokana na tozo kubwa inayodaiwa na dereva huyu.

Abiria tumechoka na kuanza kukata tamaa kwa kua njaa imetawala na hatuna matumaini ya kufika tuendako leo wala kesho.

Kwa namna navyoona kuna swali nikajiuliza vipi kama tatizo sio gari letu hili, gari ni zima kabisa vip kama tatizo lipo kwa dereva.

Vipi kama dereva hana uzoefu wa kuendesha gari na hataki kusikia ushauri wa abiria?

Tatizo kama sio dereva nini chanzo cha gari kutosonga mbele?
cbe9a1477e32fe85c6b86094dd7eecca.jpg
 
On behalf of my self and people of JF napenda kukujuza kwamba gari linasonga na lina kasi wanaodhan gar ni bovu ni waharbifu waliokuwa wanaitekenyatekenya ili ipelekwe kwa Fundi wapige deal,kwa mfano zile gari za Shirika la Posta zimejazwa mafuta wakat hazitembei we unaonaje sio kama wapiga deal kwahiyo gari inasonga mkuu kma Zisonje...........
 
Nyie tu ndo mmpepigwa opofu.

Sisi tumeshafika gairo tunaitafuta Dodoma.

Kaeni tu mnalalamika kuja kushituka 2020 hiyoooooooooo.
 
Tatizo Dereva alikuwa konda, kapewa usukani kama Zali, hakuwahi waza kama kuna siku atakuja kuwa Dereva miaka yote aliyokuwa konda, sasa gari toka lianze kuondoka Gia ni ile ile number 1, sio mlima, tambalale au mteremko. Utaalamu wa kubadili Gia hana, zaidi ya kukanyaga mafuta.
 
Nyie tu ndo mmpepigwa opofu.

Sisi tumeshafika gairo tunaitafuta Dodoma.

Kaeni tu mnalalamika kuja kushituka 2020 hiyoooooooooo.
Huna tofauti na abilia zuzu, aliyepanda gari akaona miti inarudi nyuma kwa kasi akashangilia eti "miti inatembea au kukimbia"
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!

Naona anaturudisha nyuma kwenye tope na mabonde,na bahati mbaya engine nayo imenoki
 
Akupeleke kwani wewe umekuwa zombie? Raisi Magufuli hayuko hapa kukupeleka wewe popote pale, bali wewe ndiyo unatakiwa ujipeleke mahali kwingine, wewe ndiyo unatakiwa ujitoe hapo ulipo na kwenda sehemu nyingine, wewe ndiyo unatakiwa ujifungue minyonyoro uliyofungwa na fisadi Lowasa, Mbowe & Co. na kuwa mtu huru Raisi Magufuli hawezi kulifanya hilo na wala siyo kazi yake!
Hapa hatuongelei Lowassa, Mbowe, wala Co.Tunaongelea Dira/direction ya JumaPondaMali Haipo bayana. Usitutoe kwenye mstari, anzisha Uzi mwingine. Hapa tunataka tujue tunaelekea wapi na JPM.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom