Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Jamaa wanasema awamu ya nne zilipigwa Richmond na Escrow za kutosha lakini maisha yalisonga..... saivi michango ya rambirambi wametaifisha lakini bado haitoshi...

Watu wanauliza wale wazee wa mjini wakiungurumisha escrow nyingine awamu hii nadhani nchi itatangazwa mufilisi
 
Tangu aingie biashara nyingi zimefungwa,watu hawana pesa, mahoteli yamefungwa au kubadilishwa kuwa makazi
Tangu aingie ajira zimefutika,
Tangu aingie idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu wanaopata mikopo imeshuka mno! maelfu ya wanafunzi waliochaguliwa vyuoni wamashindwa kuripoti kwa kukosa ufadhili
Tangu ameingia watu wanabomolewa tu makazi yao,
Tangu ameingia hata shughuli za kisiasa nazo zimepigwa marufuku,
Tangu ameingia maisha yamekuwa ya shida sana,wengi wanakula mlo mmoja kwa siku
Tangu ameingia bunge live limezimwa, ile furaha ya wananchi kufuatlia kinachoendelea bungeni imetoweka
Tangu ameingia wizi na ajali zimeongezeka sana pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya,
Tangu ameingia wafanyakazi hawajapandishwa madaraja wala kulipwa stahiki zao,
Tangu ameingia maisha watu ni hofu mtindo mmoja
Tangu aingie barabara na madaraja hayajengwi tena
Tangu aingie hakuna maabara wala mashule yanayojengwa tena
Tangu aingie ni matetemeko na ukame tu katika nchi
Tangu aingie mapambano ya wafugaji na wakulima
KWA UFUPI ILE NEEMA NA BARAKA KATIKA NCHI ILIYOKUWEPO IMETOWEKA
Lipa kodi, wewe ni mpiga dili, ulizoe kuibia watu maskini
 
Kwan mpka sasa umefanya jitihada gn kujitoa hapo ulipo mbn yote unayolalamika ni kama yako ndani ya uwezo wako

Em acha kuwa na fikra mgando serikali ni wewe mkuu

Under the same circumstance unalalama jukwaani umu na mashairi yako ka tenzi za rohoni wenzio wanapiga kazi na kugonga cheers jioni and life goes on...

Shtuka mkuu
 
Tangu aingie biashara nyingi zimefungwa,watu hawana pesa, mahoteli yamefungwa au kubadilishwa kuwa makazi
Tangu aingie ajira zimefutika,
Tangu aingie idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu wanaopata mikopo imeshuka mno! maelfu ya wanafunzi waliochaguliwa vyuoni wamashindwa kuripoti kwa kukosa ufadhili
Tangu ameingia watu wanabomolewa tu makazi yao,
Tangu ameingia hata shughuli za kisiasa nazo zimepigwa marufuku,
Tangu ameingia maisha yamekuwa ya shida sana,wengi wanakula mlo mmoja kwa siku
Tangu ameingia bunge live limezimwa, ile furaha ya wananchi kufuatlia kinachoendelea bungeni imetoweka
Tangu ameingia wizi na ajali zimeongezeka sana pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya,
Tangu ameingia wafanyakazi hawajapandishwa madaraja wala kulipwa stahiki zao,
Tangu ameingia maisha watu ni hofu mtindo mmoja
Tangu aingie barabara na madaraja hayajengwi tena
Tangu aingie hakuna maabara wala mashule yanayojengwa tena
Tangu aingie ni matetemeko na ukame tu katika nchi
Tangu aingie mapambano ya wafugaji na wakulima
KWA UFUPI ILE NEEMA NA BARAKA KATIKA NCHI ILIYOKUWEPO IMETOWEKA
WAPIGA DILI MTALIA SANA !
 
jidanganye tu, wengi wanaoumia ni wananchi wanyonge
Kabla ya uchaguzi tuliingia kwenye maombi, sijui nini kinaendelea?. Baada ya hotuba ya Kagera na mengineyo wapedwa wengi wanajiuliza kuwa MUNGU WETU MKUU ana siri gani?. Tunaamini kuwa MUNGU anampango mzuri kwetu.

MUNGU alituongoza tukamchagua.

MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
MTOA MADA INAONEKANA ALIKUWA MPIGA DILI MKUBWA MAGU AMEBANA KILA KONA HANA NAMNA ,FANYA KAZI ACHA MAJUNGU , HUNA NAMNA YA KUMWONDOA RAIS MADARAKANI HADI MUDA ALIOCHAGULIWA UISHE ,NA UKIISHA ATAONGEZWA MWINGINE KWA KAZI NZURI AIFANYAYO ,UTAISOMA NAMBA TU NA BADO HIYO NI TRELA ,MOVIE YENYEWE BADO
 
vumilia tu yana mwisho

Sawa Mkuu;
Lakini maumivu yanazidi.
Bei za bidhaa muhimu zipo juu, kamshahara kale kale, motisha hakuna, viposho posho hakuna na watoto wanataka kusoma, kwa kweli mkuu we acha tu, mambo ni magumu.
 
Za asubuhi wana-JF ?

Kila mwezi wa 6 bunge hukaa kupanga bajeti ya mwaka wa fedha na 2015 Serikali ya awamu 4 iliandaa bajeti yake ya 2015/2016 ambapo ilitenga fedha kwa ajili kuajiri watumishi wa kada mbalimbali na mambo mengineyo lakini cha kushangaza mpaka mwaka wa fedha umeisha hakuna aliyeajiriwa inamaana fungu la kuajiri watu imeliwa ? Duuuuh awamu ya 5 kiboko na kwa utapeli tu hawajambo.

Michango ya Kagera imeliwa na fedha za kuajiri watu alizotenga Kikwete pia zimeliwa bado ahadi nyingi kama za mikopo kwa elimu ya juu zimekuwa za uongo aaaaah inaniwia vigumu kuiamini hii serikali ya awamu tano.
 
Huyu mtu anifanya yeye ni mwema sana lakini kama kweli haya yanafanyika kwa ridhaa yake basi hatuna budi kuanza kujiuliza ni mangipi inawezekana yanafanyika nyuma ya pazia bila sisi kuyajua na ambayo yanaweza kuwa ni kwa manufaa yake binafsi?

Mtu huyu ninaanza kuwa na mashaka nae sana na huenda akawa ni hatari kuliko wote tuliowahi kuwajua/kuwasikia.
 
Huyu mtu ni zaidi ya hatari Mkuu..
Kila nikiwaza walichofanyiwa CUF kwenye pesa zao za ruzuku...
Naona huyu jamaa ana kila dalili za kuwa mtu katili sana.
 
Habari wakuu,

Chief wetu tangu apewe madaraka sijawahi kumwelewa anaongea mambo ya ajabu ajabu hana jambo jema la kujenga yote kwake ni kubomoa tu, hanaga maandalizi cha kuongea na kutoongea, hapo nyuma viongozi wenzake waliandaliwa hotuba, walijiaanda nini cha kusema hata kama ni nje ya hutuba lakini kinafata misingi ya uongozi, ila kuna kitu nimependa kutoka kwake, tangu na tangu anahubiri kubana matumizi kwa mambo ambayo sio ya msingi na nimeona sehemu nyingi anawaambia hata watumishi wake kubana matumizi..

Huu utaratibu ni mzuri kwangu, kwakua sipati chochote kutoka kwake hata nikimsikiliaza mpaka mwisho. Hivyo basi nachofanya kwa sasa akianza kuongea tu nazima TV, naswitch off kabisa nachomoa cable zote naweka pembeni, nafanya hivyo kubana matumizi hizo unit nitakazotumia kumsikiliza bora nibane kwa wakati huo ili kwa baadae nizitumia kuangalia katuni..

Nawashauri wenzangu mfanye kama mimi tubane matumizi vizuri..

[HASHTAG]#Mohagachi[/HASHTAG]
Hii imenipendeza
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom