sio tunabwabwaja , sema unaona aibu mlivyo feli.Chadema mmeguswa pabaya saivi mnabwabwaja tu.
Chadema mmeguswa pabaya saivi mnabwabwaja tu.
Active Mod 2 Mod 3 Mod 4 huu uzi kwanini mmeuunganisha?Wacheni watu tupaze sauti kupitia huu mtandao.Kama ni kukopa tu na kuanzisha miradi hata chama kichanga kama ACT-Wazalendo kisingeshindwa maana wataalamu wa ku-negotiate mikataba/mikopo wapo wengo tu ndani ya serikali na hata nje ya serikali.
Kama ni kununua ndege hata chama kama TLP kisingeshindwa kwani ni swala tu la kuamua kuagiza ndege bila kujali mambo mengine yatakuwaje.
Ukiacha mambo hayo,maswala mengine yote yamewashinda na sasa wamebaki kukimbizana na wapinzani na kuibua matukio kila kukicha.
Uchumi haueleweki(hata mh.Bashe ni shahidi) ,hifadhi ya Taifa ya chakula inazua maswali, mikopo ya wanafunzi shida(kuna baadhi ya vyuo wamezuia vyeti vya wahitimu wa mwaka jana kwasababu Bodi haijalipa ada za watu waliomaliza vyuo. Mfano St.Johns University).
Uhakiki wa watumishi umegeuka wimbo wa Taifa.Madai na malimbikizo ya watumishi hakuna anaejua watalipwa lini kila siku wanapigwa "sound"!
Hivi sasa wameahamia katika vita ya madawa ya kulevya lakini ulizeni kwenye bajeti ya maendeleo mwaka wa fedha 2016/2017 walitenga shilingi ngapi kwa ajili ya kupambana na madawa ya kulevya.
Jiulizeni miradi ya maendeleo kwa fedha za ndani imetekelezwa kwa asilimia ngapi huku miezi 8 ikiwa inakatika.
Waulizeni mpaka sasa wamepeleka fedha kiasi gani(asilimia ngapi) kwa ajili matumizi ya kawada kwenye Idara, Wizara na Taasisi za serikali,n.k
Alafu ulizeni ni fedha kiasi gani zimetumika kuendesha kesi zinazohusu wapinzani ikiwa ni pamoja na gharama za kuwakamata na kuwasafirisha ili wakajibu mashitaka na muangalie aina ya hayo mashitaka.
Kuhusu Tanzania ya viwanda majibu unayo tumejenga viwanda vingapi mpaka sasa na vya size gani(binafsi sijaona).
Ukitafakari haya yote kwa makini ndio utajua ni kwanini hivi sasa wanaelekeza nguvu nyingi kwenye haya matukio huku watu wakihoji tu inakuwa ni kosa.
Something is better than nothing-Jk ulijitahidi.
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.
Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.
Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.
Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu
Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?
Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.
Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!