Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
salamu wanabodi!
ghafla nimejikuta sina furaha, sina amani na wala sifurahi tena kuitwa mtanzania.Mwanzoni alipo ingia madarakani nilimpenda sana Rais Magufuli kwakuwa mambo mengi aliyo yafanya yalikuwa yana rudisha Tanzania tuliyo itaka.Baada ya miezi michache akageuka kuwa mbinafsi, anaonesha chuki za wazi kwa watumishi wa umma, Hafuati misingi na kanuni za uendeshaji wa taasisi za serikali, hafuati matumizi sahihi ya fedha za umma, kimsingi amegeuza Nchi hii ni mali yake binafsi.

Kwanini ghafla simpendi? Fikiria Rais mwenyewe aliagiza uhakiki wa watumishi wa umma akisisitiza wasio na sifa waondolewe kwenye payroll.Zoezi lile liliwagharimu watumishi wa umma muda na fedha nyingi kufuatilia taarifa zao ili zihakikiwe.Jumla ya watu 1887 wamepoteza ajira baada ya kubainika taarifa zao za taaluma kuwa na kasoro ama mapungufu.lakini alisimamisha nyongeza za mishahara na kulipa mishahara ya madaraja mapya kwa kisingizio hiki.Leo Bashite kajulikana hana vyeti anapata kigugumizi kumtoa kwenye utumishi wa umma! kwanini? ni msukuma mwenzake!! ni mkabila.

Kwangu mimi kitendo cha Magufuli kuidhinisha ujenzi wa uwanja mkubwa wa ndege Chato ni matumizi mabaya ya fedha za umma.uwanja ule nani atatumia? Kama anawapenda watu wa Chato ni bora angewajengea chuo kikuu kwani hata mtu mojammoja angeweza kufaidika na uwepo wa chuo kikuu kuliko uwanja wa ndege.

Amevuruga taratibu serikalini.Magufuli kwa sababu za kibinafs kabisa ameajiri wakurugenzi na Ma DAS nje ya kanuni za utumishi wa umma.sasa hivi watumishi wa umma hawana ari ya kazi kabisa.

Matamko yake mengi yamenifanya nifikie uamuzi wa kuto kumsikiliza kabisa. Huwezi kuwaambia wabunge wa ccm walio panga kwenda kumjulia Lema gerezani ni usaliti wa chama. Najiuliza Lema aliwekwa ndani kwa maelekezo ya Chama? siamini. Hivi Magufuli hajui kuwa kuna wana ccm walio oa wanachadema? hivi hajui kuwa ndani ya familia moja unaweza kuona wanachama wa vyama vyote? huko ni kuwagawa watanzania.

Magufuli huwa anaomba tumuombee kwa Mungu, sawa, mbona yeye haoneshi kuwaombea watanzania wawe na amani upendo na kuvumiliana? CUF,Kwenye vikao halali wamemfukuza Lipumba, lakini fedha za ruzuku ameruhusu apewe mtu ambaye siyo mwanachama yaani Lipumba! Magufuli ni msimamizi namba moja wa fedha za umma, kwanini anaruhusu ujinga huu wa msajiri wa vyama? Aheshimu maamuzi halali ya vya vingine. kulazimisha Lipumba kuiongoza CUF iko siku itatuletea maafa makubwa sana.

Kuna manung'uniko kuwa wateule wake wengi wanatoka kanda pendwa.Jambo hili siyo la kulipuuza. teuzi lazima zifuate kanuni za kitaasisi.Lakini pia zizingatie gender balance, dini,na ziwe na mtawanyiko mzuri kikanda. watumishi wa umma wanao tumbuliwa sababu za kutumbuliwa kwao wengi ni nyepesi mno hivyo kuleta maneno kuwa ni kulipa visasi.

Siku hizi watu hawapendi kuangalia au kusikiliza taarifa ya habari ya saa mbili usiku. Ni kama wamechoka na mabadiliko yasiyo na maana.

Mapungufu ni mengi, ndio maana nasema binafsi namuombea atawale amalize muda wake hata kama ni miaka kumi,huenda Mungu anataka kutufundisha kitu, ila siku akimaliza nitafurahi sana ingawa nitakuwa na miaka 89.
unauhakika gani kama atamaliza muhula? ndo kwanzaaa ana ka mwaka kamoja kameisha... iliyobakia ni majaliwa kuikamilisha... omba apumzike au apumzishwe
 
Mnakula matapishi yenu hata kabla ya nusu ya Muhula wake kufika.
vitendo vyake vya kibaguzi na upendeleo vimewachosha siyo tu wanachama wa ccm bali pia watanzaniaq kwa ujumla wao. nani anapenda utawala wa visasi? kutesa watu, kufukuza watu kazi bil ushahidi thabiti!
 
Hivi, ukimsikia mtu anakwambia "msema kweli ni mpenzi wa Mungu, mimi huwa napenda kusema ukweli..." halafu eyeee, ukifanya hivi nitafanya hivi. mimi ni mkweli....

lakini hapohapo kunakuwa na double standard kwenye kuwajibisha watu walioko chini yake, wengine wanaadibishwa, wengine wanaachwa waendelee kutamba, na hapohapo mtu huyo anayemtaja Mungu, anaonyesha visa na visirani vya waziwazi...na ikifika siku ya kusali huyo anaenda kugusa msalaba na kujifanya anaombewa. UTAMWELEWAJE MTU KAMA HUYO?

lets just be serious, sisi sio watoto wadogo ati. tuna akili zetu na elimu zetu..tujadili hili kwa ukweli toka moyoni ili wanaoongea kauli kama hizi wajifikirie kwanza kabla ya kufumbua mdomo.
 
"Huyu Ndiye Mwanawangu Mpendwa Ambaye nimemchagua, msikilizeni"
 
1.Rais kukosa busara mbele za wananchi badala yake kuhubiri chuki,ubaguzi na vitisho
2.Nchi kuongozwa kwa matamko yasiyo na ticha kwa maendeleo na ustawi wa taifa e.g bila cheti cha kuzaliwa hakuna kuoa,mtu mmoja kuwatisha wengine kuwafukuza mkoani kwake ilikhali naye yu ugenini
3.Serikali kustisha ajira kwa miaka mpya kwa miaka miwili bila ya kuwa na mbadala ingawa bado kuna upungufu wa wataalamu katika jamii m.f.n sekta ya afya,elimu..
4.Nchi kuendesha kwa vitisho na visasi vinavyopelekea kuiweka rehani amani na demokrasia yetu iliyokuwa imeanza kuzaa matunda kwa kuvutia wawekezaji
5.Tumbua tumbua za watumishi wa umma bila ya kufuata sheria hivyo serikali kujiongezea mziko wa watumishi wanaoendelea kulipwa mishahara pasipo kuwa na kazi hivyo kuongeza mzingo kwa taifa
6.Serikali kuendesha nchi bila ya kuwa na dira thabiti wamebaki kudakia kila lionekanalo mbele ya viongozi.tunashindwa kuelewa ni nchi ya viwanda au vi wonder na kiku za shelawadu
7.kuzuia bunge mubashara kwa kile kinachodhaniwa kuwakomoa wapinzani na kurusha mubashara sherehe binafsi katika tv ya taifa bila kujali kodi za walala hoi zinazoteketea bula faida
8.Kuendeshwa kwa chuki za wazi kwa wapinzani kwa kuwaweka rumande kwa kile wasemacho uchochezi.imekuwa nchi ya kidikteta asemalo MTUKUFU linakuwa sheria
9.Kudolola kwa huduma muhimu za jamii huku serikali ikitoa matamko yanayokatisha tamaa m.f.n ni ukosefu wa dawa kwenye hospitali za umma,upungufu wa chakula uliosababishwa na ukame,wanafunzi kusomea chini ya miti kwa kutekeleza sera ya mwendokasi
10.Kukosekana kwa pesa za mikopo kwa wanafunzi wa vyuo hivyo kwenda kinyume na moja ya sera zake katika uchaguzi[emoji22][emoji22][emoji22]



HIVYO NI MUDA KWA KIJANA WA KITANZANIA KUTAFAKARI MUSTAKABALI WA WANAE SASA



USIRUDIE KOSA 2020

R.I.P ZAMA ZA MAWE JEMBE NA NYUNDO
 
Hadithi za abunuasi, endelea kujifariji! CCM ni chama cha watanzania milele na milele!
 
Mwenye Enzi Mungu azidi kukubariki rais wetu
 
Mtazoea tu mabadiliko

Mazoea ya kuishi mlivyoishi zamani ndio msahau


Mh. JPM oyeeeeeee

Bila kumsahau

Kipenzi cha Watanzania naye ni

Mh. Makonda oyeeeeeee


Hapa kazi tu
 
Mtazoea tu mabadiliko

Mazoea ya kuishi mlivyoishi zamani ndio msahau


Mh. JPM oyeeeeeee

Bila kumsahau

Kipenzi cha Watanzania naye ni

Mh. Makonda oyeeeeeee


Hapa kazi tu
Hivi wewe mama/binti kila CCM na Serikali ikitajwa hata kama ni kwa facts wewe ni kushabikia tu na kuitetea?Acha hizo jiongeze basi sio kila kitu ni kuweka ukada mbele mama/binti.Wakati mwingine heri ukae kimya kuliko kuchangia kinafiki!!!
 
Hivi wewe mama/binti kila CCM na Serikali ikitajwa hata kama ni kwa facts wewe ni kushabikia tu na kuitetea?Acha hizo jiongeze basi sio kila kitu ni kuweka ukada mbele mama/binti.Wakati mwingine heri ukae kimya kuliko kuchangia kinafiki!!!

Ha ha haaaaa

Nashukuru kwa kuninoti kuwa mimi nimeshikilia msimamo wa kutetea hao wasio na tatizo lolote.

Uhuru na uamuzi ni wangu ndugu, na mimi naadika yanayojiri sifati mkumbo wa wanaovutwa na wachache.

Makonda oyeeeeeee

N.b. mimi sina chama
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom