Watu wengi makini wamekuwa kimya juu ya mwenendo wa utawala wa JPM, Viongozi wengi wameamua kufunga mdomo. Serikali yake imekuwa ikitumia nguvu sana katika kukandamiza hoja kinzani. Kwanza walianza kwa kukata matangazo ya bunge live kwa kibwagizo cha hapakazi tu, baadae wakaanzisha kamatakamata katika mitandao kwa kutumia cybercrime act, sheria ambayo mpaka sasa imekamata wapinzani tu, baadae wakapiga marufuku mikutano ya kisiasa na maandamano mpaka 2020 kwa kigezo kwamba hapakazi tu, wakapeleka muswada bungeni kubana vyombo vya habari, alipomaliza nje akarudi ndani ya chama chake, akajijenga zaidi,akautishi mhimili wa bunge, mara kadhaa ameelekeza mhimili wa mahakama kutenda anavyotaka. Haya yote yamefanyika kwa nia njema? Je mtu mwenye nia njema anaweza kufanya haya?
1. Kuamua matumizi ya fedha bila kufuata utaratibu wa kisheria, na bajeti iliyopitishwa na bunge?
2. Kuagiza ujenzi wa Airport chato huku nchi inakabiliwa na changamoto lukuki zinazogusa maslai ya umma?
3. Kununua ndege kwa cash bila kufuata taratibu za manunuzi?
4. Kufungia akaunti za manji, kumhusisha na madawa,kumnyanganya mali zake, kudai sio raia wa tanzania?
5. Kufumbia macho ufojaji wa vyeti kwa RC.
6. Kufumbia macho tuhuma za RC kumiliki mali za watuhumiwa wa madawa ya kulevya, baadhi kuziuza na nyingine kuzitumia.
7. Kufumbia macho uvamizi wa ofisi ya kituo cha redio ili kulazimisha tukio kurushwa hewani.
8. Kufumbia macho matumizi ya anasa ya sherehe ya RC aliyorushwa live katika tv huku akidai anabana matumizi.
9. Mkuu wa Mkoa kuhongwa gari na GSM na kubadili plate namba na kuweka ya RC
Binafsi nadhani JPM na Albert wanashirikiana katika dili za upigaji, wameamua kujinufaisha kwa kivuli cha uzalendo. Kwa hali hii bado wanaoweza kumwamini ?