Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.

Anatupeleka kwenye moto wa gesi kutuuuunguza
 
Tutafika anako taka tufike ni suala la muda tu.
 
Rais wetu anatupeleka nchi ya ahadi ambayo matunda yake yanaonekana hata na kipofu na wananchi wana enjoy maisha mubashara,mapato yameongezeka,wanafunzi wanasoma bure,madawa hospitalini imebaki historia na watumishi wa umma hela yao ya mshahara imekuwa na thamani#unataka uishi nchi gani zaidi ya hii!tunakuombea rais wetu uendeleze yote haya na kuzuri zaidi na reli yetu ya standard gauge umeshasainiwa na ujenzi utaanza muda si mrefu hata hao wenzetu wa kenya reli yao tumewatanguliza kwa baiskeli ya mbao!
 
Kama kupotea umepotea ww,nchi iko poa tunaelekea Tanzania ya viwanda kama hautaki kula malimao subiri 2025
 
Tunapelekwa kwenye ujima....utekaji,uuaji....na kuishi km mashetani......hakuna tena utawala wa sheria zaidi ya vitisho tu........tunaelekea kwenye dimbwi la ufukara.
 
bei ya unga juu
bei ya mchele juu
bei ya sukari juu
ujenzi ni shidah
nguo nazo ni bei ghari
.......hivyo ni basic needs......
projects alizozipa kipao mbele
1. tanzania ya viwanda
2.ajira
3.mikopo
4.maisha mazuri kwa kila mbongo
5.kupambana na mafisadi
nakuendelea
........alizozifanya.....
1.kununua ndege
2. kutengua teua
........nyie endeleeni kumtetea mkazani kunakitu kitakacho badirika...maisha yatawaendea kombo mpaka mkome......
2020 mpeni tena ili mverify kuwa maisha na huyu jamaa hayaendi kabisa...anaakili ndogo sijawah kuona
 
Nchi ya viwanda kuifikia 2020
Ajira zitakuwa tele
wanafunzi watapata mikopo
wafanyakazi wataboreshewa mishahara
machinga Na bodaboda mm nitawakomboa.
uchumi WA tz utakuwa km singapore

sasa 2017

wabunge wanalia njaa.
wananchi wanalia Hali Ngumu
wafanyskazi nyuso zimejaa makunyanzi
bodaboda Na polisi sisemi

At the moment

Nchi ina hofu,watekaji wanatia hofu,wasanii kilio,wabunge kilio,raia kilio.

madaraka ya kulevya( kimyaaa)

twafaa

assadsyria3
 
Mkuu assadsyria3,
Kwani kuna specific time frame iliwekwa kutimiza hayo?. Subiri basi ikifika 2020 hayo ndipo upandishe uzi huu.

Paskali
 
Ni kweli ni sahihi tulibugi watanzania naimani tokea nizaliwe hii miaka mitano ndiyo ya hovyo kuliko zote ,naamini kweli hichi kiti sio cha kufanyia majaribio maisha yamekuwa magumu sana kila bidhaa bei juu alisema hakutakuwa na gep kubwa baina ya watanzania ni vipi tena maskini tunazidi kuumia ,bashite hana ushauri inabidi amfate jk ampe mpango kazi na jinsi ya kuishi na watu kukuripuka,matamko,mateuzi hayana tija kwa MTU wa hali ya chini . kwanza hajui vyeti feki ambavyo vimeishia kolomije,hajui Ndege ambazo hazipandi wala kutarajia kupanda anachotaka ni kula tu,aishi kwa furaha .na uhakika miaka mitano itaisha hamna kiwanda cha maana na ndo hivyo wizara kapewa msanii wa poroja hakuna kiwanda hapo

Kabana matumizi wapi wakati mwenge unakula hela ,bashite anaenda kula raha Paris Dubai marekani nahisi kabisa Mali alizonazo bashite ni zake ni swala LA mda tu utasema ,hamna nidhamu ya kazi yani ni kama zamani tu .

Nasema hamna kitu huyu jamaa atafanya zaidi ya kuweka watu gerezani
 
Tena mkuu atazidi kuchanganyikiwa maana sasa hivi kizazi cha kuhoji nyuma ya keyboard kinazidi kuongezeka. Na yeye kila akisoma habari za kwenye social media anazidi kupagawa.

Bora wenzie kina Ben na Mzee Ruksa walitawala kipindi cha analog hawakupata hizi challenges za mitandao ya kijamii.
 
Kilimo chetu giza!
Uchumi wetu giza!
Ajira mpya giza!
Elimu yetu giza!
Madini yetu giza!
Karibu kila sekta giza!

Na sasa hata usalama wetu ni giza totoroooo!
Ni kutekana kila upande!
Si wabunge si walala hoi.

Eee Mwenyezi Mungu tunusuru na janga hili.

Binadamu wanawezaje kuwindwa ndani ya nchi ya wazazi wao mithiri ya majangiri wawindavyo ndovu?
 
Tangu huyu bwana apate kiti cha urais amani imepungua kwa kiasi kikubwa ,matukio ya utekaji yameongezeka, rushwa imeshamiri huku yeye akibariki kwa kuita ni vihela vya kubrashia viatu tu hivyo

Pia na hata mapato ya nchi yamepungua na yanazidi kupungua kila kukicha kwa kufanya maamuzi ya kukurupuka .

Huyu bwana tangu akwae hicho kiti amekuwa akiwagombanisha vyombo vya usalama na raia imefika kipindi raia anaogopa vyombo vya usalama kuliko vibaka na majambazi.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…