Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Hahahaaaaaaaaaa ma digo, post: 16332591, member: 268964"]kama hujui unapokwenda... basi huwezi kupotea.[/QUOTE]
Hahahaaaaa
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Asiyejua maana haambiwi maana-wahenga walisema ! Wewe una PREDUDICE ndo maana huoni kinachoendelea !
 
Bus linaelekea Rwanda ingawa break zimeshakata sijui kama tutafika salama
 
Kauli ya Rais wetu mpendwa isemayo mtaishi kama mashetani nani mpaka sasa anaishi kama mashetani kati ya sisi masikini na matajiri.
 
Kwa ujumla nakerwa na mengi mnayotufanyia watanzania. Serikali yako ni bora msifanye baadhi ya mambo maana kuna mambo mnafanya hata zero brain anaona mnatudharau. Kwanini mnajivua nguo hivyo!? Kwa mini mnachukua maamuzi bila kufikiria?

Hivi kweli inaingia kichwani kusikia eti uhakiki haujafanyika kwa wanasiasa na wateule wa raisi kisa sifa yao ni kujua kusoma na kuandika tu? Mbona wakati wa kuteua (I'm not sure enough) wakuu wa mikoa/mabalozi uliitisha vyeti? Au kwa vile wa karibu yako umpendaye ameguswa katika hili ndo ukaona utupoteze maboya?

Mimi nimekaa darasani miaka yangu 21 nikisoma nikiamini nitakuwa bora kimaisha ukilinganisha na ambaye hakwenda shule. Jamii inaniangalia na kuthaminisha umuhimu wa kwenda shule na kutokwenda. Sasa hivi ambao wamekwnda stationery na kufyatua vyeti wanalipwa mamilioni Mimi nalipwa laki NNE!!!!! Does it sound? Wewe ni Dr, niambie tu ni sawa????

Wazazi wangu waliuza mbuzi, ngombe na hata shamba nisome, Leo unanipa hela ambayo hata mwendesha Bodaboda anaipata kwa mwezi na zaidi nawe unakumbatia nayo majizi eti kisa ni wateule!!

Kati ya waliosoma ulikosa wenye vyeti halali na kuwapa hizo nafasi hadi uangalie wanaojua kusoma tu na kuandika? Tena wenye vyeti feki!!? Kwa nini uwalinde?

Laki nne inanisaidia nini kama sio kunidhalilisha? Halafu kunikomoa eti unaagiza bodi ya mkopo wazidishe makato ili nizidi kuteseka!! Na posho ukaondoa ili niteseke zaidi!!Naishi maisha ya kijinga. Nasema kabisa kama huongezi mshahara na kushughulikia hao majizi nitakuachia likazi lako. Nitachukua mkopo ninunue bodaboda!! Nina uhakika nitamake 600000+ kwa mwezi.

Nikipata ajali nikifa poa tu. Nasubiria mwezi July na nipo serious. Nimechokaaa!! Watumishi tumejikakamua then tunaonekana mapoyoyo tu
 
[emoji654]Nchi ambayo uongozi sharti ujuwe kusoma na kuandika.
Zero wanaongoza bright and smartest people.

[emoji654]Nchi ambayo wakuu wa mikoa,wilaya,wabunge, siyo watumishi wa umma wakati wanatumikia wananchi.

[emoji654]Nchi ambayo raisi anakumbatia wafoji vyeti na majambazi ambao walitakiwa wawe gerezani.

[emoji654]Nchi ambayo ukiongea ukweli unaonekana mchochezi.
[emoji51][emoji51][emoji51][emoji51][emoji51][emoji51][emoji51][emoji51][emoji51][emoji51]
 
a7c75d72d244c31498b75b2dba5fda4b.jpg

Utadhani mtu mzima anacheza michezo ya kitoto kumbe ndio tunaishi hiviii.....[emoji2] [emoji2]
Salute!...
Kiufupi sana kwa hili la vyeti sijakubaliana hata kidogo na maelezo ya serkali kuhusu vyeti feki,inaonesha wanaokaa kwenye vyombo vya maamzi hakika wapo kwa ajili ya kuteteana tu.na sio kuwatetea wananchi.

"Mtukufu rais usiwe unasema wewe ni rais wa wawanyonge sema wewe ni rais wawanyongwa"


Kuna vitu kwa ulimwengu wa leo,kwa namna tulipofikia unasema unaenda kuwafukuza watu 9932 kazi lakini muda huohuo unasemma hawa wengine wao haina shida,.

Nilichogundua mimi TANZANIA KUGUSHI VYETI WALA SIO TATIZO,Na hasa ukigushi then ukapata bahati ya kuwa mkuu wa mkoa wala hakuna shida.

Sasa maajabu wakuu wa wilaya,na mikoa ndio wanaosimamia uhakiki wa vyeti kwenye maeneo yao,wataitendeaje haki ili hali wao pia waligushi?

Manalipeleka wapi taifa?.

Hao manaowatetea ndio wanakula mishahara minono,wanalindwa na kupewa posho,nyumba,magari lakini eti sharti wajue kusoma na kuandika tu.

Ndio maana watoto mashuleni hawasomi maana hawaoni FUTURE YEYOTE MBELE,mtu anajua kusoma tu anaoishi vizuri,wakati huohuo mtu anakomaa anasoma degree yake miaka kadhaa hata kazi tu kupata ni shida.Then mnataka watoto wasome watasemaje ilinhali mnashindwa ku-demonstrate faida za kusoma na hasara za kutosoma?...ACHENI MAHABA YA AJABU AJABU NA YASIYO NA MAANA KWENYE MAMBO YA MSINGI.
 
Bodaboda wanatuacha mbali mkuu

Ukiwa na boda boda nne, kwa mwezi unakunja karibu milioni,
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom