uttoh2002
JF-Expert Member
- Feb 3, 2012
- 17,060
- 32,400
Kwa ujumla nakerwa na mengi mnayotufanyia watanzania. Serikali yako ni bora msifanye baadhi ya mambo maana kuna mambo mnafanya hata zero brain anaona mnatudharau. Kwanini mnajivua nguo hivyo!? Kwa mini mnachukua maamuzi bila kufikiria?
Hivi kweli inaingia kichwani kusikia eti uhakiki haujafanyika kwa wanasiasa na wateule wa raisi kisa sifa yao ni kujua kusoma na kuandika tu? Mbona wakati wa kuteua (I'm not sure enough) wakuu wa mikoa/mabalozi uliitisha vyeti? Au kwa vile wa karibu yako umpendaye ameguswa katika hili ndo ukaona utupoteze maboya?
Mimi nimekaa darasani miaka yangu 21 nikisoma nikiamini nitakuwa bora kimaisha ukilinganisha na ambaye hakwenda shule. Jamii inaniangalia na kuthaminisha umuhimu wa kwenda shule na kutokwenda. Sasa hivi ambao wamekwnda stationery na kufyatua vyeti wanalipwa mamilioni Mimi nalipwa laki NNE!!!!! Does it sound? Wewe ni Dr, niambie tu ni sawa????
Wazazi wangu waliuza mbuzi, ngombe na hata shamba nisome, Leo unanipa hela ambayo hata mwendesha Bodaboda anaipata kwa mwezi na zaidi nawe unakumbatia nayo majizi eti kisa ni wateule!!
Kati ya waliosoma ulikosa wenye vyeti halali na kuwapa hizo nafasi hadi uangalie wanaojua kusoma tu na kuandika? Tena wenye vyeti feki!!? Kwa nini uwalinde?
Laki nne inanisaidia nini kama sio kunidhalilisha? Halafu kunikomoa eti unaagiza bodi ya mkopo wazidishe makato ili nizidi kuteseka!! Na posho ukaondoa ili niteseke zaidi!!Naishi maisha ya kijinga. Nasema kabisa kama huongezi mshahara na kushughulikia hao majizi nitakuachia likazi lako. Nitachukua mkopo ninunue bodaboda!! Nina uhakika nitamake 600000+ kwa mwezi. Nikipata ajali nikifa poa tu. Nasubiria mwezi July na nipo serious. Nimechokaaa!! Watumishi tumejikakamua then tunaonekana mapoyoyo tu
WAKATI mwingine ni haki kufikiri Serikali inakukomoa:
Laki nne inanisaidia nini kama sio kunidhalilisha? Halafu kunikomoa eti unaagiza bodi ya mkopo wazidishe makato ili nizidi kuteseka!!