"Memori fullu!"
Ukigeuka hivi, huyu kacharazwa na Dc, ukitaka kujikuna, huyu kanyimwa dhamana, ukisema uanze kusali, huyu kasepa na rambirambi! Ukitaka kwenda kuoga, huyu anazuia sabuni hadi ulipe deni la ugoro... Ukitaka kuketi kula, huyu ashaagiza uhame mji bila ndala!
Ukitaka kujipumzisha baada ya stress za mchana, buldoza linachungulia dirishani! Ukisema ushike mswaki upunguze wadudu mdomoni, mkemia anataka mkojo apime wadudu wa mdomoni...
Ukitaka kula makande, huyu ashazuia mahindi anasema yasagwe! Ukiinama ufunge kamba za viatu, noah ishafunga breki miguuni... Ukisema ufanye kazi kwa bidii, huyu anataka ukrem jina lake... Ukitaka kulia kwa ghadhabu, unawekwa korokoroni kwa kupigia watu kelele isiyowahusu....
Ukitaka kuandika shairi lako, washakudaka na sheria ya mitandao... Ukitaka kupanda bajaji, washakulazimisha upande pangaboi... Ukimdai bosi mshahara wako, ashakutupia jembe ukalime... Ukikodisha shamba ukalima, jua lishaizidi mvua na hakuna msaada....
Ukitaka kumpeleka mwanao chuo, washakuitia mkopo kwenye ofisi za chama... Ukitaka kwenda Zimbabwe, usharudishwa na ushuzi wa babalao.... Ukitaka kuwa karibu na mema ya nchi, ushaulizwa kama wewe ni "sibling".'.. Ukitaka haki yako, washakulazimisha usimamishe msafara wake....
Ukitaka "kupupu," ushadakwa uoneshe risiti ulikula wapi.... Ukitaka jshshsjsosks, jshdjejsie????(peni imegoma ngoja nijaribishe tena...) nsnsjshdeueuhdisisksks! (Naenda dukani kusaka nyingine)
Ila nikirudi, Hasira zote nazimaliza kwa marafiki wanaopost picha kuanzia januari hadi disemba...... No, sio hao... Ngoja.... Nimekumbuka... Wale wanaohamisha posti za wenzao hawataki kushea, wanazikopi na kuzifanya zao.... Nawablokuuuuuuuuuuuuu hadi vidole viume....
Memorifufjfjdirirrirkkkmmldjdjdieiss!'&#&#$&÷&#