Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Miaka kumi! Hivi kumbe mmeisha badilisha katiba?
Najua umenielewa,basi tu.Mkuu kwani Katiba haimruhusu kama akichaguliwa kuendelea na miaka mwingine mitano baada ya kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano kwisha?Au ni ubishi ule ule wa akina Halima na Lissu.
 
Kupambana kwetu inategemea na Sera bora za serkali kuhusu uchumi wa nchi yetu

Naamin ninaposema Sera bora unaelewa haiiishi kupeleka dawa hospitalin tu

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Any decision you make in life you are responsible for it



 
Mkuu unaweza kuwa na mawazo sahihi katika ego moja but ukaacha kundi kubwa la watu

Mh maguful bado anakosea mambo mengi na asipobadilika uchumi utayumba

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Wasikukatishe tamaa hao mkuu,ni wale Mwalimu Nyerere aliosema watazomea kila jambo jema kiongozi analolofanya kwa niaba ya mapebari.Hao ni makuadi wa mabepari achana nao.Mimi nawaita "huyoo huyoo" maneno ambayo Mwalimu alitumia.
 


Mkuu, nadhani kuna kitu unakikosa. Jukumu KUU la serikali yeyote ni kuweka Mazingira sahihi kwa watu wake wawe na maisha bora. Mazingira bora ya elimu, afya, KILIMO, biashara, MIFUGO n.k.

Sikiliza ninasema Mazingira bora maana yake nini. Rais hakutakiwa kununua bombardier leo. Alitakiwa awaangalie jeshi kubwa la vijana wanaotoka mashuleni kuingia soko la ajira (ambalo halipo) Mfano; pesa ile angejenga mifumo ya umwagiliaji.

Angalia pesa ya bombardier zote hizo zingejenga mtandao wa umwagiliaji ekari ngapi ? Kwa miaka mitano mtandao huo wa umwagiliaji ungeajili watu wangapi? Nchi ingekusanya kodi kiasi gani. Tungepunguza vibaka wangapi ? Hilo ndilo jukumu la serikali. Ni ujinga kuamini mhitimu atarudi kijijini kushika jembe LA mkono.

Wenzetu Singapore, Malaysia. Korea Kusini, serikali waliweka Mazingira mazuri ya fursa, waliwawezesha wananchi. Isitoshe watu wawe huru katika nchi yao, pasiwe na udikteta, mtu mmoja asiwe ndiyo sheria. Samahani nikutoe kidogo.

Uliona kilichotokea Tanga siku za nyuma kidogo. Mama aliyeingia na bango akitaka Rais amwone ili kudai mirathi yake. Siku ya sheria nadhani. Rais alitoa agizo kwa Jaji Kiongozi hadharani, eti Jaji chukua simu ya mama huyo shughulikia shida yake. Ooh my God. Rais anamwamulisha Jaji Kiongozi !!!!? Rais anaingilia Mahakama !!

Acha ile mpya ya awali; Mahakama wamalize kesi haraka na kuwafunga mafisadi ili awape pesa wanayodai !!!? OK katika hali kama hii, Kiongozi Dragoon utapata nchi na wananchi wenye maisha bora. Kwa kusema hayo siwatetei wala rushwa, wakwepa kodi, wala wapiga dili maofisini.

Hao wapo na wataendelea kuwepo maana hata Marekani, Japan bado wapo. Tujitajidi walau tuwe kama Kenya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ufukara au umaskini uletwa na Tawala mbovu ktk Nchi Husika ....
Pili umesema hakuna Rais /serikali inayo gawa pesa kwa Raia zake sio kweli zipo NCHI DUNIAN hugawa pesa kwa Raia zake tena pesa nyingi tu kwa watu wake wote wasio kuwa na kazi ..



Zimwi likujualo......
 
Huu ni ushauri mzuri kabisa

Bila hata nchi kugawanywa kwenye zone kwa wakati huu angeweza kutumia hata wati wanaomzunguka ana washauri,mawaziri, makam rais, majasusi ya kiuchumi nk

Nchi ingeweza kuwa stable tu kuliko saiv tunapiga maktaim

Mh asiamin katika kile kilichopo kichwani mwake tu kuna watu very intelgence and patriotic awatumie

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Kwa maana hiyo unataka watu wasifukuzwe kazi hata kama hawastahili kuwepo kazini? Ndicho hiki kutu mnacholilia?
Kufukuzwa kazi ni makosa ya mtu bnafis haiusiani na uchumi wa nchi kuporomoka au kuganda

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Unataka kusema wananchi wote tunaufahamu wa kitoto isipokuwa kiongozi wetu mkuu?, nauliza hivyo kwa kuzingatia mfano uliotoa wa mzazi na watoto. kwa kuwa watoto wanakuwa bado hawajapevuka kiakili lakini kwa hili la raisi na wananchi wenzake ni mwafaka kwa mfano wako?.
 
Mkuu kuna mambo mengi hayapo sawa
Mfn mdogo
Watumishi wa umma ambao huwa wanapata annual increment kila mwaka toka aingie madarakan hakuongezea unafikiri wamedhulumiwa kias gani mpaka sasa

Na wasipoongezewa kwa 5 or ten years watadhulumiwa shilling ngap

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 

Mkuu, kuna uhusiano mkubwa sana kati ya utawala bora Vs Maendeleo ya nchi. Unajaribu kuonyesha kana kwamba serikali au viongozi wa umma hawana nchango wowote katika maendeleo ya watu. Eti kwamba kila mtu apigane tu kivyake. Huo ni ujinga wako wa mwaka 1947! Kuna uhusiano mkubwa sana, na tena wa moja kwa moja kati ya hivyo vitu viwili.
 
hivi nyie mnaosema vijana wanashinda vijiweni chakula ni serikali inawapa au huwa wanakuja makwenu kuwaomba chakula? niondolee upuuzi hapa
Kuna watu hawajui jinsi watu wanavyopigana mtaan kupata mkate wa siku

Labda hawa wapo ofisi znazozolipa vizur sana

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Hayati Nelson Mandela, aliwaambia wananchi wake kuwa, hawatapata kile wanachokitaka bali watafuata maelekezo yake, na nchi ikasimama kweli. Hii ni baada ya uhuru wananchi wake walitaka vita kuwaondoa wazungu. Haya maneno ya wananchi wa Tz ni sawa na elimu za fursa za ujasiriamali na jinsi zinavyowachanganya wahitimu na wasomi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…