Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kweli wewe ni mjinga kuliko watu wote duniani na mbaya zaidi hujui kama ni mjinga. Nani alikuambia maendeleo ya nchi yanaletwa na mtu mmoja hata hapo kwako maendeleo yataletwa na wanafamilia wote!! Sasa itakuwa nchi?? Ila kukiwa na kiongozi makini anaweza kusaidia kuleta maendeleo!!
Usisahau kuwa uchumi unazidi kuporomokaWanasiasa wapo.
Lakini siasa zetu sio kama hizi zibazofanyika tz,
Kutembeza bakuli hilo ndio nalisikia kwako, sijapata taarifa rasmi.
Kuhusu maendeleo wao wameweza kutofautisha muda wa siasa na muda wa majukumu
Kuhusu kutoa misaada ni suala la muda, udhibiti wa mali asili umeanza, masharti maoya ya uwekezaji umeanza ili uwe na tija kwetu.
Tutaanza kunufaika na maoato yatokanayo na mali asili zetu
Acha Siasa uchwara wa namna hii,Nikupe mifano miwili hai:
MFANO wa 1.
Marekani na nchi za magharibi waliwadharau sana Urusi walipoanzisha kituo chao cha utafiti angani kilichoitwa MIR. Warusi walitumia teknologia rahisi sana ya kupeleka/kurejesha watu na vifaa kwenye MIR yao. Walijifunza mengi kuhusu athari za binadamu kukaa angani kwa muda mrefu.
Wakati wote huu Marekani ilitimbwirika kupeleka mtu mwezini na kumrudisha hai, waliunda space shuttle kupeleka vyombo angani. Mwisho wa siku Wamarekani wakakubali kuwa mission na system za Kirusi ni bora kuliko zao na ndipo wakaomba waungane kujenga hiyo ISS na kutumia system rahisi kama ya Kirusi ya kupeleka na kurudisha wanaanga kwenye ISS.
Mrusi walimdharau mwanzoni lakini mwisho wa siku wakakubali kuwa system za Kirusi ni bora na bei ya chini kuliko zao.
MFANO wa 2.
Kwa kipindi kirefu sana Marekani na Ulaya waliona kuwa mfumo wao wa kibepari (capitalist system) ni bora zaidi na kuwadharau China kuwa mfumo wao wa kijamaa ni duni. Wachina waligangamala na mfumo wao, wengi wakiuita ni wa kidikteta (reminds you of anyone?). Leo hii China imeikaribia marekani kiuchumi na ndio wanaowakopesha Marekani. Marekani inadaiwa mpaka kwenye kope na Wachina.
Imekuaje nchi ya mfumo wa kikomunisti iwapite wenye mfumo wa kibepari? Swali zuri sana.
HITIMISHO:
Usizidharau juhudi za Magufuli katika kuleta maendeleo TZ. Hii nchi ilikuwa haiendelei kwa sababu kila mtu alikuwa anachota toka serikalini tani yake. Sio viongozi wa juu, makampuni ya nje, mpaka mtumishi wa chini kabisa (mesenja) alikuwa amategemea kuchota kutoka hii serikali. Hatua ya kwanza ya kuleta maendeleo ni kuhakikisha hii mianya ya uchotaji rasilmali zetu inazibwa. Magufuli amejaribu kwa kiasi kikubwa kuiziba na ndio maana wale waliokuwa wanategea ule mfumo wa zamani wanapiga kelele kuwa maisha magumu.
Kama Marekani ilivyowakejeli Urusi na Uchina hapo nyuma na sasa wanafuata nyayo zao, vile vile hata watu wanaomkebehi Magufuli kwa sasa watakuja msifia na kufuata nyayo zake hapo baadae.
Mungu nakuona.Acha Siasa uchwara wa namna hii,
Nyota njema uonekana asubuhi Magufuli ana Roho ya visasi tu ndani ya moyowake mbona hili kilamtu ameshaliona?
Kama angedhamiria kuleta maendeleo pia watu wangeshaona.
Hayo maendeleo unayatarajia lini?
Unafikiri maendeleo yanakuja SMG mitutu ya vita au ni kutumia Akili na zingine za ziada pia..
Magufuli kwanza ni muongo juzi alisemakua wakati anaingia madaraki alikuta sukari ni sh 5000 na anataka kutuaminisha hivo unavotaka kutuaminisha.
Magufuli ataendelea kupambana na khaliyake tena khali ya kuendesha nchi kishamba na kutafuta kiki zisizo za maana tu.Swala la meendeleo sahau.
Hlf kuna siku mtu mmoja humu anasema nidhamu ya kazi imeongezeka. Nikamuuliza je hao wanafnyakazi wanafanya kazi toka moyoni au kwa sababu ya hofu? Je hizo huduma zina ubora au ilmradi tu?Mfano suala LA kutoongeza mishahara watumishi ni mbaya mno ni ushenzi tu
Jon anaamini atayaleta yeye,ndo maana anaamini rushwa ataiondoa yeye na anaamini akisafiri kwenda abroad NYUMBANI kutaharibika[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kweli wewe ni mjinga kuliko watu wote duniani na mbaya zaidi hujui kama ni mjinga. Nani alikuambia maendeleo ya nchi yanaletwa na mtu mmoja hata hapo kwako maendeleo yataletwa na wanafamilia wote!! Sasa itakuwa nchi?? Ila kukiwa na kiongozi makini anaweza kusaidia kuleta maendeleo!!
So 2025 atasukumizwa TENA?Ni bora tu ubaki kuwa mjinga kuliko kujifanya mwerevu wakati unajua huyo ndio rais wako hadi 2025.
Mambo mengine ya kuwaza waza haya wakati ukijua hakuna chochote unachoweza kukifanya zaidi ya kupigana na hali yako katika kujiletea maendeleo yako wewe mwenyewe bila kusubiri maendeleo ya Magufuli ni upuuzi.
Unasubiri Magufuli akuletee maendeleo. Waliomtangulia wenyewe hawajaleta maendeleo na hata hao tunaowasubiri wakiingia madarakani walete maendeleo tutasubiri sana na wakiingia hawawezi kuleta hayo maendeleo.
Maendeleo yaanze kwa mtu mmoja katika maisha yake. Hayo ya Magufuli yakija au yasipokuja atajua mwenyewe.
Kwa kuhakikisha wanaopata RAHA ZA AJABU wanaish kama MASHETANIMaendeleo ya kweli yataletwa na watanzania wenyewe na ni kwa kuchapa kazi tu hakuna njia nyingine
MAGUFULI:najua maneno haya ni machungu lakini ndio ukweli asiyefanya kazi na asile
Tulimchagua atuambie ukweli
Hapa ni kazi
2015:Walisema tumpe mudahali inaweza kubadilika,
he still have time
Kwa hiyo kwenye kampenilitudanganya? Sabu mlisema mtaleta maendeleo mbona sasa mnatugeuka?Kweli wewe ni mjinga kuliko watu wote duniani na mbaya zaidi hujui kama ni mjinga. Nani alikuambia maendeleo ya nchi yanaletwa na mtu mmoja hata hapo kwako maendeleo yataletwa na wanafamilia wote!! Sasa itakuwa nchi?? Ila kukiwa na kiongozi makini anaweza kusaidia kuleta maendeleo!!
Kama mkulu anaamini MIKUTANO ya KISIASA inamfanya asiiletee maendeleo nchi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Ipo siku humu baada ya miaka kupita baadhi ya watanzania wasiojua maana ya maendeleo watakuja kuwambia watoto wao kuwa wameshindwa kuwapa huduma nzuri kwa sababu ya magufuli[emoji38] [emoji38] [emoji38]
Siku mwanao atakapoenda peku na ukamsingizia magufuli[emoji38] [emoji38] [emoji38]
Siku familia yako itakapojikunyata kwa njaa wewe ukiwa unamfanyia usaili magufuli na ukamsingizia yeye[emoji38] [emoji38]
Siku utakapojikuta cheti chako kimo ndani kama picha za kumbukumbu kwa elimu yako ili hali hakuna mchango wowote wa elimu yako kwa maisha yako na ukamsingizia magufuli[emoji38] [emoji38] [emoji38]
Hizo siku ndizo utakazojua nini maana ya hapa kazi tuu[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38]
Wamepungua!Sigara Kali, uzuri na ubaya wa demokrasia ni kwamba kila mtu, hata mjinga ana haki ya kuamini atakavyo. Mimi binafsi pia nawashangaa wanaoamini kuwa serikali ya magufuli italeta maendeleo katika nchi hii. Hata hivyo sidhani kama wanaomini hayo ni wajinga na kama ni wajinga basi iko siku ujinga utawatoka na wataufahamu ukweli. Wasi wasi wangu ni kwamba yawezekana ni wapumbavu na kama ni wapumbavu tusitarajie mabadiliko katika fikra.
Hata hivyo nina imani kuwa wapumbavu ambao kwa kawaida huwa ni 'wadanganyika' endelevu, wamepungua mno katika nchi hii; yaani sasa hivi watu hawadanganyiki tena.
We subiri uone nini kitatokea pindi wakitindikiwa na uvumilivu!
Sasa Mwanasiasa anayeahidi Maendeleo kwenye majukwaa hadi anapiga joging UTAMWITAJE?Mpaka leo mnakuja na kutambia Magufuli hafai lakini hamtwambii m badala wake awe nani??
NI UJINGA KWA MTU MWELEWA KUTEGEMEA MAENDELEO KUTOKA KWA MWANASIASA YEYOTE YULE HAPA DUNIANI.
Hakuna nchi hata moja iliyoweza kuwaajiri wasomi wake woooooote waliohitimu kutoka vyuo mbalimbali duniani?
Usomi wa mtu faida yake ni kumtatulia mtu changamoto zake, vinginevyo unakuwa ni utumwa wa aina nyingine tena.
Faida ya msomi ni kutatua changamoto za maisha katika jamii ili jamii ijivunie kusoma kwako, shida inakuja pale wewe mwenyewe unapokuwa changamoto hasi katika jamii yako.
Kuna mifano ya wasomi wachache anbao elimu zao zimetumika kutatua changamoto za jamii zao na hao hutawasikia na kelele hizi.
KILA SIKU UNALIA LIA SERIKALI IKUFANYIE NINI, WEWE UMEIFANYIA NINI TOKA UWEMO HUMU??