Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Kwani Vilibinafsishwa na Upinzani.. si na Hao hao kidumu chama Cha Mapinduzi
 
Kwanza nafahamu kuwa kuna mijitu mioga itafuta huu uzi h

Napenda kuwatangazia umma wa watanzania wote kuwa kinachofanyika nchini sio matukio yanayotokea sio kwa bahati mbaya. Katika jicho la tatu ni wazi Magu anataka kubadilisha katiba kutawala milele. Magufuli

1.Mauaji ya kutisha.

Ni wazi na wengi wetu mmeona matukio ya mauaji ya kutisha yanayotokea toka uhuru wa nchi hii. Tunaanza na Kibiti,watu kupotea,viongozi wa upinzani kupigwa risasi na kuuwawa na hata kuminya demokrasia. Magufuli anachotaka kufanya watu wasiongee na wala wasiwe na maoni juu ya nchi yao na yeye kufanya kile anachotaka kufanya nacho ni kutawala maisha.

2.Utawala wa Mabavu (Police State).

Sasa hivi kama mnavyoona,jinsi gani polisi wameshika nguvu na kutumia mabavu juu ya wananchi. Wanatumia nguvu nyingi kushindana na raia ambao hawana silaha.
Kwa mfano tukio lililosababisha kufa kwa mwananfunzi kwenye basi ni tukio liliopangwa.Haiwezekani katika mtu kwenye basi akapatwa na risasi (point black) kama hakuna aliyedhamiria na kufanya target kuua raia. Huyu mwanafunzi aliuwawa kwa makusudi kabisa.

3. Singularity and popularity.
Magufuli anachotaka kufanya ni kutawala milele na kufuta kabisa kwa kila namna yoyotw ukosoaji wa serikali yake na upinzani.
Anachotaka ni kubadilisha katiba na wabunge wa CCM hawtakuwa na kipingamizi bali kusema ndio. Hapo ndio itakuwa mwisho wa Tanzania.Raisi magufuli pia anatafuta matukio kwa hali yoyote kwa kutunga au uwongo kujaribu kuwa relative na kuonyesha anapendwa.

Nilichokiandika hapa ni mawazo yangu mwenywe na maon yangu.
 
aisee ww uliandika muda mrefu uliopita lakn ukisoma sahiz ni kama umeandika jana. hongera sana. kiujumla tushapotea mazima
 
Mkuu mbele ni giza giza giza. Hakuna nuru kabisa.
 
Kuna thread humu inaelezea ahadi za Magufuli nenda kaisome....

Halafu kuna Ilani ya CCM nenda kaisome pia.

Halafu rudi hapa uje kutuuliza ambacho hujakielewa..
Ahadi ahadi ahadi. Zitatekelezwa lini?
 
Anachokitaka hakieleweki katika nyanja hizi:-
  • Uchumi.
  • Siasa.
  • Jamii (ustawi na utangamano wake).
Kiuchumi. Taifa liko ktk mserereko hasi (deceleration) awamu hii. Ni muda muafaka wa kumkatalia na kumkataza anakotupeleka.

Kwenye siasa. Tunachagua kiongozi kusimamia tulichokubaliana kifanyike (katiba) na siyo kutuamlia nini kifanyike. Tusikubali kugawanywa na kujengeana chuki.

Kijamii. Asibadilishe mila na desturi za watanzania bali avisimamie.
 
Kiuchumi anataka yeye ndio awe tajiri mkuu nchini ili akitoa msaada wa milioni kumi aonekane mungu.
Kijamii anataka kutugawa ili atutawale vizuri - divide and rule
Kisiasa hataki habari ya kupingana kwa hoja iwe ndani au nje ya ccm, ni 'ndiyo mzee'
 
Ni rahisi zaidi kuwatawala masikini na wajinga, "kutawala" ndio kipaombele chake
 
Ukiwa hujifunzi na kutangamana na wenzio hata vitu vya kawaida unaweza kufikiri ni vipya sana kwako..wini wini situesheni ni ya kawaida sana kwenye maisha ya kila siku !
 
Sio "win win" ni wiini wiini. Siku nyingine umsikilize vizuri
 
Huyu mtu ni simply mshamba,kule Uganda kina Kenyatta walikuwa wanamcheka kwa kebehi kwa kila utumbo alokuwa anamwaga
 
Huwa na mawazo mkurupuko ambayo anashindwa kuyaweka kwenye mkakati sahihi.
Kifupi ni mwenye ndoto na matamanio isipokuwa anaamini yeye anajua kila kitu na haamini wasaidizi wake.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…