Mulhat Mpunga
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 27,256
- 16,317
haha kashakula kitu chenye ncha kali itakuwa sandarusi zinaelea kila siku bahari ya hindi ..........Angerudi atupie tena japo mstari mmoja
Ova
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
haha kashakula kitu chenye ncha kali itakuwa sandarusi zinaelea kila siku bahari ya hindi ..........Angerudi atupie tena japo mstari mmoja
Ova
Hahahaha safari ni moto!!!moto!! Unaelekea chatokama hujui unapokwenda... basi huwezi kupotea.
Ina maana tangu Mei, 2016...watu mlijua huyu JPM hana dira..Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Hatuwezi kuwa na Rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.
Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli, hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya Rais au Waziri Mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.
Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.
Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu.
Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je, anajua jinsi ya kututoa?! Anajua anakotupeleka?
Nimejitahidi kuangalia Bunge ili nione labda Mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.
Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Siyo kila mtu ukumbini amepevuka kama wewe.Kuna thread humu inaelezea ahadi za Magufuli nenda kaisome....
Halafu kuna Ilani ya CCM nenda kaisome pia.
Halafu rudi hapa uje kutuuliza ambacho hujakielewa..
Ndugu unasema gharama za maisha zimepanda. Mkuu wa kaya hana habari. Angekuwa na habari asingekuwa anarusha mamilioni kila akipita vijijini. Yeye anazo.Waheshimiwa hebu nijuzeni kidogo,hivi huyu captain wetu wa nchi ndiye yule yule wa kipindi cha uchaguzi au kuna lijamaa limevaa ngozi ya captain?
Nakumbukuka kipindi cha kinyang'anyilo nilikuwa mkoani Mbeya,captain alipokuwa akiomba kura wananchi walikuwa wakipiga kelele za 'PEOPLE'S POWER', nilipomtazama kwa hakika niliona huruma,niliona jinsi watu walivyokuwa wakihitaji mabadiliko ya dhati na hawakuhitaji kijani kibichi kushika uskani tena. Alitia huruma,alikuwa innocent mpaka nikawaza ningekuwa na uwezo ningechapa viboko hawa wananchi.
Nakumbuka statement yake baada ya kuona upepo ukanda ule ni mgumu ikabidi nae aitikie 'PEOPLE'S POWER ila akamalizia kwa kuomba naombeni hiyo power nipeni mimi nikawaletee mabdiliko,mchuma ukawashwa wakasepa.
Jamani mimi kwa kweli sielewi,nini kinaendelea Captain wetu ni yule yule au nini kimetokea,au mimi sielewi. Sio siri nikiwaza huwa ninaumia sana.
Au anahujumiwa? Pengine ameingilia maslahi ya watu kwa uadilifu wake sasa anafanyiwa kuchafuliwa? Wateule wake wanampka mafuta kwa mgongo wa chupa? It doesn't make sense kabisa Captain ku act as if nothing wrong is happening. Captain aseme neno basi roho yangu iliridhike.
Mbona ni rahisi sana kuishika mioyo ya watu,mbele wanasema winning people's hearts. Sio siri huku mtaani ni kama captain anakuwa disqualified siku baada ya siku. Aseeme neno basi tujue ni yeye au hata yeye haelewi nini kinaendelea. Kama kuna mikono michafu ya mataifa uliyoingilia maslahi yao atuambie.
It doesn't make sense and no logic hata kidogo kutupuuza wananchi wako. Ajira hujatupa sawa tutajiari,umepunguza wafanyakazi sawa, sasa hivi waalimu wa sekondari wanarudisha shule za msingi,je hii kwako ina make sense?. Wafanyakazi ni manung'uniko tu, Mishahara ndo hivo,gharama za maisha baba zimepanda,au wateule wako hawakujuzi?
Sio siri mambo huku yako hovyo hovyo kabisa. Asiwasikilize hao watu wake wa karibu huko ambao tukilalamika wanamwambia eti tulikuwa wapiga dili eti mambo ni shwari.
Hao washauri wake vipi hawamwambii vipaumbele vya wananchi,wananchi wanataka nini,mbona kama anayoyafanya yeye ni ya kwake,mfano uwanja wa ndege chato,ni mshauri gani alimwbia apeleke uwanja wa ndege kule.?
Mimi binafsi naelewa kuwa ushindi wake aliutafuta kwa nguvu,alitumia ushawishi wa kiwango cha juu sana maana ushindani ulikuwa mkubwa,lakini je ndio ameamua kuutokomeza upinzani? Nani alimwambia upinzani unamalizwa kwa bunduki,kufungwa jera,kuporana mali na kutishana,nimwambie wananchi hawataki kaki wala kijani wanataka ile kweli,uongozi wa kweli,uadilifu,uwazi,haki na demokrasia. Yeye afanye hivo aone kama kuna mtanzania atakumbuka kama kuna makamanda,upinzani utajifia wenyewe hana haja ya kukimbizana na upinzani. Je anawatuma polisi,mahakama,tume wavunje sheria na katiba au wanamzunguka aonekane mbaya.?
Watu hubadilika lakini kama ni yeye captain basi mabadilko yake yamekuwa ya kasi sana.
Mwenye uelewa juu ya haya mabdiliko ya captain anijuze tafadhari.
Shukrani.
Na kisha kuwa operation nunua wabunge na madiwani wa upinzani pamoja na kuteka na kuua raia wasio na hatia.Kutoka vita dhidi ya Ufisadi hadi Operesheni Safisha Mafisadi.