Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Anayo dhamila ya dhati kuiondoa nchi mahali ilipokwama lakini tatizo amekosa ushirikiano labda njia inayotumika siyo rafiki.lkn kwa nchi hii ilipokuwa imefikia ilikuwa hakuna namna lazima ubabe utumike.
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Hatuwezi kuwa na Rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli, hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya Rais au Waziri Mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu.

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je, anajua jinsi ya kututoa?! Anajua anakotupeleka?

Nimejitahidi kuangalia Bunge ili nione labda Mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Ina maana tangu Mei, 2016...watu mlijua huyu JPM hana dira..

Yani leo ni dhahiri jamaa yupo yupo tu.

Siku airtel yetu ikirudishwa na kuwa TTCL ndo ntamwamini JPM..
 
Waheshimiwa hebu nijuzeni kidogo,hivi huyu captain wetu wa nchi ndiye yule yule wa kipindi cha uchaguzi au kuna lijamaa limevaa ngozi ya captain?

Nakumbukuka kipindi cha kinyang'anyilo nilikuwa mkoani Mbeya,captain alipokuwa akiomba kura wananchi walikuwa wakipiga kelele za 'PEOPLE'S POWER', nilipomtazama kwa hakika niliona huruma,niliona jinsi watu walivyokuwa wakihitaji mabadiliko ya dhati na hawakuhitaji kijani kibichi kushika uskani tena. Alitia huruma,alikuwa innocent mpaka nikawaza ningekuwa na uwezo ningechapa viboko hawa wananchi.

Nakumbuka statement yake baada ya kuona upepo ukanda ule ni mgumu ikabidi nae aitikie 'PEOPLE'S POWER ila akamalizia kwa kuomba naombeni hiyo power nipeni mimi nikawaletee mabdiliko,mchuma ukawashwa wakasepa.

Jamani mimi kwa kweli sielewi,nini kinaendelea Captain wetu ni yule yule au nini kimetokea,au mimi sielewi. Sio siri nikiwaza huwa ninaumia sana.

Au anahujumiwa? Pengine ameingilia maslahi ya watu kwa uadilifu wake sasa anafanyiwa kuchafuliwa? Wateule wake wanampka mafuta kwa mgongo wa chupa? It doesn't make sense kabisa Captain ku act as if nothing wrong is happening. Captain aseme neno basi roho yangu iliridhike.

Mbona ni rahisi sana kuishika mioyo ya watu,mbele wanasema winning people's hearts. Sio siri huku mtaani ni kama captain anakuwa disqualified siku baada ya siku. Aseeme neno basi tujue ni yeye au hata yeye haelewi nini kinaendelea. Kama kuna mikono michafu ya mataifa uliyoingilia maslahi yao atuambie.

It doesn't make sense and no logic hata kidogo kutupuuza wananchi wako. Ajira hujatupa sawa tutajiari,umepunguza wafanyakazi sawa, sasa hivi waalimu wa sekondari wanarudisha shule za msingi,je hii kwako ina make sense?. Wafanyakazi ni manung'uniko tu, Mishahara ndo hivo,gharama za maisha baba zimepanda,au wateule wako hawakujuzi?

Sio siri mambo huku yako hovyo hovyo kabisa. Asiwasikilize hao watu wake wa karibu huko ambao tukilalamika wanamwambia eti tulikuwa wapiga dili eti mambo ni shwari.

Hao washauri wake vipi hawamwambii vipaumbele vya wananchi,wananchi wanataka nini,mbona kama anayoyafanya yeye ni ya kwake,mfano uwanja wa ndege chato,ni mshauri gani alimwbia apeleke uwanja wa ndege kule.?

Mimi binafsi naelewa kuwa ushindi wake aliutafuta kwa nguvu,alitumia ushawishi wa kiwango cha juu sana maana ushindani ulikuwa mkubwa,lakini je ndio ameamua kuutokomeza upinzani? Nani alimwambia upinzani unamalizwa kwa bunduki,kufungwa jera,kuporana mali na kutishana,nimwambie wananchi hawataki kaki wala kijani wanataka ile kweli,uongozi wa kweli,uadilifu,uwazi,haki na demokrasia. Yeye afanye hivo aone kama kuna mtanzania atakumbuka kama kuna makamanda,upinzani utajifia wenyewe hana haja ya kukimbizana na upinzani. Je anawatuma polisi,mahakama,tume wavunje sheria na katiba au wanamzunguka aonekane mbaya.?

Watu hubadilika lakini kama ni yeye captain basi mabadilko yake yamekuwa ya kasi sana.

Mwenye uelewa juu ya haya mabdiliko ya captain anijuze tafadhari.

Shukrani.
 
Kuna baadhi ya wana CCM wanadhani haya yanayotokea kuwa yatapita bure na kwamba hayaweki athari yoyote.

Nchi ina malalamiko kila kona, CCM wanadharau kwa sabababu wao ndio walalamikiwa, watawala na wenye dhamana.

Mauaji yanayoendelea na watu kupotezwa na viongozi kuwa kimya hii ni hatari.

maonevu na kupindisha sheria zilizokubaliwa kwa wapinzani na wale wanaokosoa serikali kamwe hakutaiacha nchi salama.

Haki za binadamu na haki za kikatiba kuminywa ikiwemo uhuru wa kujieleza na kupata habari unaminywa kwa makusudi na kila anayepaza sauti kukosowa anaitwa mchochezi.

TAHADHARI.
Wakati haya yanafanyika mchana kweupe CCM iko kimya , wastaafu wako kimya, mahakama iko kimya, Bunge liko kimya, viongozi wa dini wako kimya. Tunawaona wana siasa wa vyama vya upinzani wakipaza sauti wameachiwa jukumu peke yao, wananyanyaswa.

Baadhi ya taasisisi na vyombo vya habari zinajaribu kupaza sauti, zinazuiwa na kupigwa faini.

Nani sasa aseme au TUNASUBIRI MPAKA NCHI IIINGIE MTAFARUKU NDIO TUANZE KUFANYA UNAFIKI ?

Mimi natoa tahadhari kuwa MUNGU HADHIHAKIWI. Wanaofanya haya ni viongozi na watawala wa CCM kwa vyovyote vile CCM inahusika.

Kitakachokuja tokea CCM kama chama Tawala kitahusika nacho, wakati ni sasa. Hali ya nchi yetu ni mbaya.

Viongozi wanapalilia uovu kwa mikono yao wasije kupiga kelele ooh . Mungu kasababisha' Shit Mungu asisingiziwe.

Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania.
 
Kuna thread humu inaelezea ahadi za Magufuli nenda kaisome....

Halafu kuna Ilani ya CCM nenda kaisome pia.

Halafu rudi hapa uje kutuuliza ambacho hujakielewa..
Siyo kila mtu ukumbini amepevuka kama wewe.
 
Waheshimiwa hebu nijuzeni kidogo,hivi huyu captain wetu wa nchi ndiye yule yule wa kipindi cha uchaguzi au kuna lijamaa limevaa ngozi ya captain?

Nakumbukuka kipindi cha kinyang'anyilo nilikuwa mkoani Mbeya,captain alipokuwa akiomba kura wananchi walikuwa wakipiga kelele za 'PEOPLE'S POWER', nilipomtazama kwa hakika niliona huruma,niliona jinsi watu walivyokuwa wakihitaji mabadiliko ya dhati na hawakuhitaji kijani kibichi kushika uskani tena. Alitia huruma,alikuwa innocent mpaka nikawaza ningekuwa na uwezo ningechapa viboko hawa wananchi.

Nakumbuka statement yake baada ya kuona upepo ukanda ule ni mgumu ikabidi nae aitikie 'PEOPLE'S POWER ila akamalizia kwa kuomba naombeni hiyo power nipeni mimi nikawaletee mabdiliko,mchuma ukawashwa wakasepa.

Jamani mimi kwa kweli sielewi,nini kinaendelea Captain wetu ni yule yule au nini kimetokea,au mimi sielewi. Sio siri nikiwaza huwa ninaumia sana.

Au anahujumiwa? Pengine ameingilia maslahi ya watu kwa uadilifu wake sasa anafanyiwa kuchafuliwa? Wateule wake wanampka mafuta kwa mgongo wa chupa? It doesn't make sense kabisa Captain ku act as if nothing wrong is happening. Captain aseme neno basi roho yangu iliridhike.

Mbona ni rahisi sana kuishika mioyo ya watu,mbele wanasema winning people's hearts. Sio siri huku mtaani ni kama captain anakuwa disqualified siku baada ya siku. Aseeme neno basi tujue ni yeye au hata yeye haelewi nini kinaendelea. Kama kuna mikono michafu ya mataifa uliyoingilia maslahi yao atuambie.

It doesn't make sense and no logic hata kidogo kutupuuza wananchi wako. Ajira hujatupa sawa tutajiari,umepunguza wafanyakazi sawa, sasa hivi waalimu wa sekondari wanarudisha shule za msingi,je hii kwako ina make sense?. Wafanyakazi ni manung'uniko tu, Mishahara ndo hivo,gharama za maisha baba zimepanda,au wateule wako hawakujuzi?

Sio siri mambo huku yako hovyo hovyo kabisa. Asiwasikilize hao watu wake wa karibu huko ambao tukilalamika wanamwambia eti tulikuwa wapiga dili eti mambo ni shwari.

Hao washauri wake vipi hawamwambii vipaumbele vya wananchi,wananchi wanataka nini,mbona kama anayoyafanya yeye ni ya kwake,mfano uwanja wa ndege chato,ni mshauri gani alimwbia apeleke uwanja wa ndege kule.?

Mimi binafsi naelewa kuwa ushindi wake aliutafuta kwa nguvu,alitumia ushawishi wa kiwango cha juu sana maana ushindani ulikuwa mkubwa,lakini je ndio ameamua kuutokomeza upinzani? Nani alimwambia upinzani unamalizwa kwa bunduki,kufungwa jera,kuporana mali na kutishana,nimwambie wananchi hawataki kaki wala kijani wanataka ile kweli,uongozi wa kweli,uadilifu,uwazi,haki na demokrasia. Yeye afanye hivo aone kama kuna mtanzania atakumbuka kama kuna makamanda,upinzani utajifia wenyewe hana haja ya kukimbizana na upinzani. Je anawatuma polisi,mahakama,tume wavunje sheria na katiba au wanamzunguka aonekane mbaya.?

Watu hubadilika lakini kama ni yeye captain basi mabadilko yake yamekuwa ya kasi sana.

Mwenye uelewa juu ya haya mabdiliko ya captain anijuze tafadhari.

Shukrani.
Ndugu unasema gharama za maisha zimepanda. Mkuu wa kaya hana habari. Angekuwa na habari asingekuwa anarusha mamilioni kila akipita vijijini. Yeye anazo.
 
Tuendelee kukumbushana hii nchi ni yetu sote. katiba lazima iheshimiwe na kila mtu bila kujali cheo wala kabila. Uvunjaji katiba hauwezi kutuacha salama. CCM badilikeni
 
Mabadiliko yoyoye yana hatua 3 yaani: 1.Mwanzo wa mabadiliko
2.wakati wa mabadiliko na Mwisho wa mabadiliko.Kwa kila hatua kuna changamoto zake kwa mfano mwanzo wa mabadiliko hapo ndo kunatokea migongano,misuguano,malalamiko.Kipindi hiki ni kifupi na karibu tunakivuka.Kwa hiyo niwatake uvumilivu na matunda tutayaona mwisho baada ya kuyapokea,kuyaelewa na kuyafanyia kazi mabadiliko.
 
Naam wakubwa...
Kwa akili Timamu kabisa nimejitokeza juu la jukwaa hili kuupongeza utawala wa serikali ya awamu ya tano kwa kufanya yafuatayo.....
1. Kuondo na kuminya mianya ya rushwa
2. Kukabiliana na tatizo la madawa ya kulevya...
3.suala la watumishi hewa
4. Kushughulikia tatizo na migogoro. Ya ardhi
5.elimu bure
6.kutoa mikopo kwa wakati vyuoni
7.kupambana na wakwepaji kodi

Wapi imeingia mkenge.....
1. Kuminya uhuru wa kujieleza
2.kukandamiza vyama vingine vya siasa
3. Kuminya uhuru wa mahakama
4.kuzorotesha mahusiano ya kimataifa kwa makusudi
Maoni
Isikilize sauti ya watu maana serikali iliapa kutetea watu na watu wanaona wanakoenda siko, basi serikali Isikilize watu....
Pleas me mtanzania wa kawaida nisitafutwe..
 
barbosa cjawah kuona umeandika cha maana. zaid unadili na majina ya watu tuu. kila post we ni lowasa na mbowe.
 
Nakumbuka wakati Raisi Magufuli anaingia madarakani alikua anakubalika sana nje na ndani ya Nchi hasa kwa zile mbwembwe zake za kutumbua na ziara za kushtukiza

Wananchi wakawa na imani nae,nakumbuka wakati ule wananchi waliku hawakosi kuangalia News ifikapo SAA 2 hasa ITV watu walijazana kwenye mabar kuangalia habari za magufuli

Aliandikwa vizuri na vyombo mbalimbali vya kimataifa akaitwa 'Bulldozer' jembe mtetezi wa wanyonge

Ghafla bwana yule akabadilika uhuru wa kutoa maoni kwa wananchi ukaminywa

Akafukuza watumishi wa umma

Akashindwa kuajiri vijana katika kada mbalimbali

Akaharibu uchumi wa Nchi hadi sasa unapumulia mashine

Watu wakaanza kutekwa na kuuliwa

Kesi zisizo na kichwa wala miguu zikaibuka dhidi ya wapinzani

Bulldozer kageuka Dictator Nchi imemshinda hii,cha muhimu asituharibie Nchi yetu aachie tu uongozi sio lazima kutuongoza

Tukutane 26/4/2018 Jah Bless[emoji377] [emoji377] [emoji380] [emoji380] [emoji379] [emoji379] [emoji379] [emoji379]
 
Tena Akwende kabisa,Urais sio segere atasema tuamke tucheze.
Ameshindwa Asubuhi kabisa.Mto Kagera kuna Mamba nasubiria akatupwe huko.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom