Kwa mwenye akili timamu na anayeipenda nchi ya Tanzania anajua kwamba tumepelekwa shimoni ndani ya miaka 2 tu
*social life imeharibika kabisa,police wametiwa kiburi cha ajabu,leo hata kumiliki gari ni dhambi
*Kiuchumi,hali halisi inajulikana jamani haina haja ya kuongea
*Kisiasa,ndo kabisaaaaaaaa,leo wanasema maendeleo hayana vyama,kesho wanahonga watu hela waachie vyeo ili chaguzi zirudiwe
Kabla sijaendelea mbele naomba nikazie suala hilo la siasa, wanaodhani kufa kwa chadema au madiwani kuhama ndiyo mwisho wa upinzani wakapimwe akili zao.
Nyerere alinusurika kupinduliwa mara mbili na watu ambao hawakuridhika na utawala wake, hakukuwa na vyama vya upinzani ila kuna watu walikuwa na upinzani mioyoni mwao
Mtaua vyama, mtaua na kufunga wapinzani mwisho wa siku mtatengeneza waasi wasio hata na kiongozi wa kuwaambia acheni,ndo haya ya tarehe 26/04, hamjui hata mna deal na nani.
Tena hawa kina mbowe bora mngewachukulia kama marafiki badala ya maadui, kuna kundi kubwa linaloichukia ccm, limekuwepo kabla ya Mbowe na litakuwepo baada yake, hata mkigawa 10,000 kila siku kwa raia na maziwa kwa kila mtu bado kuna watu watawakataa so LEARN TO LIVE WITH IT, NDIYO MAISHA HAYO, MBONA HATA YESU NA MTUME MUHAMED KUNA WATU WALIWAPINGA, WEWE NI NANI USIYETAKA KUPINGWA?
Miaka 3 iliyopita upinzani wa ccm na cdm ulikuwa kama simba na yanga,utani wa jadi sikudhani kuna siku mtu mmoja angetufikisha kwenye hali ya chuki kama ile ya kule visiwani ya cuf na ccm, leo chadema hata kuzika hawaruhusiwi?? vikao kwenye misiba, kuna misiba isiyo na mikusanyiko ndani yake na vikao vidogovidogo? unataka wakae kama kanisani?
Utawala huu umeharibu sana ndani ya miaka 2 beyond repair,ukiona mtu ambaye anadhani kujenga madaraja na reli ndiyo furaha ya watu basi yupo out of touch kabisa,nadhani yeye ndiye angekuwa kafanikisha ile miundombinu ya Ethiopia sijui ingekuwaje????
maisha ni zaidi ya hayo ndugu yetu,open your eyes,UMEHARIBU SANA NDANI YA MIAKA 2 TU,HATUNA LA KUFANYA TUSUBIRI 2025 TUANZE UPYA KUSHONA VIRAKA NA KU REPAIR MAKOVU ULIYOYAACHA NA HAPO TUOMBE MUNGU HAYA MACHUKI UNAYOCHOCHEA YASIFIKE PABAYA
Nasema 2025 kwa sababu hiyo trailer tuliyoona kwenye chafuzi ndogo za madiwani na ule wa kinondoni ni kwamba 2020 utashinda kwa asilimia 98 kwa msaaada mkubwa wa policcm
So sad,umetuharibia, umeharibuuu mnoooooo.