Mheshimiwa Rais,
Pole kwa Majukumu!.....natumai ujumbe wangu huu utakufikia hapo "Jumba Jeupe" japo unaweza kuonekana ni ujumbe usio na maana na wa hovyo but kikubwa ufike sehemu husika.
Mh. RAIS, Nimejaribu kutafakari mambo mengi yahusuyo hatma ya taifa letu tangu ulipoingia madarakani, naona umeshapoteza dira na lengo lako uliloingia nalo madarakani.....
Mh. Rais, bila kupepesa macho wala mikono nathubutu kusema ya kwamba wewe ndiye Rais unayeweka historia ya "Rais kimeo kuwahi kutokea tangu tupate Uhuru" huna dira, huna lengo thabiti, huna maono, huna Utu, nakiri kuwa cheo cha urais kimepata m'bakaji (Nisamehe kwa lugha yangu kali).
Mh. Rais, wewe ndiye Kiongozi pekee uliyeleta balaa, malalamiko, shida, manyanyaso na mgawanyiko mkubwa katika taifa (umekuwa adui mkubwa wa demokrasia na mshikamano kitaifa, umekuwa Nepotist na selfish wa kiwango cha hali ya juu, Ukanda, Ukabila na hata Uchama! Inasikitisha!
Mh. Rais, tangu uingie madarakani, ajira hamna (vijana waliomaliza vyuo kuanzia ulipoingia madarakani yaani 2015+ wanakula msoto mtaani).....Hali ngumu ya maisha, nani aliyesalimika katika hili? Wewe ndiye rais pekee ambaye chini ya uongozi wake, upinzani unaonekana ni uadui, manyanyaso ya polisi na vyombo vya usalama kwa raia hakika umeweka pamba masikioni!!
Mh. Rais, huu ni mwaka wa tatu tangu uingie madarakani (soon utaingia wa nne), ila najua unajidanganya kwa kujivuni Elimu Bure (ilhali hakuna implementation na strong strategies), lakini pia utajivunia MaBombardier, SRG, Stiglers Gorge na Uwanja wa ndege wa Chato!...ila nakuhakikishia utaondoka madarakani ukiwa na deni kubwa kutoka kwenye mioyo ya Watanzania wengi walioteseka na uongozi wako dharimu.
Nani anayetaka Stiglers Gorge na Mandege wakati hapewi nafasi yake kikatiba kama mwananchi mwenye imani, itikadi, na maono huru? Hakika mtu uyo hayupo, na kama yupo hawezi kuwa si punguani wa akili!!
Mh. Rais, nikukumbushe tu ya kwamba hao wakuhadaao kwa kisingizio cha kukuunga mkono, ndio haohao watakao pelekea anguko lako....
Nimalizie kwa kukupa ujumbe huu "THE NUMBER OF FOLLOWERS YOU HAVE, DOES NOT MAKE YOU A BETTER PERSON THAN ANYONE ELSE,..REMEMBER, ADOLF HITLER HAD MILLIONS, JESUS HAD ONLY TWELVE".......
__nakungoja mlangoni____