Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Sidhani kama kuna kitu kingine kinachoendelea zaidi ya rushwa kufanikisha haya na hii rushwa atakuwa anaifanya kwenye kila manunuzi au mikataba anayoisimamia sasa na haya yatakuja kujulikana siku zijazo.

Nashukuru hata Mhe.mmoja katika mtandao wa twitter leo ameeleza kinachofanyika sasa ili kuwashawishi waheshimiwa walioko katika jimbo lake nao waasi kama wenzao katika maeneo mengine.

Tujiulize anafanya mangapi ya aina hii kwa manufaa yake binafsi kwa kutumia nafasi aliyonayo?

Huyu mtu ni hatari sana na ni wazi hana maadili kabisa.
 
Kinacho niuma kuona kod zetu zikitumika ovyo ovyo

Yan izo pesa kwa jinsi zinavyo tumika kwa hakika tungewekeza katika mambo ya msingi ah ah ah my friend tungefika mbali sana

Sijui baadhi ya wasomi wetu huwa wanafikili kwa kutumia matako badala ya kichwa
 
tutaiamini kama ni rushwa pale mtakapo tuonyesha live, eidha mtuonyeshe aliyeingiziwa hela kwenye acc yake na ikasoma hizo hela mnazodai wamenunuliwa, au mtuonyeshe mtu akikabidhiwa bulungutu la minoti live tofauti na hpo twende na kauli moja, " usimwamini mwanasiasa yyte yule".
 
Mna ushahidi wa hizo rushwa? Mmeziba masikio hamtaki kusikia matatizo yaliyomo kwenye vyama vyenu, na watazidi kuondoka. People are not stupid anymore. Watu wanataka maendeleo na siyo porojo za kushawishi watu kususia serikali eti kisa ni mpinzani.
 
Paint the bigger picture wabunge 95% CCM plus madiwani wote CCM, change katiba come 2025 nini kitatokea........Mungu ni mjuzi zaidi
 
tutaiamini kama ni rushwa pale mtakapo tuonyesha live, eidha mtuonyeshe aliyeingiziwa hela kwenye acc yake na ikasoma hizo hela mnazodai wamenunuliwa, au mtuonyeshe mtu akikabidhiwa bulungutu la minoti live tofauti na hpo twende na kauli moja, " usimwamini mwanasiasa yyte yule".
Hivi kwa akili yako MTU hasa mwafrika kweli anaweza acha mshahara wake,marupurupu,posho za vikao,kuinua mgongo na kwenda kuunga mkono bure bure bila ahadi yeyote si umeona ya siha na kinondoni, maana fursa ngekewa,chakula kimekuja mbele mlangoni mwako nawe una njaa. Wenye aibu wakitazama waliopata ulemavu kwa ajili yao na matatizo mengine uingiwa na utu usita,wafia tumbo hawana haya wao tumbo kwanza,mengine baadae.
 
mkuu cjakataa, hawa watu wooote hata ile ushahidi wa acc zao kutuna au hata mabulungutu tuyashuhudie, vyama vya upinzani vina intelijensia yao pana sana, imeshindwa hadi sasa kuja na ushahidi wa nunuzi hata moja?
 
Hivi kwa akili yako MTU hasa mwafrika kweli anaweza acha mshahara wake,marupurupu,posho za vikao,kuinua mgongo na kwenda kuunga mkono bure bure bila ahadi yeyote si umeona ya siha na kinondoni, maana fursa ngekewa,chakula kimekuja mbele mlangoni mwako nawe una njaa. Wenye aibu wakitazama waliopata ulemavu kwa ajili yao na matatizo mengine uingiwa na utu usita,wafia tumbo hawana haya wao tumbo kwanza,mengine baadae.
Nyalandu baada ya kuhama amepewa nini?
 
Sidhani kama kuna kitu kingine kinachoendelea zaidi ya rushwa kufanikisha haya na hii rushwa atakuwa anaifanya kwenye kila manunuzi au mikataba anayoisimamia sasa na haya yatakuja kujulikana siku zijazo.

Nashukuru hata Mhe.mmoja katika mtandao wa twitter leo ameeleza kinachofanyika sasa ili kuwashawishi waheshimiwa walioko katika jimbo lake nao waasi kama wenzao katika maeneo mengine.

Tujiulize anafanya mangapi ya aina hii kwa manufaa yake binafsi kwa kutumia nafasi aliyonayo?

Huyu mtu ni hatari sana na ni wazi hana maadili kabisa.
Mrundi huyo yeye anachojuwa ni rushwa
 
Mkuu nadhani sasa uelekeo unauona anakotupeleka.Kama ushawahi kufika mlima kitonga basi kule kwenye lile korongo/poromoko refu ndio destination yetu kwa awamu hii.
 
Mheshimiwa Rais,

Pole kwa Majukumu!.....natumai ujumbe wangu huu utakufikia hapo "Jumba Jeupe" japo unaweza kuonekana ni ujumbe usio na maana na wa hovyo but kikubwa ufike sehemu husika.

Mh. RAIS, Nimejaribu kutafakari mambo mengi yahusuyo hatma ya taifa letu tangu ulipoingia madarakani, naona umeshapoteza dira na lengo lako uliloingia nalo madarakani.....

Mh. Rais, bila kupepesa macho wala mikono nathubutu kusema ya kwamba wewe ndiye Rais unayeweka historia ya "Rais kimeo kuwahi kutokea tangu tupate Uhuru" huna dira, huna lengo thabiti, huna maono, huna Utu, nakiri kuwa cheo cha urais kimepata m'bakaji (Nisamehe kwa lugha yangu kali).

Mh. Rais, wewe ndiye Kiongozi pekee uliyeleta balaa, malalamiko, shida, manyanyaso na mgawanyiko mkubwa katika taifa (umekuwa adui mkubwa wa demokrasia na mshikamano kitaifa, umekuwa Nepotist na selfish wa kiwango cha hali ya juu, Ukanda, Ukabila na hata Uchama! Inasikitisha!

Mh. Rais, tangu uingie madarakani, ajira hamna (vijana waliomaliza vyuo kuanzia ulipoingia madarakani yaani 2015+ wanakula msoto mtaani).....Hali ngumu ya maisha, nani aliyesalimika katika hili? Wewe ndiye rais pekee ambaye chini ya uongozi wake, upinzani unaonekana ni uadui, manyanyaso ya polisi na vyombo vya usalama kwa raia hakika umeweka pamba masikioni!!

Mh. Rais, huu ni mwaka wa tatu tangu uingie madarakani (soon utaingia wa nne), ila najua unajidanganya kwa kujivuni Elimu Bure (ilhali hakuna implementation na strong strategies), lakini pia utajivunia MaBombardier, SRG, Stiglers Gorge na Uwanja wa ndege wa Chato!...ila nakuhakikishia utaondoka madarakani ukiwa na deni kubwa kutoka kwenye mioyo ya Watanzania wengi walioteseka na uongozi wako dharimu.

Nani anayetaka Stiglers Gorge na Mandege wakati hapewi nafasi yake kikatiba kama mwananchi mwenye imani, itikadi, na maono huru? Hakika mtu uyo hayupo, na kama yupo hawezi kuwa si punguani wa akili!!

Mh. Rais, nikukumbushe tu ya kwamba hao wakuhadaao kwa kisingizio cha kukuunga mkono, ndio haohao watakao pelekea anguko lako....

Nimalizie kwa kukupa ujumbe huu "THE NUMBER OF FOLLOWERS YOU HAVE, DOES NOT MAKE YOU A BETTER PERSON THAN ANYONE ELSE,..REMEMBER, ADOLF HITLER HAD MILLIONS, JESUS HAD ONLY TWELVE".......

__nakungoja mlangoni____
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom