Tunasikitishwa mno na Uongozi wa Rais Magufuli kwa kitendo chake cha kuiongoza Nchi kupitia Mkono wa Chuma (Umwagaji Damu). Kwa muda mfupi wa miaka mitatu ya Uongozi wa Rais huyu, tumeshuhudia wa- Tanzania wengi wakifariki kupitia Vifo vya kutatanisha na visivyo na maelezo yakutosha na wa Tanzania wengine wakitekwa, kuteswa na ama kuachiwa au kuuawa/ kupotea kabisa!
Mfano:- Mwaka 2016 alitekwa Ben Saanane. Hajaonekana. Mwaka 2017 alitekwa Mwenyekiti wa Halmashauri Kibondo Mr. Kanguye hajaonekana vile vile, alitekwa Mwana Habari Azory Gwanda hajaonekana. Mwaka huu 2018 ametekwa Mohammed Dewji, yaani wiki hii, jambo la kushangaza Vyombo vya Ulinzi na Usalama vinatuletea Hutuba ile ile tuliyokwisha izowea eti wako wanaendelea na kumtafuta na upelelezi unaendelea!
Tunaomba sana Rais na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Tanzania ingawa hawapendi basi wajilazimishe kututambua kuwa sisi ni Wa-Tanzania wenzao, watuheshimu, watujali, watudhamini, Watulinde na wasitudharau kwani nasi ni Binadamu wenzao tena wenye Akili timamu ya kutosha inayotuwezesha kung'amua mambo kama wafanyavyo wao. Wa-Tanzania tuna weledi mkubwa wa kuchanganua yaliyo MEMA na MABAYA. Viongozi wasitulee Hutuba zilizo jaa Vitisho vyenye lengo la kutuziba Mdomo tusijadili na kuongelea kitendo hiki cha utekaji Wananchi kilichoshamili Nchi/miongoni mwetu, wasituletee hutuba zilizojaa Propaganda, Dharau na Dhihaka kwa Wananchi, wakumbuke kwamba, tunajua namna ya kuchanganua Kauli, vitendo, Sura nk. ya Kiongozi anayetuhutubia kisha tukafahamu wazi kama jambo analotueleza ama lina ukweli au laa!
Yapo mambo mengi yanayotuaminisha kuwa Rais Magufuli na Watu wake ndiyo wanaotekeleza Opereshen hii ya Utekaji, utesaji na Uuwaji wa Wananchi wasiyo na hatia ndani ya Nchi kwa sababu za KIUCHUMI na KISIASA. Mfano-
Eneo ambalo Mo Dewji alikotekwa ni lenye Ulinzi Mkali zaidi Nchini, lina umbali wa kilomita chache kutokea Ikulu, ni jirani na Makao Makuu ya Usalama wa Taifa - TISS, jirani na Makazi ya Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais Zanzibar na Waziri Mkuu Mstaafu. Mtaa una CCTV za kutosha, lakini jambo la kushangaza, Vyombo vyetu vya usalama vinatulea maneno mepesi ya kutulaghai eti wanamtafuta MO kwa juhudi kubwa, nguvu na Akili zao zote, siyo kweli, hatuamini kabisa kwani Ufalme siku zote huwa haujipingi wenyewe! Ikiwa wameshindwa kumwokoa MO, huyu aliyetekwa maeneo salama ya Dar je, Mwananch ambaye anaweza kutekewa mkoani tena Wilaya ya mbali huko, wanaweza kumpata kwa muda gani, na ikiwa watampata atakuwa hai au ameshakufa!!?
Kuna utofauti Mkubwa kati ya kuwatafuta na kuwapata kwa WAKATI Watu waliopotea/waliotekwa hata kuwatia mbaloni Watekaji husika na kitendo kile cha kuwatafuta Watu hao kwa Muda mrefu usiyojulikana kikomo chake wala taarifa kutokutolewa kwa Wananchi. Mfano:- Mpaka sasa, hatuoni aliyekwisha tiwa mikononi mwa Police aliyempiga Risasi Mh. Lissu, aliyemtesa Dr. Olimboka, aliyempoteza Ben Saanane na wengine wengi!! Ni hutuba nyingi tu tunazopewa ambazo kimsingi ukizitafakari zaidi, utagundua Wana Usalama hawa, hawana nia ya kweli kulishughulikia jambo hili. Ni sababu zipi zinazowafanya wasilishughulikie jambo hili wakati tunajua kabisa pasipo mashaka, wana uwezo mkubwa wa kutokomeza vitendo vyote vyenye nia ya kuhatarisha Amani ya Nchi!?
Rais wetu Magufuli, tunamjua alivyo mwepesi kulisimamia/ kushughulikia jambo lolote linalogusa, kuwatesa na kuwahuzunisha Wananchi hususani maswala ya Kiuchumi, huwa hasiti kuwafukuza kazi Viongozi wazembe, ni mwepesi kuitisha Wanahabari Ikulu ili kuwahutubia Wananchi LIVE kuhusu maswala mbali mbali anayoyafanya kwa manufaa mapana ya maendeleo ya Wananchi lakini, pia kama kuna swala halimpendezi, huliongelea na kulichukulia hatua ya haraka zaidi. Je, kwa nini Rais haoni haja ya kutuhutubia juu ya Vitendo hivi haramu vinavyoshamiri Nchini vya Utekaji, Utesaji na uuwaji wa Wananchi wake!? Je, kwa nini haoni sababu ya kuwafukuza kazi Viongozi wakuu wenye dhamana ya kuilinda Amani ya Nchi hususani Wananchi na Mali zao!? Mbona Viongozi wa Wizara nyingine anaweza kuchukua hatua ya kuwatimua kazi kwa haraka lakini kwa hawa wa Vyombo vya Ulinzi vipi!?
Ukweli ni kwamba, kwa tofasili ya Viongozi wa Serikali, Nchi ina Amani tele lakini kwetu sisi WANANCHI WA TANZANIA, hatuioni hiyo Amani inayopigiwa chapuo! Kila kukicha Wa- Tanzania wanapotea katika mazingira ya kutatanisha, mmoja mmoja anadondoka, haijulikani kesho ni yupi atafuatia!! Tukiwaomba Serikali watuletea VYOMBO VYA KIMATAIFA WAJE KUTUONDOLEA MZIZI WA FITINA KATIKA KUCHUNGUZA NINI CHANZO NA NI WAKINA NANI WAKO NYUMA YA MPANGO NA UOVU HUU, Serikali inakataa! Rais Magufuli tumweleweje!?
Kimsingi, Wanasiasa hawana Pesa ya kuanzisha Viwanda vikubwa vyenye uwezo wa kuwaajiri wa- Tanzania zaidi ya 100, hata wakivianzisha huajiri watu wa Familia zao na ndugu na majaa wa karibu nao! Sasa Matajiri wa Nchi hii wenye Viwanda vikubwa vya kuajiri wa Tanzania zaidi ya watu 200, ndiyo hao Wanatekwa, wanateswa na kuuwawa! Maana yake ni kwamba hao walio ajiriwa watakosa kazi, na njaa kali itaingia kwenye Familia zao! Uzalishaji na mzunguko wa Pesa Nchini utakwisha siyo muda mrefu, watanzania wataandamwa na njaa kali.
Jambo kubwa la kusikitisha, wakati Utekaji wa Matajiri ukiendelea na kusababisha ukata wa Ajira Nchini, Serikali ya Magufuli haina Mpango wowote wa kuajiri. Vijana wako mtaani wakizurula na ukata wao pamoja na kuwa na Elimu na ujuzi mkubwa wa Mambo!
Hakika CCM, Viongozi wastaafu hususani Marais, mmetuletea Nchini balaa na laana kubwa kwa kitendo chenu cha kumteua Dr. Pombe Joseph Magufuli kuwa Rais wa Nchi yetu Tanzania, Nchi iliyokuwa ya Amani, watu wake wakiwa na Furaha tele, sasa Furaha na Amani Mioyoni mwao imetoweka ghafla katika kipindi hiki kifupi cha Utawala huu, huzuni na hofu imetanda kila kona ya Nchi. Mungu atusaidie, atuepushe hali hii. Amen!!