Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Bwana Membe vunja vunja Makufuli kisha mwaga Pombe yote inayo nywewa na ndege John
 
Shikamooo baba,

Ninaamini unalihisi joto japo kuwa huelewi linatokea wapi kutoka pale ulipo.
Joto hili linatokana na moshi,moshi unaofuka kutoka kwenye mto.
Mto huo ndiyo unaoutegemea ukupatie pumuziko nyakati zako hizi za mwisho kwenye maisha yako ya hapo nyumbani.

Nyumbani wameungana,wameshikamana na kukubaliana wauchome ili usilale wala kupumzika ili ukiweza kuishi uhame chumba na mtaa.

Nyumbani wanalalamika,wageni unawajali kuliko wanao,kwa faida ya nani?
Nyumbani umewatelekeza,hata ndani kwao umewazuia wasifanye chochote zaidi ya kuimba mapambio na ngoma za sifa.

Umeanza pia kuwapiga makofi ya machoni kisa tu wameimba taarabu na wengine kila kukicha unawatisha utawafukuza na bibi zao utawachapa bakora.

Mimi ni mwanao,nina marafiki,wamezama katika roho mpaka kule ambako kila mtu anapatamani afike,umechumbia wasio na vyeti,unawaacha wenye vyeti wasote mtaani kwao kwa kuwatenga mara ooh hawajasoma 'uchawi wa kizungu',roho inaniuma sana tena sana.

Hivi baba,wewe si ndiye ulisema ukishasafisha chumba chako ukawatoa buibui utaleta wasaidizi wapya,utapandisha neti chumbani kwetu? Imekuwaje?!

Miezi 36 inakatika,bado wewe unahangaika kutafuta mchawi,utaagua lini? Ugonjwa wako ni kuamini waganga wa kienyeji kuliko sisi uliotupeleka maabara za kileo,hatujui tukusaidie vipi?
Nyumba imechafuka,magodoro uliyoleta eti ni mapya....ha ha ha! Yana kunguni kibaaao.
Mzee wangu,zama zimebadilika,siyo kila homa ni maralia.

Kapime tu uhakikishe.Mto amechoma mjomba na ndugu zake akiwemo mama mdogo na yule mjomba mkubwa tena mkuuubwa kuliko wewe mara mia nne na themanini.

Kesho na keshokutwa hautalala maana hata nyumba wamekubaliana wauze baada ya kutalakiana na mama.

Lala baba,lala tu ......
 
Tumekusoma mzee. Hongera sana kwa kukitendea haki kiswahili japo huku mbele umeanika ulichokusudia
 
Ni vizuri kuelewa kuwa hata shetani alipata waungaji mkono wengi, lakini cha kushangaza huyo mtu aliyekujaza wewe uongo kuhusu shetani na makosa yake huyo mtu leo ukienda kwake ukimuuliza kama anamjua shetani, atakuuliza huyo mtu ni nani?

Umenielewa kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu nakuona bado hujapanuka mawazo, kwa maneno mengine, bado uko gizani. Naomba uelewe kitu kimoja kuwa huyo mtu aliyekudanganya kuhusu shetani hivi sasa vizazi vyake vinawaza jinsi ya kuiacha planet dunia na ku-immigrate kwenye sayari nyingine, wakati wewe na mimi bado tunalumbana kutafuta nani ana right kuliko mwenzake katika system ambayo mtu yule yule aliyekufundisha wewe kuhusu matendo ya shaetani, ametuachia.

Fumbua macho kwa ajili ya maisha yako na yetu katika nchi yetu. Usipende kuiga mambo ya watu wengine ambayo hayata tusaidia sisi kitu. Mara nyingi watu wanaokimbilia kuwaona wenzao au wengine ni wajinga au wapumbavu, kwa masikitiko yangu wao wenyewe hawajijui kiasi gani wako gizana na hawana akili kichwani. Wanashabikia tu wanasiasa ambao katika taifa letu hawana nafasi ya mtu kuwatambua tena kwa chochote kile ambacho wamekifanya.

Angalia sana usije ukajikuta huja ambulia kitu kwa kuendekeza ukaidi ambao hauna tija. Maisha hayakusubiri wewe, jaribu kwenda na wakati na usisubiri mpaka mtu aje kukukokota na kukuonyesha njia.

Fungua macho kijana wa leo na angalia fursa ambazo ziko nchini na tafuta maarifa ya kuzitumia fursa hizo. Usikae kuota ndoto za mchana za kufikiria kuwa mambo yatarudi tena kama enzi za zamani.

Wako wengi siku za nyuma walikaa na kulaumu maisha na mfumo ambao Mwalim Nyerere aliuleta, matokeo yake walisubiri mpaka mvi zikawaingia na hatimaye kwenda kaburini bila kuambulia matunda ya uhuru wao wa kweli ambao Tanzania kupitia Mwalim Nyerere ulishushwa kwao, wakitegemea waingereza wanarudi tena.

Jipange upya kijana. Umeshushwa duniani peke yako na utaiacha dunia peke yako, tena bila msindikizaji. Maisha ni mazuri sana na itakuwa busara kama utaifurahia.
 
Duh
 
Ndio ana roho mbaya, tena roho mbaya kweli kweli, na msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
Amewafanya watu wasiaminiane tena, watu wanakaa kwenye vikao lakini akili ziko nje, ya kwamba humu tutoke vipi.
Watu wanaingia kwenye vikao bila ajenda. Roho mbaya iliyotukuka. Kila mmoja kapoteza dira miongoni mwa timu.
Roho mbaya ya kuwanyima ajenda wenzio. Kila kona amekaba. Wapinzani hawana tena ajenda. Mzee anatoa majibu kuntu mpaka kwenye korosho, hakuna upenyo.

Ndege zimeshindikana kuwa ajenda.

Umeme umeshindwa kuwa ajenda.

Afya imegoma kuwa ajenda.

Miundombinu imegoma kuwa ajenda.

Michezo na wasanii mzee anacheza nao fair.

Kiufupi ni roho mbaya kuwanyima wenzio ajenda ya kusemea.

NB: Labda hapa penye nyongeza ya mishahara kwa watumishi ndio wanaweza kutokea. Ukiziba na hapa 2020 kampeni chapisha vipeperushi halafu acha UVCCM wavisambaze halafu wewe nenda likizo CHATO usubiri kuapishwa.
 
Anaroho mbaya ukiongea tu kuhusu ndege Pyupyu, ukiongea kuhusu Mo unaitwa polisi, ukifanya mkutano unasukwa ndani. Ukidai haki we ni adui wa taifa. Alisema "kununua korosho ni siku mbili tu" leo siku ya ngapi bado sijaona mjeda akibangua na meno,au itakuwa maonyesho ya sherehe za uhuru
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…