Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Tulimlilia Mungu atupe rais wa namna hii asiyeona haya,asiyefumba macho kwenye Mali ya umma,mkali kwa mafisadi ..Mungu akatusikia kilio chetu akatupa Magufuli.Mungu NI mkuu Sana
 
kwani kabla ya magufuli kuingia madarakani, mtoa maada ulikuwa unaelekeza wapi? direction yako ilikuwa ni nini?

na je EL angechukua nchi unajua plan yake ilikuwa wapi?

unaweza ukaelezea chadema ilipo kwa sasa ki direction ukiwa una refer context ile ile ya magufuli kwa taifa? ( rudia kusoma tena)
 
J Hatuwezi kupotea kwa sababu hatujui tunapoenda!
 
Mdanganye
 
..Duh!!

..wakabangue korosho kwa mdomo?

..kwanini anatoa matamshi kama hayo?

..ninavyoelewa mimi maganda ya korosho yanaunguza, sasa kuna kiongozi anafikiria kuamrisha wananchi wabangue korosho kwa midomo?

.

tindo, Nguruvi3, chige
 
Wengi kumbe lazima watumie unaakili zako timamu huwezi fanya huo upuuzi
 
..Duh!!

..wakabangue korosho kwa mdomo?

..kwanini anatoa matamshi kama hayo?

..ninavyoelewa mimi maganda ya korosho yanaunguza, sasa kuna kiongozi anafikiria kuamrisha wananchi wabangue korosho kwa midomo?

.

tindo, Nguruvi3, chige
Tena yanaunguza kweli kweli! And the question is: halafu vijana wetu wa JKT wakishaenda kubangua korosho kwa mdomo kisha wanazipeleka wapi!!!
 
Huko nyuma haikuwa rahisi kudhani kwamba Tanzania ingekuwa mojawapo wa nchi ambayo ingeingia katika nyanja za nchi zinazosemwa kuwa na ukiukwaji wa haki za binadamu. Haya mambo tulisikia yakisemwa juu ya nchi za wenzetu, lakini kwa nchi yetu lilikuwa jambo nadra sana.

Lakini sasa ni wazi kwamba chini ya utawala wa awamu ya tano, kadiri siku zinavyokwenda ndivyo hali ya Tanzania kusemwa na Watanzania wenyewe ndani ya nchi pamoja na mataifa mbali mbali, taasisi za kimataifa kutia ndani zinazotetea haki za wanadamu nk, kwamba ina kiuka misingi ya haki za binadamu na utawala wa sheria.

Ninachojiuliza, hivi Raisi Magufuli anadhani kwamba kelele zote hizi zinazopigwa juu ya ukosefu wa haki za binadamu na utawala wa kisheria nchini zinasemwa na watu wasio na akili ambao wameamua kuropoka bila kuona kwamba kweli Tanzania kuna tatizo? Ni ngoma ya aina gani Raisi Magufuli anataka apigiwe ili aelewe kwamba utawala wake una walakini katika suala la haki za binadamu na kwamba kuna haja ya kurekebisha kabla hali haijawa mbaya zaidi?

Au tuna tatizo la sikio la kufa kwa raisi wetu?
 
Nachukia udikteta wa hili jiwe

,hapendi kukosolewa

hapendi uhuru


hapendi upinzani


hapendi mawazo mbadala


hashauriki



wapinzani kwake ni maadui



hana diplomasia



anakurupuka



ameua uchumi



Ameua misingi ya demokrasia yote


huu ni zaidi ya udikteta

Note: Sijataja mtu anajijua mwenyewe abadilike aache udikteta na ugaidi wa kisiasa
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…