Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
I reserve my comments. I'll nchi ilioza. Ndio maana hata kwa kuanzia ilikuwa kazi
Kwani walio leta uozo ni nani?
Serikali iliyokuwa madarakani kabla 2016 ni ya chama gani?
 
Dhiki kuu.
 
Lombardi inaonekana unapata taarifa kutoka Fort Meade www.nsa.gov
 
Tatizo ni uvivu, wanavyoona nchi nyingine zinaendelea wanadhan serikali inagawa hela,
 
Faida zake ni sukari kupanda bei

wewe hujawahi kununua sukari

Wananchi vijijini ni masikini wa mlo mmoja

bado mafuta taa ya taa ya chemli ni bei mara 2

Umeme wa REA uko wapi, kila siku ahadi

Umepata taabu bure kumjibu huyo mboga nane kula kulala
 
Mkuu ulichokianza unakijua mwenyewe.
Unapotaka kutupeleka unakujua mwenyewe.
Ila sisi tunapambana kila siku tuijue kesho yetu.
Mkuu unatuua, tuache tu tuishi kivyetu na wewe uishi na mawazo/ maono yako.
Asante.
Umeandika "Mkuu Unatuua", unamanisha nini? Tunaomba Ufafanue maana hatujakuelewa mkuu
 
Mkuu ulichokianza unakijua mwenyewe.
Unapotaka kutupeleka unakujua mwenyewe.
Ila sisi tunapambana kila siku tuijue kesho yetu.
Mkuu unatuua, tuache tu tuishi kivyetu na wewe uishi na mawazo/ maono yako.
Asante.
Mmeshaanza kazi rasmi, au bado mpo kwenye rehearsal?
 
IPTL bado wanalipwa kinyume na maadhimio ya bunge
 
I
Kuna thread humu inaelezea ahadi za Magufuli nenda kaisome....

Halafu kuna Ilani ya CCM nenda kaisome pia.

Halafu rudi hapa uje kutuuliza ambacho hujakielewa..
Ilani kwa majibu wa kamusi ya kiswahili ni TANGAZO LA ZUIO, ANGALISHO JUU JAMBO FULANI.
 
duh angalia facial expr..ya jakaya.....
Wewe umeona ya Jakaya tu, hata wale wapiga makofi wengine waangalie usoni. Pia waangalie alipomsifia Shein kwa kung'angania madaraka.
"walivyofanya waliyoyafanya" imeweka mshangao kwa wengi.
 
Kwa nini na wewe unajibu kwa kishindo? Uwe unajipa muda wa kusoma na kuelewa. Au uliamka kutoka usingizini na kuamua kumalizia hasira zako kwa ndoto uliyoota?
Karibu kitaa kwenye nchi iliyotukuka ya wadanganyika.

Zamani nchi ile ya ndotoni ilikuwa na watu wa aina mbili. Watu kondoo ambao walikuwa kundi kubwa na watu mbwa koko ambao mfugaji wao aliwalisha na kuwapatia mahitaji yao bure.
 
Poleni ndugu, baada ya dhiki faraja
 
Msijali bado hamjapotea,mkipotea kabisa ndugu zenu watawatangaza kwenye bango la tbc
 
Huku niliko giza tu.
..nani yuko karibu na soketi awashe taaa?? Yaani nilipo sijui ni wapi
 
Naweza sema bado nchi yetu inatambaa kwa miaka mingi sana ila imeshindwa kutembea hata basi kusimama tu.

Hakuna mzazi anaependa kuona mwanae akiwa kiwete ila kwetu sisi wananchi na Watanzania tunashuhudia nchi ikiwa kiwete na imeshindwa kusimama hata (dede).

Naombeni tujifananishe na Rwanda wakati wao wanatwangana vita sisi tulikuwa huru kabisa yaani tena kwa raha zetu tukivinjari ila vita ile iliyokuwa na madhara makubwa kwao haikufanya Rwanda kurudi nyuma katika ujenzi wa uchumi wa maana na wa kueleweka.

Tunajivunia sana historia na ndio chanzo kinachotufanya tuzikumbatie hata kama ni za kipumbavu mfano historia moja ipo inayosema kuwa Tanzania ni kisiwa cha amani Amani gani Albino wanauliwa? Amani gani tembo wanapukutika kama majani kwenye mti hiyo amani yetu ni amani gani tunazungumzia amani ya ndoa au amani ya ukimya?

Sitaki kuzungumzia hilo ila nirudi niangalie katika mwelekeo wetu huko mbeleni ni wapi tunaenda kwanini Warwanda na Watanzania wana tofauti sana katika uchumi katika nchi zao ni wingu gani limetushika tumeshindwa hata kutengeneza kiwanda cha sindano ya mkono ili kuendeleza taifa letu?

Tanzania kwa nini tunapewa hadithi kuwa tuna madini Ghali Duniani ile hali hatujui chochote hata kuhusu mikataba hiyo na wawekezaji wa kigeni?

Tunapochafuliwa kuwa sisi ni nchi yenye rasilimali nyingi katika uso wa dunia na sisi kutuna bila aibu inaonesha ni ujinga kiasi gani tulionao kwa kushindwa kuthamini kile tulichonacho?.

Deni la taifa linapofika Trillion 45 tunategemea kulilipa au dawa ya deni ni kukimbia anaekudai, tunashindwa kuwa huru kisa madeni haya ambayo sijui yalifanya kazi gani hapa nchini (Nani anajua hizi Trillion 45 tunazodaiwa zilitekeleza mradi gani hata wajukuu wakija niuliza niwape majibu yasiyo na kwanini).

Mwisho kabisa hakuna siku mtanzania alifurahia serikali huku wakicheka wale wanalia, wale wakilia hawa wanacheka MIMI KWA UPANDE WANGU SIJUI TANZANIA INAELEKEA WAPI NA HUU UTAJIRI WA RASILIMALI ZAKE ZINAZOFANYA KUONEKAMA KUBWA JINGA.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…