Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Tanzania yangu hizi phd(permanent head damage)..na usomi wote hausaidii hii nchi kwenda mbele.. kwamba watu wameweka masilahi..yao binafsi na ya vyama..mbele zaidi kuliko nchi... cha zaidi Wananchi wananchi kuumizwa...kwa maamuzi ambayo hayana upeo wa kuunganisha watanzania..bika kujali..itikadi...kwa nchi hii ni janga kubwa .. mungu ibariki Tanzania na watu wake ...
Dhiki kuu.
 
Kuna pressu kubwa sana ya ndani kwenye mifumo! Ndio maana anasisitiza kuombewa! Ameshapewa info zote jinsi uprising ilivyosukwa toka kwa ndugu wa baba kambo kama angetumbua Lugumi na Dr Msomi sana wa Darajani.....!!amestuka! Angekwenda na maji!!! Angalau busara imemfikia akakubali ushauri!
Lombardi inaonekana unapata taarifa kutoka Fort Meade www.nsa.gov
 
Mmekazania sukari tu,hebu tumieni akili kidogo,mbona ilipoondolewa service charge ya Tanesco moja Kwa moja hamsifii??,ongezeko kidogo la sukari tena Kwa muda mfupi mmekomalia sukari tu kila siku,jaribu kufatilia kwanini vibali vimedhibitiwa na faida zake,inasikitisha sana vijana wa ki TZ ni walalamishi kupita maelezo na kila kukicha mnakuja na mbinu Mpya za ulalamishi,sijui ni matatizo ya kurithi??
Tatizo ni uvivu, wanavyoona nchi nyingine zinaendelea wanadhan serikali inagawa hela,
 
Faida zake ni sukari kupanda bei

wewe hujawahi kununua sukari

Wananchi vijijini ni masikini wa mlo mmoja

bado mafuta taa ya taa ya chemli ni bei mara 2

Umeme wa REA uko wapi, kila siku ahadi

Umepata taabu bure kumjibu huyo mboga nane kula kulala
 
Mkuu ulichokianza unakijua mwenyewe.
Unapotaka kutupeleka unakujua mwenyewe.
Ila sisi tunapambana kila siku tuijue kesho yetu.
Mkuu unatuua, tuache tu tuishi kivyetu na wewe uishi na mawazo/ maono yako.
Asante.
Umeandika "Mkuu Unatuua", unamanisha nini? Tunaomba Ufafanue maana hatujakuelewa mkuu
 
Mkuu ulichokianza unakijua mwenyewe.
Unapotaka kutupeleka unakujua mwenyewe.
Ila sisi tunapambana kila siku tuijue kesho yetu.
Mkuu unatuua, tuache tu tuishi kivyetu na wewe uishi na mawazo/ maono yako.
Asante.
Mmeshaanza kazi rasmi, au bado mpo kwenye rehearsal?
 
IPTL bado wanalipwa kinyume na maadhimio ya bunge
 
I
Kuna thread humu inaelezea ahadi za Magufuli nenda kaisome....

Halafu kuna Ilani ya CCM nenda kaisome pia.

Halafu rudi hapa uje kutuuliza ambacho hujakielewa..
Ilani kwa majibu wa kamusi ya kiswahili ni TANGAZO LA ZUIO, ANGALISHO JUU JAMBO FULANI.
 
duh angalia facial expr..ya jakaya.....
Wewe umeona ya Jakaya tu, hata wale wapiga makofi wengine waangalie usoni. Pia waangalie alipomsifia Shein kwa kung'angania madaraka.
"walivyofanya waliyoyafanya" imeweka mshangao kwa wengi.
 
Sio peke yako mnaoamini kuhusu kishindo its a stage in ur dreaming brain called "denial"kwa serikali ya sasa blaza mlianza kwa kushindwa znz mkarudia but sumu sasa ipo mtaani and its spreading like a plague deep down nnchi is worsening msingekumbatia polisi hivi kama sio uwoga na kutojiamini "TRUTH HAS A WAY OF COMING OUT AND WHEN IT DOES EVERYTHING CHANGES".
Kwa nini na wewe unajibu kwa kishindo? Uwe unajipa muda wa kusoma na kuelewa. Au uliamka kutoka usingizini na kuamua kumalizia hasira zako kwa ndoto uliyoota?
Karibu kitaa kwenye nchi iliyotukuka ya wadanganyika.

Zamani nchi ile ya ndotoni ilikuwa na watu wa aina mbili. Watu kondoo ambao walikuwa kundi kubwa na watu mbwa koko ambao mfugaji wao aliwalisha na kuwapatia mahitaji yao bure.
 
Sukari yetu tulikuwa tunaipata kwa shs 2000 kwa Kilo Taratibu

sukari ni bidhaa ya mnyonge

Wakatia neno, sukari ikaadimika na sasa ni 2500 kwa kilo

Bado nishati ya kupikia ni ghali...Gesi ya majumbani bei ni juu,

watu wanakata miti ya kuni na mkaa

Wakapandisha VAT ya utalii ghafla....

Mafuta taa kodi yake ni mara 2

Kijiini hakuna umeme, mafuta taa ni ukombozi ila sasa ni hatari.... Watu wa mikoa pembezoni wanachukua mafuta taa Kenya na Zambia
Poleni ndugu, baada ya dhiki faraja
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Msijali bado hamjapotea,mkipotea kabisa ndugu zenu watawatangaza kwenye bango la tbc
 
Huku niliko giza tu.
..nani yuko karibu na soketi awashe taaa?? Yaani nilipo sijui ni wapi
 
Naweza sema bado nchi yetu inatambaa kwa miaka mingi sana ila imeshindwa kutembea hata basi kusimama tu.

Hakuna mzazi anaependa kuona mwanae akiwa kiwete ila kwetu sisi wananchi na Watanzania tunashuhudia nchi ikiwa kiwete na imeshindwa kusimama hata (dede).

Naombeni tujifananishe na Rwanda wakati wao wanatwangana vita sisi tulikuwa huru kabisa yaani tena kwa raha zetu tukivinjari ila vita ile iliyokuwa na madhara makubwa kwao haikufanya Rwanda kurudi nyuma katika ujenzi wa uchumi wa maana na wa kueleweka.

Tunajivunia sana historia na ndio chanzo kinachotufanya tuzikumbatie hata kama ni za kipumbavu mfano historia moja ipo inayosema kuwa Tanzania ni kisiwa cha amani Amani gani Albino wanauliwa? Amani gani tembo wanapukutika kama majani kwenye mti hiyo amani yetu ni amani gani tunazungumzia amani ya ndoa au amani ya ukimya?

Sitaki kuzungumzia hilo ila nirudi niangalie katika mwelekeo wetu huko mbeleni ni wapi tunaenda kwanini Warwanda na Watanzania wana tofauti sana katika uchumi katika nchi zao ni wingu gani limetushika tumeshindwa hata kutengeneza kiwanda cha sindano ya mkono ili kuendeleza taifa letu?

Tanzania kwa nini tunapewa hadithi kuwa tuna madini Ghali Duniani ile hali hatujui chochote hata kuhusu mikataba hiyo na wawekezaji wa kigeni?

Tunapochafuliwa kuwa sisi ni nchi yenye rasilimali nyingi katika uso wa dunia na sisi kutuna bila aibu inaonesha ni ujinga kiasi gani tulionao kwa kushindwa kuthamini kile tulichonacho?.

Deni la taifa linapofika Trillion 45 tunategemea kulilipa au dawa ya deni ni kukimbia anaekudai, tunashindwa kuwa huru kisa madeni haya ambayo sijui yalifanya kazi gani hapa nchini (Nani anajua hizi Trillion 45 tunazodaiwa zilitekeleza mradi gani hata wajukuu wakija niuliza niwape majibu yasiyo na kwanini).

Mwisho kabisa hakuna siku mtanzania alifurahia serikali huku wakicheka wale wanalia, wale wakilia hawa wanacheka MIMI KWA UPANDE WANGU SIJUI TANZANIA INAELEKEA WAPI NA HUU UTAJIRI WA RASILIMALI ZAKE ZINAZOFANYA KUONEKAMA KUBWA JINGA.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom