Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kweli mkuu msema kweli mpenzi wa Mungu.mambo yamekuwa magumu mpaka basi .yaani tokea nmezaliwa sijawahi kutana na life ya ivi kwenye nchi yenye utajili kama hii.nikimkumbuka Jk nalia alikuw mpigaji ila wananchi tulikula na kusaza na tulikuwa huru.sio uyu mkuu wa malaika [emoji57][emoji57]
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Hatuwezi kuwa na Rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.
Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli, hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya Rais au Waziri Mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.
Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.
Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu.
Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je, anajua jinsi ya kututoa?! Anajua anakotupeleka?
Nimejitahidi kuangalia Bunge ili nione labda Mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.
Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Kwani mnaenda wapi ?Binafsi nadhani ana nia nzuri.
Lakini sidhani anajua anakoelekea.....
Yupo yupo tu.
Tuambie anaipeleka nchi wapi na lini?epuka 'r' panapotakiwa 'l'
neno lolote ambalo ni kinyume, herufi 'a' lazima iwe 'ha'.
Magufuli ni chaguo la watu, maamuzi ya wengi ndio yaliyomuweka kuwa Rais Magufuli. unataka Rais awe anachaguliwa na familia yako ndio atakiwe kuwa? Rais Magufuli yupo pale akiwakilisha watu wengi. Hakuna kiumbe yeyote duniani anayependwa na kila mtu , hivyo watu kama ninyi lazima muwepo tu ila wenzako wakikusikia unasema haya maneno, wataanza kuhoji mwenzetu kapatwa na nini mpaka apingane na uamuzi wa wengi?
Mlamba nyayo,tuelezee anatupeleka wapi?epuka 'r' panapotakiwa 'l'
neno lolote ambalo ni kinyume, herufi 'a' lazima iwe 'ha'.
Magufuli ni chaguo la watu, maamuzi ya wengi ndio yaliyomuweka kuwa Rais Magufuli. unataka Rais awe anachaguliwa na familia yako ndio atakiwe kuwa? Rais Magufuli yupo pale akiwakilisha watu wengi. Hakuna kiumbe yeyote duniani anayependwa na kila mtu , hivyo watu kama ninyi lazima muwepo tu ila wenzako wakikusikia unasema haya maneno, wataanza kuhoji mwenzetu kapatwa na nini mpaka apingane na uamuzi wa wengi?
Hilo halina ubishi yeye mwenyewe kakiri mara kadhaa kuwa hakuutaka urais alikuwa anabip tu lakini wakapokea na wakamsukumizia. Amesema pia hiyo kazi ni ngumu kiasi kwamba amehamishia mafail yote kitandani hadi kukosa mahali pa kulala. Amesema pia kumwambia mkewe kuwa kazi ni ngumu kiasi kwamba huwa anashindwa hata kula chakula cha jioni. Uzuri ni kuwa yeye mwenyewe ndiye anayesema hadharaniLeo siandiki mengi kama mlivyozoe maandiko yangu..Nasema tu JPM akutakiwa kuwa mkuu au mtawala wetu kabisa ..Utawala na uongozi wa Taifa siyo uwakirishi au unyampala.
Huyu akutakiwa kuwa mtawala wala kiongozi wetu.