Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Karibuni sana great thinkers wote tujadili na kutafakari mapungufu ya kimfumo na uendeshaji wa serikali ya Tanzania kuanzia awamu ya kwanza wakati tunapata uhuru mpaka utawala huu wa John Pombe Magufuli .

Tujadili bila ushabiki wa kisiasa juu ya mapungufu hayo na tutoe mapendekezo yanayoweza kusababisha mapinduzi makubwa ya kimandeleo kwa wananchi na uchumi wa Taifa letu kwa ujumla

Sisi wote ni mashuhuda wazuri wa lindi kubwa la ufukara na muelekeo mbovu wa uchumi wa Taifa letu kwa sasa .

Ninaamini tunaweza kubuni mfumo
Mzuri na ambao unafaa katika Taifa letu ili kujikwamua na kutupeleka katika hatua nyingine kubwa sana .

Wakati tunapata uhuru katika taifa letu kuna nchi kama Korea , Taiwan , Vietnam nk ambazo tulikuwa nazo au tulikuwa tunatofautiana kidogo sana katika level ya kimaendeleo ya kiuchumi . Leo hii sisi ndo wakuomba misaada kwao ,

Je ni wapi tumejikwaa na ni jinsi gani tunaweza kujikwamua kutoka katika giza hili ?

Kuna msemo maarufu unasema "Welevu hujifunza kutoka katika makosa ila wapumbavu huendelea kufanya makosa bila kujifunza chochote toka kwayo " .

ONYO :
Matusi na kejeli hayaruhusiwi , tujadili na kupambana kwa hoja na si matusi

Karibuni wakuu .

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app

Ukianzisha ' Uzi ' wa Kuzijadili akili mbovu za baadhi ya Watanzania ambao Kutwa wanailaumu Serikali tu, wakati na Wao kama Wananchi wana ' Mapungufu ' yao makubwa naomba ' Unitagi ' tafadhali ili nije nitiririke na niserereke kwa uzuri kabisa bila Kupepesa macho, Kutikisa masikio na Kumung'unya maneno.
 
Ufisadi tilioni 2.4 ,mauaji ,utekaji , uvunjaji wa katiba na sheria , uteuzi wa wasio na sifa hasa Rc ,DC ,Ded ,Ra's ,Das ,matumizi mbaya ya usalama wa taifa kugeuzwa usalama wa ccm , uvunjaji wa haki za binadamu ,demokrasia na utawala bora , ccm yenyewe tu ni tatizo haitakiwi kuwepo kabisa , matumizi mabaya ya polisi ,mihimili ya bunge na mahakama kuingiliwa ,manunuzi ya bila kufuata utaratibu , One man show , matumizi mbaya ya madarakani ,matumizi mbaya ya Mali ya umma ,ubabe ,visasi ,maamuzi ya kukurupuka ,ukali wa Mkuu na kutoshaurika .
 
Karibuni sana great thinkers wote tujadili na kutafakari mapungufu ya kimfumo na uendeshaji wa serikali ya Tanzania kuanzia awamu ya kwanza wakati tunapata uhuru mpaka utawala huu wa John Pombe Magufuli .

Tujadili bila ushabiki wa kisiasa juu ya mapungufu hayo na tutoe mapendekezo yanayoweza kusababisha mapinduzi makubwa ya kimandeleo kwa wananchi na uchumi wa Taifa letu kwa ujumla

Sisi wote ni mashuhuda wazuri wa lindi kubwa la ufukara na muelekeo mbovu wa uchumi wa Taifa letu kwa sasa .

Ninaamini tunaweza kubuni mfumo
Mzuri na ambao unafaa katika Taifa letu ili kujikwamua na kutupeleka katika hatua nyingine kubwa sana .

Wakati tunapata uhuru katika taifa letu kuna nchi kama Korea , Taiwan , Vietnam nk ambazo tulikuwa nazo au tulikuwa tunatofautiana kidogo sana katika level ya kimaendeleo ya kiuchumi . Leo hii sisi ndo wakuomba misaada kwao ,

Je ni wapi tumejikwaa na ni jinsi gani tunaweza kujikwamua kutoka katika giza hili ?

Kuna msemo maarufu unasema "Welevu hujifunza kutoka katika makosa ila wapumbavu huendelea kufanya makosa bila kujifunza chochote toka kwayo " .

ONYO :
Matusi na kejeli hayaruhusiwi , tujadili na kupambana kwa hoja na si matusi

Karibuni wakuu .

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii aliyolalamikia CAG sijui ni changamoto au mapungufu, je limeshasawazishwa, kushughulikiwa, kunyooshwa au kuwekwa sawa?

Link Kwa mujibu wa Sheria mpya za madini, CAG hana mamlaka ya kukagua migodi - JamiiForums


Aliyetengeneza sheria amehamishiwa Wizara ya TunduLissu na ushirikiano wa ........
 
Huu ni uzi muhimu, ila jina halijakaa vizuri, kwa sababu wenyewe wenye serikali yao, hawapendi kuambiwa ukweli kuwa wana mapungufu, na serikali ina mapungufu, hivyo badili title uiite " Kuijadili Changamoto za Serikali Awamu ya Tano".
P
P,nawe sio mzalendo? Mtoa mada amejificha kwenye utambulisho. Kiongozi wa ukoo amesema yeye ndiye ukoo wenyewe.
 
Sijui unashangaa nn, Mzee wetu hakuwaza kama iko siku atakuwa yeye, hivyo hakuwa na hana mpango ulioandaliwa. Hana ramani, ndiyo maana hata ilani imewekwa pembeni, na sasa OSHA, NEMC na vingine ambavyo vipo Kwa mujibu wa kanuni.
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Hatuwezi kuwa na Rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli, hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya Rais au Waziri Mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu.

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je, anajua jinsi ya kututoa?! Anajua anakotupeleka?

Nimejitahidi kuangalia Bunge ili nione labda Mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
"ANATUTOA MISRI ANATUPELEKA KANAANI"

Full sto!
 
Wakuu nchi yetu (Tz) iko pabaya sana. watalaamu wa sheria na mambo ya uchumi hili mnalitambua wazi, mnatupeleka wapi, chukueni maamuzi magumu kunusuru taifa hili, hivi mnajadili mnapokutana na wasomi wenzenu? au huwa mnawaambia ukweli kwamba 'HAYA TUNAYOFANYA YANAWEZEKANA TANZANIA PEKEE'??????
Enyi watumishi na wateule wa Mh. Rais mmeshindwa kusimama imara na kulitetea taifa kwel!

Huko mbinguni mnakokusema kuwa mtapokelewa kwa bashasha, walahi nawaahidi mtapokelewa na jehanamu ya moto wa gesi.

Ukweli uko hivi ingawa mnaficha, wacha niseme ukweli. Ukweli ni kwamba serikali ya awamu ya tano imeharibu mahusiano ya kidiplomasia na nchi zingine, watanzania wenzangu yafuatayo ndiyo yajayo na yanafurahisha je mko tayari?.

1. Mradi wa bomba la Mafuta kutoka Uganda to Tanzania haupo tena, Siwezi kujua kama alietoa maamuzi au ushauri uliopelekea tatizo hili ni raisi/waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa/mwanasheria mkuu wa serikali, serikali yetu inalazimisha kuwa endapo kutatokea mgogoro wowote kwenye mkataba wa ujenzi wa bomba la mafuta, usuluhishi(arbitration) ufanyike kwenye mahakama zetu za ndani, wazungu wakupe hela then uwape mashariti kwenye hela zao? Kikao cha raisi wa uganda na kenya kilifichofanyika Kenya mwezi uliopita walienda kupanga namna ya kupata zile hela ili miradi hiyo ihamie kenya to uganda, sisi ni mashahidi Kenyata kashajiongeza juzi alikuwa na Odinga wakijianda kwenda nje kutafuta misaada.

2. Mradi wa umeme Stigler G. tunaojivunia na kupigia makerere kila siku mradi huu utaishia njiani, ukweli ni kwamba hawa jamaa wanatusindikiza tuanze hii kazi tukifikia nusu wataleta vikwazo na kutelekeza mradi.

Nimesema ni tetesi, najua mlioko ndani ya mfumo uhalisia mnaujua kuliko sisi waganga njaa na masufuria ya mama lishe tulioko huku nje ila mnaogopa kwa sababu mnahofia kupoteza ulaji, lakini ukweli ni kwamba leo mmekula kumbukeni kesho inakuja, hilo shimo mnalochimba tutazama sote na watoto wetu. YAJAYO YANAFIKIRISHA.

Najiandaa kuhamia Zimbabwe/mikoani nikalime maana muda sio mrefu hapa Dar es salaam hapatakalika
 
Kumbe William Ruto na Laila safari yao ya China ni kwenda "kukopa" kwa ajili ya bomba la mafuta?!!! Sasa mkuu mbona hata kabla safari haijaanza wameishajigawa makundi mawili ya safari? Jiulize kama wewe ungekuwa unakopesha Mr na Mrs wakaja tofauti huku ukiona hawa jamaa hawaivi?

Hebu jikumbushe malalamiko ya wakenya kuhusu "kupigwa" kwenye ujenzi wa reli ya kisasa na sasa waongeze na bomba la gesi......

Kama madaktari tu wa kujitolea kutoka Cuba wananyakuliwa na Alshabab kama kipanga je hao mafundi na mradi wao unadhani utakuwa salama...hakuna mwekezaji mjinga anayeweza kuwekeza Kenya kwa sasa!

Sisi watanzania tunaamini "KAMA IPO IPO TU"
 
Hivi naombeni kujua wanaopanda zile ndege alizonunua mheshimiwa ni wakina nani? Ni asilimia ngapi ya wale wanyonge wake watazipanda?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom