Tigershark
JF-Expert Member
- Oct 9, 2018
- 7,051
- 12,566
Huu uzi utaishi sana!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yupo yupo tuBinafsi nadhani ana nia nzuri.
Lakini sidhani anajua anakoelekea.....
Yupo yupo tu.
Ha ha haaa unahisi ameshaokotwa kwenye kiroba?Mwanzisha mada yupo wapi maana naona Last seen march 2018?
Adm atusaidie kupata taarifa
Kwa hiyo mkuu saizi unajua anakoelekea?nadhani ana nia nzuri.
Lakini sidhani anajua anakoelekea.....
Yupo yupo tu.
Nilishaandika mada mbili tatu kuhusu yanayojiri, kwa wenye kufahamu walielewa: Tahadhari kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya: Maigizo mnayofanya yatawagharimu... - JamiiForums
Mbona kila mtu anajua jpm anatupeleka wapi wewe tu ndio hujui. Watu wema wote watu wanayopenda maendeleo wote wanajua. Wewe labda ulitumbuliwa kwa cheti feki ndio maana hujui.Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Hatuwezi kuwa na Rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.
Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli, hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya Rais au Waziri Mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.
Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.
Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu.
Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je, anajua jinsi ya kututoa?! Anajua anakotupeleka?
Nimejitahidi kuangalia Bunge ili nione labda Mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.
Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!