Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Huwa nachukizwa nakauli kwamba watu flani nimafisadi akafuhawakamatwi hii inamaanisha serikali haiwez kuwakamata?
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Hatuwezi kuwa na Rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli, hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya Rais au Waziri Mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu.

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je, anajua jinsi ya kututoa?! Anajua anakotupeleka?

Nimejitahidi kuangalia Bunge ili nione labda Mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Mbona kila mtu anajua jpm anatupeleka wapi wewe tu ndio hujui. Watu wema wote watu wanayopenda maendeleo wote wanajua. Wewe labda ulitumbuliwa kwa cheti feki ndio maana hujui.
 
Assalaam Alleikhum....
Niseme tu kila nabii na kitabu chake,kila zama zina mambo yake,awamu ya tano/awamu ya jiwe inaongozwa zaidi kimkakati na propaganda,falsafa nyingi sana zimezaliwa,wananchi wamekaririshwa kuamini serikali haikosei,na atakayeona serikali inakosea na akapaza sauti huitwa 'si mzalendo',kwenye uzi huu nitaangazia dhana/kauli mbalimbali ambazo hutumika/zimetumika kama kichaka cha kunyima stahili za mwananchi bila mwananchi mnyonge kugundua kirahisi
1.Uchochezi_kuminya haki ya kutoa maoni/mawazo
2.Watu wasiojulikana_kukwepa jukumu la kuwajibika haswa kwa vyombo vya ulinzi
3.Uhakiki ni Endelevu_kuminya stahili za mtumishi
4.Sio Mzalendo_hii imetumika kuwajengea chuki kwa raia viongozi wanaoikosoa serikali
5.Hapa kazi tu_ni kauli ya muendelezo wa kuminya maslahi ya mtumishi,kuminya haki ya mikusanyiko n.k
6.Uchunguzi/Upelelezi haujakamilika/kesi itaskikizwa mwezi flani_hii ipo kimkakati kukomesha mtu fulani aendelee kusota rumande
7.Serikali ina pesa_ni muendelezo wa kuhadaa umma kwamba mambo yanaenda vizuri hata kama sio kweli.
Unaweza kuongeza dhana au kauli zingine zilizozaliwa/kuasisiwa katika awamu ya Jiwe ambazo yamkini unaziona zipo kipropaganda au kimkakati zaidi...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akina Pole pole, nawaccm wote ni waongowaongo, hawana vision wala strategies ndio maana tunayumba kama vichaa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom