Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Usafiri wa anga unaibua utalii? Tumia akili zako siyo za kufikirishwa, hakuna mtalii atakuja na ATCL wanakuja na ndege za kwao na ndizo wanarudi nazo, ndege siyo Uber utakayoiita ije ikubebe.
 
Wameamua kuwa wapumbavu na hakuna wa kuwasaidia kuondokana na upumbavu wao.
 
Rais wa wanyonge ni wimbo ambao nimekuwa nikiusikia masikioni mwangu kila mara.

Mimi sina mengi, naomba wanyonge tuambizane nini mmepata kwa utawala huu, angalau wengine tujiunge na kundi hilo tufaidike.
 
Mkiandikaga nyie ngumu kueleweka mpaka sisi tuliomo ndani ya chama ingawa una point
 
Unaongelea vijijini?!

Dar hiiii hiiii ambayo hamna Taifa linaloijua Tanzania Lisiiijue DAR

Maji ni shida na ya Tabu (baadhi ya sehemu hadi leo)

Utasema huku nako ni kijijini? AU unataka kusemaje kwa mfano?

Huko unapopaita kijijini wako hivyo kwa sababu Maji hawana Pesa hawana

Huku mjini MAJI HATUNA pesa tunayo ila point ni MAJI so Unatakiwa ulie kilio kimoja tu

Tanzania tupate Rais wa kusema MAJI ni kipaumbele chake kama Magu alivyoamua Miundombinu ndio kipaumbele chake

ila huwezi acha pongeza anayofanya Rais kwa sasa,ukija na point yako hiyo ya Maji asee utatolewa knock out.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria mwezi Julai mwaka 2017 katika eneo la Kazehill Manispaa ya Tabora, hakuna aliyekuwa akiamini kama mradi huo utakamilika kabla ya muda wake wa miezi 30 kwa mujibu wa mkataba uliosainiwa.



 
Tumepata Ndege, Stigilaz goji, SGR, Madaraja, Flayiova, mabarabara, wahujumu uchumi wamepitisha maburungutu n.k

#Maendeleo_hayana_chama
 
Mada kama hizi ndio huwa zinawashushia hadhi wapinzani.

Yani ni sawa na mtu ahoji kwamba badala ya kuchukua hela ufungulie duka kwanini hiyo hela usiwanunulie watoto nyama wakala?

Kwa mtu mwenye akili fupi kama mleta mada ataona kweli aisee!
Kumbe hilo duka ndio litawafanya wawe wanakula nyama miaka yote.
 
Plan B pekee mifumo ya umwagiliaji na kuvuna maji ya mvua ya ziada angeweza kuongeza tija ya kilimo na malighafi za uhakika viwanda. Ingepunguza wanyonge wengi na multiplier effect ya uchumi ingekuwa kubwa sana. Hata hitaji la std gauge nk ningefuata
Kumwagilia zao gani ?
Soko lake lipo wapi ?
 
Matusi na kejeli, Kura yake imemfanya ashinde urais.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Nmekupa LIKE mkuu...ila subiri matusi kutoka ufipa
 
Kula LIKE
 
Sisi kule kijijini kwetu kama unavyo jua Iringa kuna milima, sasa walichofanya wananchi wakaenda kule milimani ambapo ndio kuna maporomoko ya maji, wakachimba mtaro kuanzia kwenye ule mporomoka huo mtaro ukaenda hadi kijijini umbali wa kilometa kama 15,

Baada ya ule mtaro kukamilika, ilichofanya selikali ni kuwaletea tu mpira wakaenda kuutega pale linapoanzia lile poromoko maji yakaelekea kijijini, huwezi amini kwa presha ya yale maji huwa inafika wakati yanapasua mabomba, na inabidi waachie mengine yamwagike ili kupunguza presha.

Na huwezi amini yale maji hakuna mambo wowote unaoyasukuma.

Point yangu ni kwamba Tanzania hakuna kijiji kisicho na chanzo cha maji, shida ni kuyatoa huko yaliko kuyaleta kwa wakaazi. Na hapo ndio unakuta kila kitu wanangojea selikali.
 
Umasikini wa kujitakia, mtu huna hela unaishi kijijini kula shida bado unazaa watoto 10, huna pa kuwalisha, watu wa vijijini wanatuongezea umasikini bora wachinjwe wabaki wale wanaojiweza, hawa wengine futilia mbali kama iddi amini

Nilimsikia magufuli anawashawishi watu wazae kiholela ili 'wakuze uchumi' wa Tanganyika!
 
CCM na wapambe mnaposema Rais wa wanyonge huwa mnamaanisha wakina nani
Wanyonge ni watu ambao wanaoonewa na wale wenye wadhifa au nafasi fulani kwenye serikalini. Mfano awamu ya nne kulikuwa na kitu ile ya "unanijua mimi nani" waliokuwa wanasema hivyo ni wababe wanyonge walikuwa wanaufyata.

Ila kwa dhana ya maendeleo hatuwezi kuwa sawa ndo maana kuna Bar bia elfu 10 na nyingine bei elekezi ya TBL na kote kuna watu. Kwa hiyo huwezi kumfurahisha kila mtu.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…