Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
nikifuatilia comment za RAIA zaidi ya 60% wamesha mchoka tofauti na alipp kua ananza
 
Wapatikane wapi wakati tunao hapahapa kwetu, tatizo hatutaki kuwatumia!
 
Naamini wote hao wanaona na wanafuatilia vioja vya JPM na ninaamini huwa wanaziba nyuso kwa mshangao lakini hawafanyi lolote kwa sababu wanajua watakuwa wanapoteza muda na busara zao maana yeye anajua kila kitu. Kwa hiyo ni "ngoja aicheze ngoma yake mwenyewe."
 
We ndo nabii nani?
 
Makanisa na misikiti yao ikifungwa je watakuja kwako? Yule bwana ana phd ya kemia. Si unajua ni wachache sana? He knows what he is doing
 
Leo nimeona raisi akiendelea kuomba kula uko singida....!!hivi hakuna mtu wakumshtua raisi a mwambie kuwa kampeni zimeshakwisha na yeye ndo anaedhaniwa alitangazwa kuwa mshindi!?
hahaha,andiko mujarabu
 
Huyu jamaa balaa alilianza pale aliposema atawafanya waTz waliokuwa wanaishi kama malaika waishi kama mashetani!

Mwenyezi Mungu katika vitabu vyake vyote vya dini, anatamani binadamu wote waishi maisha ya utakatifu na yeye Mungu hapendi hata binadamu mmoja apotee na kuishi kama shetani...........

Kwa kauli ile ni dhahiri Mkulu 'alibugi step' na ndicho kinachoweza kuwa chanzo kilichopelekea anatoa matamko yenye ukakasi mkubwa mfululizo.........
 
Mie nashauri tutulie tuone mwisho wake utafka wap!... Wala tusiangaike tufanye mambo yetu
 
Hakuna wa kushauri tofauti kwani tumemkubali na tunamwamini tuko naye bega kwa bega. Akisonga na sisi tunasonga. Go go our president....
 
Inasikitisha na inahuzunisha sana kwa Tanzania kuwa na Rsis wa aina ya Magufuli!
Tangu ameingia madarakani mheshimiwa JPM amekuwa ni mtu wa kutoa matamko yasiyo zingatia Katiba na Sheria na hii ni hatari sana! Rais anayeongoza Taifa lenye takribani watu milioni 50 kwa kuongozwa na hisia au mihemko ni janga kwa Taifa!
Kila kitu au mtu kuna sehemu ya uzuri na ubaya na huo uzuri au ubaya unapimwa kwa kuangalia upande upi unaoelemea mwingine!
Pamoja na sifa ya JPM kupambana na Ufisadi na kusaidia vijana wetu kielimu katika machache mazuri mizani inaelemea kwenye Wingi wa ubaya. Kitendo cha kuendesha nchi bila kufuata Katiba au Sheria ndiyo inabeba ubaya wa JPM kwa asilimia kubwa kama ni kwa aslimia basi ni 60-80%!
Kwa kiwango hichi cha ubaya wa JPM anajitengenezea kaburi lake na la chama chake cha CCM! Laiti JPM angelikaa siku moja na kutafakari kura alizopata mwaka jana 58%(8m votes) zidi ya UKAWA/Lowassa aliyepata 40%(6m votes) kati ya Watz milioni 40 alitakiwa kuwa mpole na kuwaheshimu wale 6m na wengine zaidi ya 25-30m ambao hawakupiga kura kabisa!
Kwanza Rais anapotamba na kuanza kuzuia mikutano ya siasa kwa kisingizio cha Hapa Kazi Tu siyo sawa! Rais anapozuia Bunge la JMT kuonyeshwa LIVE siyo sawa! Rais anapotumbua/fukuza/simamisha kazi watu bila kufuata taratibu na sheria za kazi hiyo si sawa!
Rais anapotisha wanachama tena wa Chama chake watakaompinga kuwapoteza hiyo si sawa!
Rais anapowatisha Wapinzani kuwa yeye Hajaribiwi na atakayejaribu ataona siyo sawa hata kidogo! Hawa Wapinzani wana haki na wana nguvu ya Kikatiba kufanya hivo na si kumjaribu JPM! Wana haki kuwatembelea na kufanya mikutano na wapiga kura wao zaidi ya 6m!Sasa unapozuia wasikutane eti tu kwa sababu hawakupata kura za kuingia Ikulu si sawa! Kwa maana hii JPM hatakiwi kufanya mikutano kwenye Majiji,miji na Majimbo yanayoobgozwa na wapinzani maana hawakumchagua! Je, hiyo ni sawa????
Nimalize kwa kusema kuwa OGOPA SANA MTU ANAYETANGULIZA UMIMI/UBINAFSI kwenye maswala ya kitaifa kana kwamba Tanzania ni nyumbani kwake,mkewe na watoto!
Sina hakika kama JPM amebahatika kusikiliza hotuba za wagombea Urais wa Marekani wa Demokratiki na Republican hasa mama Hillary Clinton ambsye Hotuba yake imesheheni "WE BELIEVE IN....." yaani Tuna amini na tutafanya 123,tuta...tuta....n.k! Na siyo NITA...... na majigambo kibao kama ya"Tanzania ya Magufuli,Serikali ya Magufuli n.k,n.k. Huo ni uzuzu wa kisiasa kutaka kuonyesha kuwa wewe peke yako unaweza na cyo Katiba ya nchi!
Kwa sheria na Katiba hizi anazotunga Rais majukwaani na kuungwa mkonon na Majeshi ya Ulinzi na Usalama ni hatari sana kwa mstakabari wa nchi!
Watu waombe na kusali sana ili Mungu aondoe moyo wa kiburi na jeuri ndani ya Rais wetu vinginevo.........!!!!!????
 
Mustakabali wa kinachoendelea kwa sasa utatoka ndani ya ccm yenyewe! Chama kimesurrender kwa mtu mmoja wote wanamsikiliza yeye tu! Anasema hadi 2020 serekali itakuwa imehamia dodoma kesho yake unasikia mawaziri kila mmoja anatamka tarehe ya karibu kuhamia dodoma kumshinda mwenzake, anasema sukari bei elekezi ni 1800 viongozi wote hadi Waziri mkuu nae anacheza wimbo huo bila hata kuhoji, anasema kuna watu walikuwa wanaimba tuna Imani na mtu fulani ningekuwa mimi mwenyekiti ningewapoteza watu wazima wanacheka kama mazuzu hata hawahoji ungewapotezaje? Anasema hapa kazi tu kila mtu anacheza hapa kazi tu wakati hamna kazi, anasema mikutano ya siasa hadi 2020 watu bila kuhoji wanacheza nyimbo yake hadi Waziri mkuu, hamna mwenye courage ya kumwambia umekosea, wakitoka njee ndio unasikia wanaulizana umemwelea muheshimiwa? Wengine ndio unasikia huyu jamaa haeleweki nakwambia hii nchi itamshinda. CCM ya sasa inaendeshwa na mtu mmoja wenye weledi wamebaki kushangilia ili wapate chakula cha kuishi!
 
Tuna Askofu mmoja tu Tanzania mwenye uwezo wa kusimama na kusema ukweli, maaskofu waliobaki ni majanga matupu wanafki tu.

Upande wa masheikh hawa ndio sina hata la kusema bei yao inajulikana, ike minoti waliopewa kwenda hija hakuna mwenye jeuri ya kuinuwa mdomo wake na kuonya.
 
sikio la kufa mkuu ..wahenga walituachia hiyo
 
umemwaga madini matupu mkuu
 
Reactions: BMT
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…