Hata kwenye hili janga la Corona, kuna watu wanaona kama tumepotea...
Mkuu TumainiEl, hatukuchagua malaika, tumemchagua binadamu, hivyo can make mistakes kama human beings wengine wote ndio maana tumemuwekea wasaidizi wa kumsaidia ikiwemo kumshauri, hawa wasaidizi ndio hawamsaidii ipasavyo!.
Nasisitiza hata kwenye janga hili la Corona, rais Magufuli asaidiwe sana na wasaidizi wake. Kila rais atakachoongea kama kina utata wasaidizi wake wajitokeze kuutatua utata wake.
Mfano vurus ana life span, baada ya muda fulani kama hajapata medium ya kuingia na kufanya mutation hawezi ku survive,
Rais Magufuli kasema kuna uwezekano barakoa zimetiwa virusi, wataalamu wajitokeze kufafanua.
Rais Magufuli ameponda Fumigation ya Makonda,
Hili lifafanuliwe.
Rais Magufuli ameshauri wananchi wajifukize, lifafanuliwe,
Rais Magufuli ameruhusu wananchi watumie barakoa za kujishonea, wataalamu walipaswa kujitokeza kesho yake kutoa muongozo hizo barakoa ziwekewe linings gani ndani ili zikidhi viwango etc.
Wasaidizi wa rais, hata kwenye hili la Corona, msaidieni rais Magufuli, msimuachie pekee yake.
P