JPM naye huwa simuelewi approach zake wakati mwingine!Wakati mwingine anaweza kuona jambo linafanyika kinyume akaliacha ili aje apate cha kuongea hadharani!Hivi,alishindwa nini kuwasiliana na Mkuu wa mkoa na kuzuia mazishi yasifanyike kinyemela na badala yake mwili usafirishwe?
Yaani anashindwa kuwasiliana na mtu aliyemteua?Hapa imenikumbusha suala la Makonda na jeshi la polisi kupuliza dawa,hivi alishindwa nini kuwasiliana nao na kuwahoji kisha kuwapa maelekezo badala yake anaangalia tu halafu anakuja kutema nyongo hadharani?Is this neccesary?
Kwanini yeye na timu yake akimshirikisha waziri wa afya wasingeshughulikia suala la maabara kwa pamoja kuona tatizo liko wapi?Je,uchunguzi ukionesha kuwa labda contamination inafanyika hapo hapo maabara kwa uzembe mdogo mdogo,atakuja vipi hadharani wakati ameshayatuhumu mataifa yanayotupa vifaa?
Tutakuwa wageni wa nani?
Something must be wrong somewhere!Wastaafu fanyeni jambo mkaongee na JPM!