Hii style ya mr. POMBE aliyokuja nayo ya kutumbua majipu kwa mtazamo wangu naiona itamgharimu sio muda mrefu. maana ilikuja kama kibwagizo cha kusherehesha mbio zake za Kuukwaa ukuu wa nchi. na ni kweli ameukwaa.
Tatizo hapa si kutumbua majipu kwa maana kwa sasa amekuwa akiimba kila siku MAJIPU...MAJIPU imefikia sasa hata kuwaambukiza watendaji wake nao wamekuwa ni wa kutumbua hata pasipokuwa na jipu wao WANAMINYAAA TU!! ili muradi wametumbua hata vidonda wakiviona wanatumbua ilhali vidonda havitumbuliwi. HII NI SHEEDAH!!
Kinachomsumbua MR. POMBE me binafsi naona kama hakioni au anapapasa tu na kuambulia MAJIPU. Lakini tumkumbushe au nimkumbushe tu kwamba majipu anayotumbua pasua ni pasua kichwa tu lkn watanzania wanaumwa kweli tena sio ugonjwa huo wa majipu anaohangaika nao kila kukicha.
Kawaida duniani hapa kila nchi majipu ni sehem ya maisha hivyo hawezi kuyamaliza na yatampotezea muda wake wa miaka mi5 aliyopimiwa na wananchi wake.
USHAURI:
Rais Magufuli nakushauri uachane na majipu sababu haya sio tatizo kuu la wananchi au linaloimaliza NCHI HII KWA UJUMLA WAKE. Naomba hayo majipu waachie vijana wako watahangaika nayo kwa kadri ya ulivyowapa maelekezo. Wakishindwa utajua nini cha kuwafanya. Najua style yako ile FUKUZA WEKA NDANI itawafaa sana hawa vijana japo haimo katika taratibu na sheria za ajira zetu.
Rais Magufuli nakushauri achana na MAJIPU tunajua yakipata dawa hata PARACETAMOL yanakauka lakini hi KANSA!! Pambana na KANSA KUU ndio inayoimaliza nchi hii na hii kansa ipo ndani ya watendaji wako na nyingine unazijua vizuri tu hizo kansa kama EPA ,ESCROW, LUGUMI, RICHMOND, KIWIRA, na nyingine nyingi tu.
Kweli sijakusikia unazigusia hata kiduchu tunasikia tu unapambana na wauza SUKARI na wakwepa kodi wa Kariakoo.
Hebu tuliza kichwa anza na kimoja kati ya hizi kansa tuonyeshe kweli unahasira nazo kama unavoonyesha hasira wakati wa kuwatumbua watendaji wako hadharani kama yule jamaa wa jiji uliyemuadhiri wakati wa ufunguzi wa daraja.