Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Leo nimepanda daladala,robo tau ya abiria walikuwa wanapiga miayo mpaka konda akalalamika,
Basi zima hakuna aliyetoa noti ya elfu kumi,elfu tano,au elfu mbili,ni hamsini hàmsini,miamia zilizochakaa.
Wengi walikuwa wamezifunga kwa nguvu kwenye pindo za nguo zao
 
Tayari nimeshaandika wosia.
 
Style yake ya uongozi ni kama ya Mugabe. Wananchi wa hali ya chini ndio tutaumia, yeye na familia yake watabaki salama kama ilivyo ada ya watawala wengi wa Afrika.
 
2020 inachelewa sana, jibu ndio litapatinaka aisee.
 
Ndio mjifunze kufanya saving, na maisha yenye utaratibu ndivyo kulivyo huko duniani kote....
 
Wanaokosea hupewa adhabu full stop
 
Kulikuwa na habari kuwa bank hamna hela za kukopesha mzunguko wa hela umekua mgumu, it was mentioned Kimei kasema, baadaye crdb wakakanusha kuwa hakusema na hela ziko kibao za kukopesha! Then bandarini watu wakasema hamna mizigo! Akaja jamaa wa bandari (sijui msemaji sijui mkurugenzi!) Akasema mizigo iko tele wala hakuna shida ya mizigo! Jana wamethibitisha mizigo hakuna na waende wakamshauri kama atapokea ushauri sijui
 
Mh. Rais ni vema abane uchumi mara 3 ya hapa. Ili watu wafanye kazi za kuzalisha. Vijana waondoke mjini wakajiajiri kwenye kilimo. Na kubana matumizi serikali itapata pesa ya kuwapelekea pembejeo, elimu ya kilimo cha kisasa na huduma za jamii. Mjini tuheshimiane.
 
Hanna hats hati ya mashitaka,mashahidi,hukumu? Atahukumu yeye hapohapo au?
 
Unafikiri kuongoza nchi ni vitisho na mikwara, nani awezae kupambana na wafanya biashara? Mlidhani mtawakomoa mlipokua mnawachukulia sukari yao nanyi mkishangilia? Ndo kwanza safari imeanza
 
Mkuu inabidi tuite fundi umeme....hii gari ina shoti na tunakoenda hatutafika,tutaungua humu ndani
 
Aache kutegemea mawazo ya PhD holders kutoka vyuo vikuu wao wana majibu ya kinadhalia ya Google. Wafanyabiashara, wakulima, wafugaji, wavuvi, meneja wa biashara na wafanyakazi kwenye makampuni makubwa ndo wana majibu kutoka field. Hao PhD holders kama hawajawahi kufanya biashara ategemee majibu ya kupika kama wanavyo cook data za research.
 
Kipindi changu hakutakuwa na pesa za bure bure - JPM. Sasa tulielie au tutafute shughuli za kipato tuendelee na maisha yetu.
 
Nchi imemshinda hi..kuna sehemu za kuleta ubabe siyo kwenye biashara za watu..
 
Na kweli tunakaa sawa,kama una pesa zako kipindi hiki ni cha kujizolea majumba/viwanja. maana hali ni mbaya kitaani.
Hata hao wanazo wanazikumbatia..Kwani wao hawaoni uchumi uporomoka mdogo mdogo
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…