Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Hatujawahi kuchagua "Kila siku tunaamua !
Kuchagua kuna maana
ya kuchuja faida na hasara !
Kuamua ni kumpa tu
pasipo kujihoji na kuangalia v
Vigezo !

Ukichagua hata matatizo
yakitokea mnayamaliza kwa amani !

Tusichoke kuombea Nchi yetu !
 
Raha ya bavicha ni kuona serikali ikishindwa kila kitu.

Sasa Mungu anazidi kuwaumbua mshindwe na mlegee kabisa
 
Daaaah nikikikumbuka kile kizee lubuva[emoji35] [emoji35] daaah ila IPO SIKU
 
Ndio mnyooke ili 2020 msirudie tena!..inatakiwa mnyooke sana mpate akili maana bila hivo hamuelewagi
 
Ile J3 ya 26/10/2015 nilikosa furaha kabisa nilijua tayari Maradona alishafanya yake, timu yangu ya England ikiwa imevalia mavazi meupe ilipokwa tonge mdomoni...hiyo ni baada ya kuangalia mipira ya zamani kwenye VHS mbovu pale home....ila kombe la dunia huchezwa kila baada ya miaka....anayejua aniambie
 
toka uchaguzi uishe hali imekuwa mbaya sana kwangu aisee hadi natamani nirudi utotoni nikale ugali wa mama na baba
 
dah kwa hali ilivyokua ngumu tutakumbuka mengi sana mwaka huu ila ndo hivyo hakuna namna
 
Hapo penye bei mbaya ya mazao umenigusa nimeuza mbaazi zangu kwa bei ya sh.500 kg1 ilianza bei ya sh.1300 imeporomoka mpaka kufikia sh500 kwa kg1

Utawala wa kikwete tuliuza 1500"1600" 2000" Mpaka kikwete anaondoka madarakani mwaka Jana tuliuza sh.1900" tukaishia sh.1800 kwa kg1
 
Raisi wetu kaziba mianya yote ya ufisadi,safari za nje empty,kafukuza mafisadi wote ni kwa sababu anabana matumizi,ila analalamika pesa haipo mtaani kwa kuwa watu wameficha,na kweli pesa mtaani ngumu hata biashara haziendi kabisa.najiuliza je ni mzimu wa lowasa unaanza kumwandama raisi wetu au? Maana lowasa anatuaminisha wananchi kwamba alishinda ila kaporwa ushindi wake(mi naita uchonganishi kati ya serikali na wananchi kama ilivokuwa Mwanahalisi).kwamba wafanyabiashara wameanza kumhujumu raisi wetu? Maana lowasa alisema yeye atakuwa lafiki wa wafanyabiashara.tujadili kwa hoja na sio matusi.karibuni
 
kwa hali halisi ilivyo na mambo yanavyozidi kuharibika huku kila kitu kikiwa disorganized, ccm wanajutia uteuzi walioufanya mwaka 2015.

kwa yeyote mwenye uelewa hana haja ya kuhoji kuwa wanajuta kwa lipi kwa sababu halihalisi anaiona.

Sina cha zaidi, kikubwa tuungane na nia ya Rais wetu ya kubadili noti ili tuanze kuneemeka
 
Hapo penye bei mbaya ya mazao umenigusa nimeuza mbaazi zangu kwa bei ya sh.500 kg1 ilianza bei ya sh.1300 imeporomoka mpaka kufikia sh500 kwa kg1

Utawala wa kikwete tuliuza 1500"1600" 2000" Mpaka kikwete anaondoka madarakani mwaka Jana tuliuza sh.1900" tukaishia sh.1800 kwa kg1
Acha uchochezi mara moja uta wekwa chini ya ulinzi na kufikishwa courtin[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji12]
 
Kuanzia Raisi John Magufuli aingie madarakani mpaka sasa sijaona chochote ambacho kimebadilika kwenye utawala wake chenye faida kwa mwananchi wa hali ya chini.
==> Demokrasia kukagandamizwa.
==>Raisi ameanza kuwagawa wananchi kwa kauli zake zinaudhi.
==>Mzunguko wa pesa umekuwa finyu na hivyo kusababisha hali kwa wananchi.
==>Kukosekana kwa ajira
==>Kupungua kwa maslahi kwa watumishi wa umma kutokana na kutopewa nyongeza ya mishahara na kupandishwa madaraja.
==>Hospital zimeendelea kukosa dawa kwa baadhi maeneo mengi nchini.
==>Uhaba wa baadhi ya mahitaji ya wananchi kama sukari.
==> Uhuru wa vyombo vya habari kuendelea kukandamizwa
==>Hali ya uchumi kuwa mbaya baada ya mizigo kuanza kupungua bandarini .
==> Watalii kupungua kuja Tanzania baada ya kuongezewa VAT kubwa.
==>Wananchi kurundukiwa mzigo wa kodi kwa mfano VAT kwenye miamala ya kibenki na miamala kwenye kampuni za mitandao ya simu.
Kwa maoni yako kuanzia raisi aingie madarakani nini kimebadilika?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom